Uchaguzi 2020 Uzinduzi wa Ilani ya ACT–Wazalendo, Kutoa Ajira mpya milioni 10. Zitto asema CCM ilitekeleza 31% ya ilani ya mwaka 2015

Jeshi la Chadema hapa JF! Kisheria hakuna muungano ni ushirikiano tu.....Nimeshaielewa campain strategy ya ushirikiano wa Chadema na ACT. Ni wazi Lissu ndiye ameshaachiwa uraisi wa jamhuri. Maalim Seif ameachiwa uraisi wa Zanzbar.

Membe yupo kimkakati kuendelea kuipa dozi CCM iliyogawanyika na kwa kunadi ilani yao nzuri ili kuisaidia ACT kupata wabunge kadhaa maeneo ya Kusini, Pwani na Kigoma huko.

Tatizo bado lipo kwenye kuachiana majimbo ya ubunge na udiwani tu. Sioni shida yeyote kwenye uraisi wa jamhuri na wa Zanzbar.
 
Hiyo ndio ladha ya ushindani wazee! Kila kukicha tuna la kujifunza!
 
Sijui huwa hamuelewi au Ni ujinga na Kila siku mzee baba anakwambia kabisa yet hapeleki pesa kwenye Jimbo la upizani
Serikali ya CCM haina ubaguziii kwenye suala la kupeleka maendedeo kwa watanzania. Arusha iringa mjini ubungo, mbeya kwa sugu, mbona maendeleo nimakubwa kwani hayo nimajimbo ya CCM?

Zito aseme tuuu kwamba hawezi ubunge, mkoa wa kigoma mpaka Leo pale kigoma mjini kwamiaka mingiiii, hapana mwakilishi wa maaanaa. Zito anatakiwa afungashiwe viragooo. Apishe wengine wenye nguvu.
 
CCM ya Magufuli, imemteua UBUNGE , aliekua mfungwa wa makenikia na mdeni wa NOAH zetu.
CHAMA CHA MIJIZI na MAFISADI PAPA.
 
Sishangai kwanini Makada wa chadema wapo kwenye huu uzi kumponda membe na act wazalendo. Wanajua, act ndio anaenda kua mpinzani mkuu bunge lijalo.

Act wazalendo imekaa kisomi sana lakini chadema imekaa kihuni.
 
ACT wamepata jabali zanzibar ila membe hata udiwani hashindi..
 
Anawalamba kichogo ccm,anawacheka maana ukikutana na kiongozi peke yake ukamwambia CCM hoyee huku unachekelea ,umejitafutia shida, hawapendi kuambiwa hivyo wakiwa kando.
 
Serikali ya ccm haina ubaguziii kwenye suala la kupeleka maendedeo kwa watanzania. Arusha iringa mjini ubungo, mbeya kwa sugu, mbona maendeleo nimakubwa kwani hayo nimajimbo ya ccm?...

Apishe watoa rushwa wa ccm?
 
Lissu ametua KIA na bombardier yetu, akifika Arusha atawaambia kuboresha miundo mbinu ni hasara 🤣
Bombardier yenu na nani mliyelima naye mbaazi mkapata pesa mkaenda kununua hiyo Bombardier. Naona hujui hata unachoongea.
 
Vitabu kama hivi huwa munatungiwa na nani? Huyu zito ndo hujidai kusoma vitabu sana, baada ya kusoma huwa anapata faida gani, kama anaandika ilani ya kijinga kiasi hiki? Ilani ni document serious, unawezaje kuiwekea maneno ya mitaani na upuuzi wa nyumbani kwako?
 
Hujajibu hoja hata moja zaidi naona unapuyanga tuu, bora wewe ndio ukae kimya..
 
Lakini siwameleta maendeleo?
Tuachane washuhudiaji wa matendo makuuu ya miujiza kama kiki ya kuhurumiwa uraisi kamakifuta machoziii.

Unasema Kigoma hamna kilichofanyika, kisha unasema si wameleta maendeleo, kama sio utoto ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…