Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Ilani ya ACT–Wazalendo, Kutoa Ajira mpya milioni 10. Zitto asema CCM ilitekeleza 31% ya ilani ya mwaka 2015

CCM imeshindwa kutimiza Ahadi zake za 2015.

Zitto Kabwe

Chama cha Mapinduzi kiliahidi Wananchi ahadi kedekede mwaka 2015 kupitia Ilani yao. Hata hivyo utekelezaji wa Ilani Katika miaka 5 ni 31% tu hivyo kupata alama D. Baadhi ya maeneo ambayo CCM haikutekeleza Ilani ni Pamoja na

1. Ibara ya 20(h)(ii) CCM waliahidi Kukamilisha hatua za kuanzisha Akaunti ya Fedha ya Pamoja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. HAIJATEKELEZWA

2. Kwenye Sekta ya Kilimo Ibara 22(c) CCM waliahidi Kuimarisha kilimo cha umwagiliaji kwa kuongeza eneo la umwagiliaji kutoka hekta 461,326 mwaka 2014 mpaka 1,000,000 mwaka 2020. Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa ya Mwaka 2020 Eneo la Umwagiliaji ni Hekta 461,326. Bajeti ya Sekta ya kilimo ilikuwa Sh. 1.08T mwaka 2015, imeshushwa mpaka Sh 201 Bilioni Mwaka 2020.

3. Kwenye Sekta ya MIFUGO: CCM waliahidi Ahadi 17 (uk.10-20) hakuna hata moja iliyotekelezwa.

4. Kwenye Sekta ya Uvuvi kuna Ahadi 16 (uk. 21-22) hakuna iliyotekelezwa. Kwa Mfano waliahidi kununua Meli 5 za uvuvi Bahari Kuu na kujenga Bandari ya Uvuvi ukanda wa Pwani.HAIJATEKELEZWA.

5. Kwenye Sekta ya Viwanda CCM iliahidi Kuongeza mchango kwenye Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kutoka 9.9% mwaka 2015 mpaka 15% mwaka 2020 (uk.31). Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa Sekta ya Viwanda ilichangia 8.5% tu kwa Pato la Taifa. ( Hali ya Uchumi wa Taifa 2020, Wizara ya Fedha Uk. 3). Mradi wa Mchuchuma na Liganga Uk. 31 kama sehemu Ujenzi wa Viwanda mama. HAUJATEKELEZWA.

Hali ya Mauzo Nje kulinganisha Mwaka 2015 na Mwaka 2020

- Bidhaa za Viwanda Mwaka 2015 mauzo USD 1.4 Bilioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 800 Milioni
- Bidhaa za Maua na mboga mboga Mwaka 2015 Mauzo USD 960 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpaka USD 174 Milioni
- Bidhaa za Samaki Mwaka 2015 Mauzo USD 402 Milioni kufikia Mwaka 2020 imeshuka mpak USD 155 Milioni

6. Kwenye Sekta Usafirishaji CCM waliahidi “Kwa ushirikiano wa Sekta Binafsi kuanza ujenzi wa reli zifuatazo:

Dar – Tabora – Kigoma
Uvinza – Msongati
Isaka – Kigali
Mtwara – Songea – Mbamba Bay (Mchuchuma na Liganga )”

Hata hivyo Serikali inatekelezwa hili kwa mikopp ghali.

7. Kwenye Sekta ya MAFUTA NA GESI ASILIA Ibara ya 44(d) CCM waliahidi Kuendeleza mradi wa Gesi (LNG) uk 71. Mradi huo HAUJATEKELEZWA.

8. Kwenye Sekta ya MAJI: CCM iliahidi Watu 85% kuwa na Maji safi na salama mwaka 2020, Lakini mpaka sasa ni 67% tu ya Watu Vijijini wanapata Maji uk.99. Waliahidi kujenga Bwawa la Kidunda, HALIJAJENGWA.

9. Kwa upande wa UWEZESHAJI wa Wananchi Ibara ya 57(d) uk.105 ya Ilani waliahidi kutenga Kiasi si cha Sh. 50M kwa kila Kijiji kama mfuko wa mzunguko (Revolving Fund). HAWAJATEKELEZA

10. Vile vile CCM waliahidi Ibara ya 57E(v) Kuanzisha mfuko mkubwa wa kitaifa wa wajasiliamali wadogo na wa kati kwa ushirikiano na mfuko wa hifadhi ya jamii. HAIKUTEKELEZWA. Badala yake Wampewa vitambulisho. Hata wanaotelekea nyanya chini wanatozwa pesa za vitambulisho.

11. Kwa upande wa AJIRA waliahidi kutengeneza Ajira Milioni Moja Katika miaka 5. ( uk. 4, 8, 9, & 10 )

Watanzania wana wajibu wa kuikataa CCM ifikapo Oktoba 28, 2020 na kuchagua ACT Wazalendo na Vyama vingine vya Upinzani ili kurejesha furaha kwenye nyoyo za Watanzania

Agosti 2020
 
ZZK na ACT Wazalendo ni wale wale vibaraka koko
Ulisaidia wezi ili ndege zetu zikamatwe na hata ukapinga Tanzania tusipiwe fedha kutoka Banki ya Dunia.
Bora ungetulia ukaomba dua labda Kigoma watakuonea huruma upate angalau ubunge .

Kaa kimya kijana Zitto na tulia kazi ya wakubwa inaendelea.

Rais wa Tanzania ni Mhe. Dr. Magufuli
 
Ccm ni chama cha kitapeli
 
CCM ni chama cha kitapeli
 
Kuna budget za serikali kama uvuvi na kilimo hazijawai kufika 65% ya utekelezaji toka mwaka 2015.

Mfano Ni kiasi gani Cha pesa kimepotea kwa mfano chukulia Labda budget ya kilimo ni 200,000,000,000x( 35/100)= 70 bilion.

Yaani 70bil x5 = 350 bilion ndani ya miaka 5 je Ni ahadi kiasi gani zimekwama kwenye wizara zote na kiasi chake cha pesa ni kiasi gani?.

Yupo busy kununua mijidege ya kifisadi.
 
Makosa Ndio hasara hiyo??
..wewe inaelekea ni mgumu kidogo kuelewa.

..tafuta mahojiano ya Prof.Lipumba na waandishi wa gazeti la mwananchi.

..prof' ana uwezo mkubwa wa kueleza mambo ya kiuchumi kwa lugha rahisi, na amefafanua makosa ktk ununuzi wa ndege.
 
Afadhali hawa masultani wanakukuruka kuvuta wapiga kura kwa ilani,Chadema ilani yao inategemea lissu ameamkaje
Siku ya ufunguzi kasema atafuta vitambulisho vya machinga,kawe akasema atafuta tozo ya vitambulisho.Ni hatari sana kuwaamini hawa wasanii
 
Nimewahi changia uzi fulani humu kwamba ukitaka kuwakamata maccm na kujua walivyofeli chukua ilani yao afu tafuta wastani wa kile walichofanya kadiri ya ilani yao utakuta yoote yako chini ya 50% lakini ukiwaachia wawe wanajigamba mara tumejenga hospitali sijui madawa hutowaweza,mathalani waliahidi kituo cha afya kila kata na dispensari kila kijiji lakini kwa miaka yote 5 wamejenga na kukarabati vituo chini ya 500 sasa kati ya zaidi ya kata 3000 za Tzn unaweza ona ambavyo hawajafanya kitu chochote cha maana kujigamba.

Ukija kwenye barabara hivyo hivyo,ile ahadi ya kuuunganisha mikoa yote kwa lami hadi leo hii bado.

Kiufupi maccm ni jipu na maongo sana lakini kwa kuwa watu wengi ni wajinga hawajielewi ndio maana wanawachagua
 
Zitto anaenda kuwa KUB, zile dharau zote dhidi yake kutoka kwa lia lia FC sasa wataanza kumpigia magoti boss wao mpya.
Inategemeana na kura za ubunge overall hasa viti maalum. Kura za majimbo yote pemba nzima hazifikii kura za Jimbo moja la Mbeya mjini.

So CHADEMA ikipata hata wabunge 15 tu ina uhakika wa viti maalum walau 20 implying ACT inahitaji wagombea wake bara waokoteze kura kila jimbo.

2015 CUF ilikua na wabunge wengi majimboni kuliko CHADEMA ila viti maalum ndio vikawaua. Walikua hawana mtaji bara kabisa same to ACT!!

Otherwise waachiane majimbo
 
Wengi wanajua kupiga kura ni mfumo wa kimila na desturi, hata hawajui kufuatilia yaliyoahidiwa yanatekelezwa kwa asilimia ngapi na kipi hakijatekelezwa!

Hata ukiwauliza na kuwajuza wengine wanakushangaa kwa kusema maendeleo yanaletwa na juhudi za MTU binafsi na si kungoja serikali ikuletee maendeleo! Tena wengi huenda mbali kwa kusema ccm imewalea kwa amani na wanaamini vyama vingine in vya fujo fujo!

Hii changamoto ni kubwa vijijini kuliko mijini na asilimia 90 vijijini ndio wapiga kura maana wao kupiga kura ni desturi ya lazima kama kushiriki ktk misiba!

Tusichoke kutoa elimu, mabadiliko yaja!
 

Mpewe fedha za nn wakati kila kitu kinafanyika kwa pesa za ndani na pesa zipo?
 
Mimi nikiwa m/kiti wa serikali ya kijiji wallah wamenikata maini. Wanakijiji wananisakama kuwa nimekula Mill. 50 zilizoahidiwa na gombea wa CCM. Hawaamini kuwa hazijatolewa.
 

ACT wana uhakika wa majimbo 18 Pemba wakioteza na moja la bara la Zitto 19. CDM wataambulia bara majimbo 5 tena hapo wamepambana haswaa, Lissu mvuto umeshakufa na pesa ya amsha amsha hana hivyo usitegemee atapata kura nyingi za kuongeza idadi ya viti maalum CDM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…