Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Ilani ya ACT–Wazalendo, Kutoa Ajira mpya milioni 10. Zitto asema CCM ilitekeleza 31% ya ilani ya mwaka 2015

CCM imeshindwa kutimiza Ahadi zake za 2015.

Zitto Kabwe

Chama cha Mapinduzi kiliahidi Wananchi ahadi kedekede mwaka 2015 kupitia Ilani yao. Hata hivyo utekelezaji wa Ilani Katika miaka 5 ni 31% tu hivyo kupata alama D. Baadhi ya maeneo ambayo CCM haikutekeleza Ilani ni Pamoja na

1. Ibara ya 20(h)(ii) CCM waliahidi Kukamilisha hatua za kuanzisha Akaunti ya Fedha ya Pamoja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. HAIJATEKELEZWA

2. Kwenye Sekta ya Kilimo Ibara 22(c) CCM waliahidi Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 461,326 mwaka 2014 mpaka 1,000,000 mwaka 2020. Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya Mwaka 2020 Eneo la Umwagiliaji ni Hekta 461,326. Bajeti ya Sekta ya kilimo ilikuwa Sh. 1.08T mwaka 2015, imeshushwa mpaka Sh 201 Bilioni Mwaka 2020.

3. Kwenye Sekta ya MIFUGO: CCM waliahidi Ahadi 17 (uk.10-20) hakuna hata moja iliyotekelezwa.

4. Kwenye Sekta ya Uvuvi kuna Ahadi 16 (uk. 21-22) hakuna iliyotekelezwa. Kwa Mfano waliahidi kununua Meli 5 za uvuvi Bahari Kuu na kujenga Bandari ya Uvuvi ukanda wa Pwani.HAIJATEKELEZWA.

5. Kwenye Sekta ya Viwanda CCM iliahidi Kuongeza mchango kwenye Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kutoka 9.9% mwaka 2015 mpaka 15% mwaka 2020 (uk.31). Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa Sekta ya Viwanda ilichangia 8.5% tu kwa Pato la Taifa. ( Hali ya Uchumi wa Taifa 2020, Wizara ya Fedha Uk. 3). Mradi wa Mchuchuma na Liganga Uk. 31 kama sehemu Ujenzi wa Viwanda mama. HAUJATEKELEZWA.

Hali ya Mauzo Nje kulinganisha Mwaka 2015 na Mwaka 2020

- Bidhaa za Viwanda Mwaka 2015 mauzo USD 1.4 Bilioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 800 Milioni
- Bidhaa za Maua na mboga mboga Mwaka 2015 Mauzo USD 960 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 174 Milioni
- Bidhaa za Samaki Mwaka 2015 Mauzo USD 402 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpak USD 155 Milioni

6. Kwenye Sekta Usafirishaji CCM waliahidi “Kwa ushirikiano wa Sekta Binafsi kuanza ujenzi wa reli zifuatazo:

Dar – Tabora – Kigoma
Uvinza – Msongati
Isaka – Kigali
Mtwara – Songea – Mbamba Bay (Mchuchuma na Liganga )”

Hata hivyo Serikali inatekelezwa hili kwa mikopp ghali.

7. Kwenye Sekta ya MAFUTA NA GESI ASILIA Ibara ya 44(d) CCM waliahidi Kuendeleza mradi wa Gesi (LNG) uk 71. Mradi huo HAUJATEKELEZWA.

8. Kwenye Sekta ya MAJI: CCM iliahidi Watu 85% kuwa na Maji safi na salama mwaka 2020, Lakini mpaka sasa ni 67% tu ya Watu Vijijini wanapata Maji uk.99. Waliahidi kujenga Bwawa la Kidunda, HALIJAJENGWA.

9. Kwa upande wa UWEZESHAJI wa Wananchi Ibara ya 57(d) uk.105 ya Ilani waliahidi kutenga Kiasi si cha Sh. 50M kwa kila Kijiji kama mfuko wa mzunguko (Revolving Fund). HAWAJATEKELEZA

10. Vile vile CCM waliahidi Ibara ya 57E(v) Kuanzisha mfuko mkubwa wa kitaifa wa wajasiliamali wadogo na wa kati kwa ushirikiano na mfuko wa hifadhi ya jamii. HAIKUTEKELEZWA. Badala yake Wampewa vitambulisho. Hata wanaotelekea nyanya chini wanatozwa pesa za vitambulisho.

11. Kwa upande wa AJIRA waliahidi kutengeneza Ajira Milioni Moja Katika miaka 5. ( uk. 4, 8, 9, & 10 )

Watanzania wana wajibu wa kuikataa CCM ifikapo Oktoba 28, 2020 na kuchagua ACT Wazalendo na Vyama vingine vya Upinzani ili kurejesha furaha kwenye nyoyo za Watanzania

Agosti 2020
 
ZZK na ACT Wazalendo ni wale wale vibaraka koko
Ulisaidia wezi ili ndege zetu zikamatwe na hata ukapinga Tanzania tusipiwe fedha kutoka Banki ya Dunia.
Bora ungetulia ukaomba dua labda Kigoma watakuonea huruma upate angalau ubunge .

Kaa kimya kijana Zitto na tulia kazi ya wakubwa inaendelea.

Rais wa Tanzania ni Mhe. Dr. Magufuli
 
Leo Chama cha ACT–Wazalendo kinazindua Ilani yake ya mwaka 2020 katika Hoteli ya Protea Courtyard. Pamoja na mambo mengine Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Bernard Membe na Mgombea Mwenza, Ndugu Omar Fakih Hamad watakabidhiwa ilani hiyo.

Tutawaletea kila kinachojiri hapa kwenye hii thread.

Karibuni.

======

UPDATES: 1112HRS

Mkutano unaanza muda si mrefu
View attachment 1553945

UPDATES 11:40

Maombi ya kufungua shughuli yanaendelea.

UPDATES 11:55

Sasa unasomwa muhtasari wa mambo 11 ambayo yapo kwenye Ilani.

Vipaumbele hivyo ambavyo ni pamoja na:-

-Ujenzi wa Demokrasia na utoaji Haki za watu

-Ufanisi na ubora wa Huduma za jamii

-Uchumi wa watu

-Uhuru kwa kila mtu

-Elimu bora ya Kivumbuzi bila malipo

-Kilimo cha kimapinduzi na mazingira wezeshi ya biashara

-Usawa na Ustawi wa Wanawake na Vijana

-Hifadhi ya Jamii kwa kila mtu/Afya bora kwa wote

-Ushirika wa kisasa kwa maendeleo jumuishi

-Haki za watu wenye ulemavu

-Maji safi, Salama na gharama nafuu

-Ajira mpya milioni 10

View attachment 1554042
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Bara. Tuko naye hapa kwenye Uzinduzi wa Ilani ya ACT–Wazalendo.

====
WEBIRO WASSIRA: KUWA MBUNIFU NI SAWA NA KUWA MHALIFU KWA TANZANIA

Webiro Wassira anayefahamika zaidi kama Wakazi, msanii ambaye pia ni mgombea ubunge jimbo la Ukonga kwa tiketi ya ACT-Wazalendo amesema serikali ya Tanzania haipo katika kukuza ubunifu kutokana na sheria ya Maudhui iliyopitishwa

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Ilani ya ACT- Wazalendo, amesema kumtaka msanii ambaye amefanya ubunifu kuwa na Tsh Laki tano ili kuiweka kazi yake YouTube itafanya wabunifu wadogo kushindwa au kuonekana wahalifu kwa kukiuka sheria

Maneno ya Wakazi yanashabihiana na wasanii wengi. Aidha Frank Mwakyembe anayefahamika kama Lugombo Makanta, aliwahi kusema sheria ya maudhui inaua ubunifu lakini pia inapoteza uwezo wa watu kujieleza kwa kuwa ili mtu kutuma maudhui anapaswa kutoa hela ya leseni

Akizungumza kuhusu Ilani yao, Wakzi ametambua umuhimu wa uwepo wa Sera ya Sanaa na wasanii ili kuwaweka wasanii katika mazingira mazuri na kukuza ubunifu

====

Mimi Webiro Wakazi Wassira, ni mwanachama Wa ACT Wazalendo, ni Mgombea Ubunge wa Jimbo wa Ukonga, ila kabla ya yote ni Msanii wa Hip Hop. Tuna changamoto nyingi sana kwenye tasnia yetu ya burudani, na mara zote ni aidha changamoto hizi hazishughulikiwi ipasavyo, hazishughulikiwi kwa wakati au hazishughulikiwi kabisa.

Nchi za wenzetu tumeona jinsi gani sanaa na burudani, na Michezo, vinavyoweza kuipatia nchi sifa na umaarufu, ila zaidi, kulipatia taifa pato la uhakika kutokana na ukusanyaji kodi, na hivyo kuwa sehemu ya ushamiri wa uchumi.

Ingawa serikali ya awamu ya tano imejisifu kuwa Kiwanda cha Sanaa na Burudani imechangia kwenye pato la Taifa kwa kiwango cha mabilioni, bado Serikali haijafanya uwekezaji unaostahili ili kujenga mazingira rafiki ya Wasanii kuweza kufanya shughuli zetu za sanaa kwa ufanisi na faida.

Bado hatuna sera ya sanaa. Bado hatujarasimishwa kwa kiwango cha kuweza kukopesheka benki, kuwa na mfuko wa hifadhi, na kupata Bima ya Afya. Miundo Mbinu na Mifumo ya usambazaji na uuzaji wa kazi zetu za sanaa bado ni duni. Udhibiti wa wizi wa kazi zetu za sanaa bado sio wa uhakika. Urasimu umeendelea kushamiri, na hii kwa miaka mingi ilipelekea Wasanii kuwa chini ya Wizara tatu (Tamisemi, Habari Sanaa Utamaduni Na Michezo, Viwanda na Biashara), na hata jitahada za kupunguza mlolongo huo zilizofanywa hivi karibuni, hazikutatua tatizo la msingi.

Cosota na Basata bado havina miundo mbinu ya kutosha kuweza kukidhi hitaji ya usimamizi wa Wasanii, ambao kwa sasa ni kila nyumba kuna msanii. (Nina uhakika hata viongozi wangu hapa, kama hamna mtu manyumbani kwenu ambae anataka kutoka kiusanii, basi pengine nyie wenyewe ndio Ma-underground ambao mnatafuta njia ya kutokea).

Cosota (iliyokuwa chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara) haina mfumo madhubuti, wala miundo mbinu ya kutosha kuweza kukusanya mirabaa nchi nzima. (Ndio maana kwa kusaidiwa na Maafisa Utamaduni wa mikoa na Wilaya, kukafanya baadhi ya shughuli zetu kuwa chini ya Tamisemi pia). Kuihamishia Cosota kwenye Wizara nyingine, wakati bado haijatengewa fungu la uendeshaji wa kazi zake, sio suluhisho la kudumu was la ulazima.

Na hivyo hivyo kwa BASATA. Haina uwezo kamilifu wa kujiendesha. Pia inajaribu kuwa kiranja wa Muziki wa kisasa na wa kibiashara, kwa kutumia Sera ya Utamaduni na Maadili. Jambo hili linaumiza ubunifu na kuinyima sanaa uhuru wake wa kuwa sanaa.

Sheria na Kanuni za Maudhui ya Mitandaoni, nazo zimeendelea kuonyesha kuwa, bado Serikali yetu haijali watu wa hali ya chini ilihali bado inajisifu kuwa serikali ya wanyonge. Katika Dunia ya sasa Internet ni Utility (ni huduma ya msingi ya kijamii kama ilivyo Umeme na Maji). Ila wabunifu wetu wamewekewa Tozo na Leseni tena za gharama ya juu pale wanapotaka kutumia Mitandao kuweka maudhui na kama njia mbadala za kujinadi, kiasi kwamba wabunifu wanaoanza (Start ups) watashindwa kukua kabisa. Sheria na Kanuni hizo zinadhihirisha kuwa UBUNIFU NI UHALIFU ndani ya nchi yetu.

Ni swala lililo wazi, kuwa hatuna viwanja bora vyenye viwango vya kimataifa vya kufanyia shughuli zetu za kisanii. Hapa naongelea Music Auditoriums, Entertainment and Sports Arenas, ambazo zinaweza kuboresha uzalishaji wa shows zetu, na hatimaye kuweza kutoa ushindani kwenye stage ya kimataifa. Pia ni fursa ya Ajira kwenye tasnia.

Pia tuna tatizo la kimikataba. Wengi wetu hatuna uelewa wa maswali ya kisheria, hivyo tumejikuta tunaingia kwenye mikataba kandamizi na makampuni pale wanapotaka kulipia huduma zetu, au wale ambao wana act kama aggregators (mtu kati) kwenye usambazaji wa kazi zetu. Tunafanya sana Kazi na makampuni ya Telecom na Beverages, na Imani yangu kuwa pengine Serikali yetu ingekuwa inawapa ruzuku au unafuu wa kodi makampuni yatakayo iwezesha Sanaa na Michezo kwa kiwango fulani, basi uwekezaji kwenye sanaa ungeongezeka na uchumi wa Wasanii ungeshamiri.

Mwisho kabisa, hatuna Academies za kukuza na kulea vipaji, wala programs kama vile karakana (workshops) ambazo zinaweza kutumika kuwaelimisha wasanii hasa wadogo juu ya mambo mbali mbali yahusuyo Sanaa, Utamaduni na Maadili ila vile vile, elimu ya biashara ya muziki (music business) na pia uelewa wa mambo ya fedha (financial Literacy). Tuna watu kama Hasheem Thabeet, Hassan Mwakinyo, Mbwana Samatta, ambao pengine hawajapitia Academy au walienda kwneye Academy binafsi, sasa jaribu kufikiria tutakuza Michezo kiasi gani ikiwa tutakuwa na academy za kutosha na kuzalisha mamia ya kina Hasheem, Samatta na Mwakinyo.

Tunahitaji Mkombozi. Na Ilani ya ACT Wazalendo ni dhahiri kuwa ndio Mkombozi wetu, maana imedhamiria kuinua sekta ya Sanaa, Burudani na Michezo kwa kuanza na maeneno muhimu kabisa yanayohitaji maboresho ya haraka. Academies za kukuza vipaji, Arenas za kufanyia maonyesho ya vipaji hivyo, na pia incentives kwa makampuni kuweza kudumisha uwekezaji kwenye vipaji hivyo. Ni Imani yangu kuwa chini ya Serikali ya KAZI NA BATA, sanaa na Michezo Vitakuwa, na pia Mimi na viongozi wangu hapa ambao I'm sure kisiri siri ni Wasanii, basi TUTATOKA. Asanteni sana

UPADETS: 12:54

Zitto Kabwe anazungumza;

CCM imeshindwa kutimiza Ahadi zake za 2015.

Chama cha Mapinduzi kiliahidi Wananchi ahadi kedekede mwaka 2015 kupitia Ilani yao. Hata hivyo utekelezaji wa Ilani Katika miaka 5 ni 31% tu hivyo kupata alama D. Baadhi ya maeneo ambayo CCM haikutekeleza Ilani ni Pamoja na

1. Ibara ya 20(h)(ii) CCM waliahidi Kukamilisha hatua za kuanzisha Akaunti ya Fedha ya Pamoja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. HAIJATEKELEZWA
2. Kwenye Sekta ya Kilimo Ibara 22(c) CCM waliahidi Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 461,326 mwaka 2014 mpaka 1,000,000 mwaka 2020. Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya Mwaka 2020 Eneo la Umwagiliaji ni Hekta 461,326. Bajeti ya Sekta ya kilimo ilikuwa Sh. 1.08T mwaka 2015, imeshushwa mpaka Sh 201 Bilioni Mwaka 2020.
3. Kwenye Sekta ya MIFUGO: CCM waliahidi Ahadi 17 (uk.10-20) hakuna hata moja iliyotekelezwa.
4. Kwenye Sekta ya Uvuvi kuna
Ahadi 16 (uk. 21-22) hakuna iliyotekelezwa. Kwa Mfano waliahidi kununua Meli 5 za uvuvi Bahari Kuu na kujenga Bandari ya Uvuvi ukanda wa Pwani.HAIJATEKELEZWA.
5. Kwenye Sekta ya Viwanda CCM iliahidi Kuongeza mchango kwenye Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kutoka 9.9% mwaka 2015 mpaka 15% mwaka 2020 (uk.31). Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa Sekta ya Viwanda ilichangia 8.5% tu kwa Pato la Taifa. ( Hali ya Uchumi wa Taifa 2020, Wizara ya Fedha Uk. 3). Mradi wa Mchuchuma na Liganga Uk. 31 kama sehemu Ujenzi wa Viwanda mama. HAUJATEKELEZWA.

Hali ya Mauzo Nje kulinganisha Mwaka 2015 na Mwaka 2020

- Bidhaa za Viwanda Mwaka 2015 mauzo USD 1.4 Bilioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 800 Milioni
- Bidhaa za Maua na mboga mboga Mwaka 2015 Mauzo USD 960 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 174 Milioni
- Bidhaa za Samaki Mwaka 2015 Mauzo USD 402 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpak USD 155 Milioni

6. Kwenye Sekta Usafirishaji CCM waliahidi “Kwa ushirikiano wa Sekta Binafsi kuanza ujenzi wa reli zifuatazo;

Ccm ni chama cha kitapeli
 
CCM ni chama cha kitapeli
 
Kuna budget za serikali kama uvuvi na kilimo hazijawai kufika 65% ya utekelezaji toka mwaka 2015.

Mfano Ni kiasi gani Cha pesa kimepotea kwa mfano chukulia Labda budget ya kilimo ni 200,000,000,000x( 35/100)= 70 bilion.

Yaani 70bil x5 = 350 bilion ndani ya miaka 5 je Ni ahadi kiasi gani zimekwama kwenye wizara zote na kiasi chake cha pesa ni kiasi gani?.

Yupo busy kununua mijidege ya kifisadi.
 
Makosa Ndio hasara hiyo??
..wewe inaelekea ni mgumu kidogo kuelewa.

..tafuta mahojiano ya Prof.Lipumba na waandishi wa gazeti la mwananchi.

..prof' ana uwezo mkubwa wa kueleza mambo ya kiuchumi kwa lugha rahisi, na amefafanua makosa ktk ununuzi wa ndege.
 
Afadhali hawa masultani wanakukuruka kuvuta wapiga kura kwa ilani,Chadema ilani yao inategemea lissu ameamkaje
Siku ya ufunguzi kasema atafuta vitambulisho vya machinga,kawe akasema atafuta tozo ya vitambulisho.Ni hatari sana kuwaamini hawa wasanii
 
Nimewahi changia uzi fulani humu kwamba ukitaka kuwakamata maccm na kujua walivyofeli chukua ilani yao afu tafuta wastani wa kile walichofanya kadiri ya ilani yao utakuta yoote yako chini ya 50% lakini ukiwaachia wawe wanajigamba mara tumejenga hospitali sijui madawa hutowaweza,mathalani waliahidi kituo cha afya kila kata na dispensari kila kijiji lakini kwa miaka yote 5 wamejenga na kukarabati vituo chini ya 500 sasa kati ya zaidi ya kata 3000 za Tzn unaweza ona ambavyo hawajafanya kitu chochote cha maana kujigamba.

Ukija kwenye barabara hivyo hivyo,ile ahadi ya kuuunganisha mikoa yote kwa lami hadi leo hii bado.

Kiufupi maccm ni jipu na maongo sana lakini kwa kuwa watu wengi ni wajinga hawajielewi ndio maana wanawachagua
 
Zitto anaenda kuwa KUB, zile dharau zote dhidi yake kutoka kwa lia lia FC sasa wataanza kumpigia magoti boss wao mpya.
Inategemeana na kura za ubunge overall hasa viti maalum. Kura za majimbo yote pemba nzima hazifikii kura za Jimbo moja la Mbeya mjini.

So CHADEMA ikipata hata wabunge 15 tu ina uhakika wa viti maalum walau 20 implying ACT inahitaji wagombea wake bara waokoteze kura kila jimbo.

2015 CUF ilikua na wabunge wengi majimboni kuliko CHADEMA ila viti maalum ndio vikawaua. Walikua hawana mtaji bara kabisa same to ACT!!

Otherwise waachiane majimbo
 
Wengi wanajua kupiga kura ni mfumo wa kimila na desturi, hata hawajui kufuatilia yaliyoahidiwa yanatekelezwa kwa asilimia ngapi na kipi hakijatekelezwa!

Hata ukiwauliza na kuwajuza wengine wanakushangaa kwa kusema maendeleo yanaletwa na juhudi za MTU binafsi na si kungoja serikali ikuletee maendeleo! Tena wengi huenda mbali kwa kusema ccm imewalea kwa amani na wanaamini vyama vingine in vya fujo fujo!

Hii changamoto ni kubwa vijijini kuliko mijini na asilimia 90 vijijini ndio wapiga kura maana wao kupiga kura ni desturi ya lazima kama kushiriki ktk misiba!

Tusichoke kutoa elimu, mabadiliko yaja!
 
ZZK na ACT Wazalendo ni wale wale vibaraka koko
Ulisaidia wezi ili ndege zetu zikamatwe na hata ukapinga Tanzania tusipiwe fedha kutoka Banki ya Dunia.
Bora ungetulia ukaomba dua labda Kigoma watakuonea huruma upate angalau ubunge .

Kaa kimya kijana Zitto na tulia kazi ya wakubwa inaendelea.

Rais wa Tanzania ni Mhe. Dr. Magufuli

Mpewe fedha za nn wakati kila kitu kinafanyika kwa pesa za ndani na pesa zipo?
 
Mimi nikiwa m/kiti wa serikali ya kijiji wallah wamenikata maini. Wanakijiji wananisakama kuwa nimekula Mill. 50 zilizoahidiwa na gombea wa CCM. Hawaamini kuwa hazijatolewa.
 
Inategemeana na kura za ubunge overall hasa viti maalum. Kura za majimbo yote pemba nzima hazifikii kura za Jimbo moja la Mbeya mjini.

So CHADEMA ikipata hata wabunge 15 tu ina uhakika wa viti maalum walau 20 implying ACT inahitaji wagombea wake bara waokoteze kura kila jimbo...

ACT wana uhakika wa majimbo 18 Pemba wakioteza na moja la bara la Zitto 19. CDM wataambulia bara majimbo 5 tena hapo wamepambana haswaa, Lissu mvuto umeshakufa na pesa ya amsha amsha hana hivyo usitegemee atapata kura nyingi za kuongeza idadi ya viti maalum CDM.
 
Back
Top Bottom