Uzi wa wenye simu za iPhone

Uzi wa wenye simu za iPhone

Habari wajanja wa mujini,
Kama una simu ya iphone hebu tupia mambo mbali mbali ambayo iPhone inafanya ili tupate maujuzi.

Please kama una simu yako ambayo sio IPhone usichangine maana hii Habari ya Iphone tu wengine simu za Kariakoo pumzikeni kwanza

Isipotokea Sent by using iPhone tutaaminije sio Tekno wherever
 
iPhone imeshuka thamani sio kama miaka mitatu iliyopita,, watu siku hizi hawana shobo nazo,, k’koo kibao tu


Sent from my iPhone using JamiiForums

Version ipi mkuu, new au used? Kila simu ina latest version na old/outdated pia huwezi fananisha simu na mifano ya simu, heshima ya iphone haifananishwi na mapicha picha wachana na hizo used au version outdated!
 
Ukitaka kujua iphone ni ni angalia hii kitu hapa, achana na mapicha picha wereva[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Adjustments.JPG
 
Display za iphone anatengeneza samsung...
Sijui unaongea nini.....
Goodluck na hiyo powerbank yako
 
Labda ni Ushamba zamani nilikuwa nahisi iPhone ndio kila kitu kwa upande wa smartphones nikapania kuimiliki mwaka juzi mwishoni nikafanikiwa kumiliki 8+ nikagundua kwasisi wa nchi maskini ni ngumu kuimiliki smartphone aina hii
1. Aichangamani na smartphone nyingine za Operating system tofauti na IOS.
2. App zake nzuri nyingi ni za kununua na ni kwa mfumo credit cards ambao sio common kwetu.
3. Wamiliki wake ktk mazingira yetu ni wachache hivyo ni vgm kupata watu wa ku share vitu
4.Kutokana na mazoea ya Android kuna kaugumu kwenye kuitumia na kukubaliana na mfumo wake.
5.App developer wengi hawaipi Umuhimu kwahiyo Apps nyingi hawazifanyiwi updates kulinganisha na App hizo hizo kwenye Android OS mfano rahisi ni hii "Jamii Forum" kwenye iPhone ina muonekano wa nyuma sana ambao kwenye Android ni version za longtime kitambo.
6.Inahitaji uwe njema mfuko hakuna cha bure ringtone lipia,Movies,Music nunua.

Ila general overview
1.Huwezi kuta zina stuck hovyo hovyo km simu za Android hasa Tecnos and alikes
2.App zake ni super hakuna yale ma App ya Android unayo download then unakuta haifanyi kazi husika "planks"
3.Hakuna mambo Ads kwenye iPhone tofauti na Androids yaani uko makini unatengeneza muamala Mara unashangaa limeingia tangazo "Dr Rajabu mtaalamu wa mitishamba"
4.Kwa upande wa Hardware niseme wako vzr hii simu yangu ninayo tu home toka ninunue haimjui fundi ,charger yake na cable sijawahi badili lkn hapa ndani nina mzigo wa USB cable na charger tofauti za simu za Android.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom