Kwanza uelewe Mm KWA SASA sio mtumiani wa Huawei wala Iphone japo zote nishawahi kutumia kwa vipnd tofauti..... hivyo sipo upande wowote kati ya hizi brand mbili KWA SASA, natumia samsung ambayo kwa sasa haihusiani na hii quote.
Turudi kwenye mada.
Mzee baba ushasema MOVIE tena za KIZUNGU...
Je na yeye akisema MOVIE za KICHINA kwa hio huawei?
Mwingne akaja akasema MOVIE za kikorea kwa Samsung?...
Kila yule lazima atangaze chake au kumsaport mwenzake....
Tuzungumzie hili kwenye maisha ya kawaida....
Maana muvie ni maigizo pia zinatumika kutangaza bidhaa.... movie za mbele kila unachokiona kinatumika basi vingi ni for purpose, specifically bussines purpose.
Binafsi sibishi ya kua iphone ni moja ya brand kubwa sana ya simu, hilo halina ubishi linapelekewa na ubora wa simu zao, kuanzia hardware mpk software..
Apple-iphones ndio simu inaongoza kwa kuingiza mapato makubwa kuliko brand ngingne yyt ya simu duniani....
Nakubali kua iphones ndio brand ya simu inayotoa update kwa simu zao kwa mda mrefu...miaka 5 mda mwingne mpk 6.
Sasa turudi hapa....
Iphone inalalamikiwa na watumiaji hasa kwenye soko la ulaya ya kua...ikitoa update KUBWA mpya, hio update inaifanya simu ya zamani iwe slow KIDOGO kwa makusudi ili mteja ashawishike kununua new model...
Waweza usione utofaut kirahisi ila technically imekua proved hivyo na juzi juzi tuuu wamepigwa faini kwa hilo france.
Iphone inashika nafasi ya 3 kwa mauzo ya simu duniani....
Ikiongozwa na samsung then huawei ambaye anapanda kila mwaka huku samsung na iphone wakiwa wanashuka kimauzo kila mwaka....apple mpk akaamua kufanya discount kwa baadhi ya maeneo.
Hii tuu inaonesha ya kua iphone sio simu inayotumika zaidi duniani LABDA uniambie iphone flani ndio iliuzika sana mwaka flani kuliko MODEL yyt ya simu.
Mfn kwa mwaka jana katika mauzo ya simu zote iphone XR ndio aliongoza.... kwaio hapa anazungumzia model ya simu sio brand, ukija kwenye brand utazungumzia samsung then huawei....
Binafsi ukiniuliza kwa nn iphone baongozi kwa mauzo ya simu zote kwa ujumla... nitakujib ya kua moja ya sbb ni kwamba Hatoi model/matoleo mengi ya simu kama mfn samsung mwenye S-series, Note-series, A-series, J-series(imethitishwa) C-series(imethitishwa)n.k n.k kulingana na hali ya mteja... kuanzia wa juu, wa hali ya kati na wa hali ya chini. Iphone yy anatoa high end tu.. utapambana mwenyewe huko, ndio maana nchi zetu hizi wengi wanatumia za nyuma, refurb au mtumba sbb ya bei.
Huawei hazijazuiwa UK tena juzi tuu hapa wameofautiana na US kwa kitendo cha serikali ua UK kuingia ubia na Huawei wa kuwatenezea miundombinu ya 5G na kuruhusu Huawei ziendelee kuuzwa UK..
Ila sikatai ya kua iphone ndio brand maarufu zaidi UK
Huawei hatumii software copy ya ihpone...
Huawei anatumia android specifically EMUI kwa kuiongezea mbwe mbwe zake kuleta utofauti
Sent using
Jamii Forums mobile app