Pre GE2025 Uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia - Singida, 10 Januari, 2024

Pre GE2025 Uzinduzi wa kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia - Singida, 10 Januari, 2024

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa mkoa Singida:
Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hii sisi wanasingida tulianza kufanya maandalizi.
Ofisi ya mkuu wa mkoa imekuwa ikitoa ikitoa huduma za kisheria kwa kushirikiana na TLS.
Tumekuwa tukitoa msaada wa kisheria kwa kushirikiana na taasisi takribani 9.

Tumejipanga vizuri maana tupo na watoa huduma sehemu mbalimbali mkoani singida.
Kampeni hii kwetu ni fursa.
Kampeni hii itakuwa chachu ya maendeleo katika mkoa wetu. Imani yetu kuwa kampeni hii itaweka mazingira ya kuwafanya wananchi wasiwe na hofu.
Ofisi yangu ilipewa taarifa kuwa msisitizo utakuwa katika
Haki za wanawake na watoto, Utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala nk.

Mkoa wa singida umeendelea kuunga mkono hatua za Rais za kuondoa unyanyasaji wa kijinsia.
Kuzindua kampeni hii ni uthibitisho tosha kuwa Rais anapenda haki. Haki huinua taifa. Tunampongeza mh. Rais.

Baada ya uzinduzi wa kampeni hii utekelezaji wa kampeni hii utakiwa wa kiwango.
 
Mhe. Balozi Dkt. Pindi Hazara Chana Waziri wa Katiba na Sheria:
Nawasalimu kwa Jina La Tanzania.
Nashukuru kwa heshima mliyonipa ya kuzindua kampeni ya kisheria ya Mama Samia.
Hii ni Kampeni ya Kisheria ya Mama Samia.
Rais wetu kila idara, wizara ameacha alama. Alielekeza wizara kuwa piteni kwa watu wote.
Ndizo zile 4R anazozisema Rais.

Dr. Samia Suluhu Hassani Oyee.

Kwa Kweli Rais wetu tunamshukuru sana sana.
Mkoa wa Singida ni mkoa wa sita.

Kampeni hii ya msaada wa kisheria inatoka na adhima ya rais ya kutaka kila mwananchi anapata msaada wa kisheria. Haya ni maelekezo maalum ya Mh. Rais. Ametutuma.
Imefika wakati kila mtanzania atambue anapohitaji jambo ajue wapi anatakiwa kwenda.

Serikali yetu imetuwekea miundombinu kila sehemu. Kule kijijini usiogope kumuona mtendaji wa kijiji.
Wakuu wa wilaya wametenga kila wiki kuwasikiliza wananchi. Ili Maswali yao hoja zao ziweze kupata majibua.

Serikali inawafuata wananchi sehemu walipo. Tusiache kutumia ofisi zetu.
Mh. Ametuelekeza msaada wa kisheria unatolewa kwa watu wote bure. Wale wenye maswali ya kuuliza yapo madawati ya kijinsia tumeyaweka kwenye vituo vya polisi.

Baada ya kuzindua tupo imara.
 
Nisisahau kuwashukuru viongozi wa dini. Wanasema shika amri ya Mungu (Usiue, Usiibe).
Lakini kwetu tunakuwa na vifungu vya sheria. Ukienda kinyume tunakutandika magerezani.
Tunataka watu waishi kwa amani wafurahi. Tanzania tunataka iwe ni kisima cha amani tupendane.

Wanasingida Hodi hodi tumekuja.
Watu wenye maswali yao wenye hoja zao karibuni tuyajenge.

Tunahakikisha wanachi wanafikiwa kwa msaada wa kisheria.
Wanachi waweze kufanyakazi kwa uhuru na kwa haki.
Rais anataka kuona kuwa Tanzania inakuwa tulivu na yenye amani. Kuona watanzania wanajua Haki zao na Wajibu wao. Siyo haki tu lakini na wajibu wa kutii sheria pasipo shurti.

Kila mtu akijua haki zake na wajibu wake tutaleta maendeleo.
Huu ni wakati wa haki na Amani kwa ustawi wa Mtanzania.

Nimepewa dhamana ya kutekeleza majukumu kuhusu masuala ya kisheria. Kuhakikisha wananchi wanapata haki kwa wakati.
Usichukue sheria mkononi. Tufuate utaratibu. Tunaye mtendaji wa Mahakama Ole Gabriel.
Hivi karibuni tulikuwa kwenye mkutano wa 77 wa mkutano wa haki.
Mkutano wa 77 wa haki za binadamu haufanyiki tu nchi zozote. Nchi zingine hazina amani.
Tanzania tumeendelea kuwa mfano bora.
 
Tanzania ilipitisha sheria za msaada wa kisheria kwa watu wasio na uwezo. Huduma bure.
Kupitia sheria hii huduma za msaada wa kisheria unaratibiwa na Wizara ya Katiba na sheria.
Maeneo ya pembezoni na ya ndani ndani tunataka watu msaada huu uwafikie.

Tupo na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa.
Mpango huu wa Mama Samia Legal Aid. Mama samia anawafikia wote. Ilani ya CCM inaelekeza kuimarisha msaada wa kisheria hususani kwa wanawake.

Wanawake na watoto hili ni kudi moja wapo mahususi. Wakina mama lazima wawe na amani pamoja na akina baba.
Kupitia kampeni hii tuna hakikisha kuwa inakidhi matamanio ya Mh Rais.
Mh. anapenda kuona Tanzania ninaendelea kuwa nchi ya amani.

Hatutaki mtu akiwa na shida anataka kwenda sehemu lazima kuwe na connection.

Ni lazima uzijue haki zako.
 
Jane Matinde: Mwenyekiti
Kampeni ya msaada wa kisheria imeanza mwaka jana.
Tumeshuhudia:-
Ushirikiano kwa watoa huduma za kisheria
Msaada wa kisheria sasa umekubalika. Wasaidizi wa kisheria wameweza kupata majengo kwenye ofisi za serikali.
Kufikisha msaada wa kisheria maeneo ambayo hawezi kufikiwa.
Migogoro mingi imeweza kufikiwa.
Kuweza namna ya kufikia maeno mengi zaidi.
Majadiliano ya kina na endelevu ya kisheria.
Kuona namna gani mfuko unaweza kuanzishwa (Majadiliano yanaendelea)
Gd
 
Wizara yangu imejipanga kuhakikisha kuwa kampeni hii inawafikia watu wote.
Naungana na Mh kuwa HAKI HUINUA TAIFA

Maeneo mengi sana kuna ukatili wa kijinsia. Tutoe taarifa (Katika taasisi na katika familia)
Kuongeza uelewa masuala ya miradhi.
Utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala.
Tanzania imekuwa ikipata sifa nzuri kwenye maswala ya haki za binadamu na watu.

Kupitia mh Rais tumekuwa na maboresho ya sheria mbalimbali.
Tunaendelea kumshukuru sana Mh. Rais.

Ni adhima ya serikali hii kuendeleza sifa hizi njema za kuzingatia utawala wa sheria.
Kwa wananchi wasio na uwezo ni kujenga jamii iliyo sawa mbele ya sheria.

Nchi yetu ni kubwa na idadi ya watu ni kubwa. Zipo jitihada kubwa za kuleta msaada wa kisheria.
Kulinda haki za wanawake na watoto.

Hivyo huduma ya msaada wa kisheria zinaendelea kutolewa na serikali na wadau mbalimbali.

Kila mtanzania analo jukumu la kusimamia haki za binadamu na kutii sheria bila shurti.

Wanachi wanatakiwa kuelimishwa. Tuna sheria lakini wananchi wanatakiwa kuelimishwa. Ndio maana tupo hapa. Wananchi wanatakiwa kuelimishwa kuhusu haki za binadamu
 
Unyanyasaji wa wanawake siyo mila. Tunatakiwa kuheshimu sheria. Vyombo vya habari mnaendelea kuripoti tunawashuru. Muendelee kutuletea habari hizo.

Jeshi la polisi linatusaidia kuchunguza na kupeleleza tuna wapongeza.
Tuendelee kuboresha sheria zetu ili ziendane na wakati hususani maswala ya kiteknolojia.

Mahakama zetu tupo katika hatua za kiteknolojia. Katika wilaya 139 wilaya 135 ofsi zetu zipo. Tupo na huduma ya mahakama inayotembea huko Mwanza.

Kampeni hii imeanza kutekelezwa April 2023. Imeweza kufikia mikoa 5.
Takwimu zinaridhisha
 
Kila siku hafla+matamasha
Tu mwisho wa siku hamna lolote
Kinachofanyika,
Ehe wasani gani hapo wapo wana perform

Ova
 
Kampeni imewezesha wananchi wengi wengi kujua masuala ya kisheria. Wananchi wameelewa kuhusu masuala ya Mirathi na wosia.

Rais ametueleze kuwahamasisha wananchi kuwa wawe na vyeti vya kuzaliwa. Chetu che kuzaliwa ni haki yako.
Tujitahidi kila mtoto awe na cheti cha kuzaliwa.

Naomba kutoa wito
Natoa wito kwa viongozi wa dini (Viongozi wa dini wamekuwa wakiendelea kukemea vitendo viovu)
Nawaomba muendelee kufanya hivyo.
Wandishi wa habari mjipange muhakikishe wananchi wanapata haki na muendelee kuibua changamoto mbalimbali.
Wanasiasa wenzangu tuendelee kumuunga mkono Mh. Rais ili kuhakikisha ukatili unaondoka katika jamii zetu.
Asasi za kiraia nawashukuru, serikali inawatambua.
Niwaombe viongozi wenzangu muwape ushirikano wa kutoka kwa wanaotoa msaada wa kisheria kutoka asasi za kiraia.
Polis wanahakikisha watuhumiwa wanapatikana nawapongeza sana. Watuhumiwa wanapotoroka wananchi tuwafichue.

Nichukue nafasi kumshukuru mkuu wa mkoa wa singida.
Kwenye bila mipango endelevu kampeni hii itafikia mwisho. Lazima iwe sustainable.
Msaada wa kisheria ukiwepo Amani na Maendeleo yanapatikana.

Mwisho niwaombe wananchi wote mjitokeze kwa wiki kwa kipindi tutachokuwa mkoa wa Singida.
 
Baada ya kusema maneno haya tunakwenda kuzindua. DJ weka mambo watu wafurahie.
Naomba kutangaza Rasm Utekekezaji wa Mama Sami Legal Aid mkoa Singida Imefunguliwa Rasmi
 
Back
Top Bottom