GE2025 Uzinduzi wa Kampeni za CCM Viwanja vya Kawe, Agosti 28, 2025

GE2025 Uzinduzi wa Kampeni za CCM Viwanja vya Kawe, Agosti 28, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
🔥 KAWE KUMEWAKA! 🔥
Leo viwanja vya Kawe vimepamba moto kwa ujio wa kampeni za Mama Samia. Umati wa watu umefurika kwa shangwe na hamasa kubwa, kijani na njano zimelipamba jiji kwa upekee. 🌟🇹🇿
Ni wazi kabisa muitikio ni mkubwa mno, wananchi wameonyesha mapenzi, mshikamano na imani thabiti kwa safari ya maendeleo tunayoiendea pamoja.

💚💛 Hii ni ishara kuwa safari imeanza kwa kishindo – na kweli HAIJAPATA KUTOKEA!

#tukawashangaze
#haijapatakutokea
 

Attachments

  • 39294D5B-5B62-440D-8055-CA13D11508EE.jpeg
    39294D5B-5B62-440D-8055-CA13D11508EE.jpeg
    311.2 KB · Views: 27
Sasa utakusanyaje watu nchi nzima kama huna pesa?
Watafika je huko Kawe bila pesa?
Hebu jiulize kwa mujibu wa statement yako
Umejibu tusichokijadili... Uwanja kujaa majivuno yake ni kama hao watu wametoka hapo Bonyokwa na buza kumbe wamesombwa toka nchi nzima.

Ingekuwa ni watu wa Dar tu, basi kujisifu kungekuwa halali!
 
Ukitaka kujua CCM imepoteza ushawishi angalia viongozi wa dini waliotumwa,Imagine Mufti katuma muwakilishi (how on earth is that possible) yaani hakuandaliwa au? Kwa upande wa TEC hakuna muwakilishi kabisa Wala CCT, Viongozi wa dini walioalikwa ni Mch Hananja na Mwamposa jamani Kuna kitu hakiko sawa
 
Katika uzinduzi wa kampeni za CCM Tanganyika Packers hatuoni uwakilishi wa Kanisa Katoliki Tanzania , Uwakilishi wa Kanisa La Kilutheri Tanzania, Uwakilishi wa Kanisa La Anglikana, TAG n.k

Hii siyo kawaida pengine Kanisa limeamua kujitenga baada ya kuona yanayofanyika siyo sawa.

Hata Mufti hajafika kaamua katuma muwakilishi, zaidi tunamuona Mwamposa Jukwaani.

Anyway hii siyo sawa na lazima Sa100 ajitafakari sana! Mbele hakuna nuru kumejaa giza.
 
Rais Samia Suluhu Hassan Mwaka 2025 CCM imejipanga vijana watoto na wazee oktoba nikutiki tu #Haijapatakutokea #tukawashangaze
 
Katika uzinduzi wa kampeni za CCM Tanganyika Packers hatuoni uwakilishi wa Kanisa Katoliki Tanzania wala Uwakilishi wa Kanisa La Kilutheri Tanzania, hii siyo kawaida pengine Kanisa limeamua kujitenga baada ya kuona yanayofanyika siyo sawa.

Hata Mufti hajafika kaamua katuma muwakilishi, zaidi tunamuona Mwamposa Jukwaani.

Anyway hii siyo sawa na lazima Sa100 ajitafakari sana! Mbele hakuna nuru
Ambacho hukijui ni hiki, hakuna Mwanaccm anayeogopa Mungu
 
JamiiForums huwa mnakera sana zikifika nyakati hizi za kampeni. Mna tabia za kuunganisha nyuzi jinsi mnavyotaka nyie, huu ubabe siyo sawa. Mwisho wa siku mtaachiwa majukwaa yenu mposti thread mnazozitaka nyie
 
Katika uzinduzi wa kampeni za CCM Tanganyika Packers hatuoni uwakilishi wa Kanisa Katoliki Tanzania , Uwakilishi wa Kanisa La Kilutheri Tanzania, Uwakilishi wa Kanisa La Anglikana, TAG n.k

Hii siyo kawaida pengine Kanisa limeamua kujitenga baada ya kuona yanayofanyika siyo sawa.

Hata Mufti hajafika kaamua katuma muwakilishi, zaidi tunamuona Mwamposa Jukwaani.

Anyway hii siyo sawa na lazima Sa100 ajitafakari sana! Mbele hakuna nuru kumejaa giza.
Hukumbuki kwamba dini inatakiwa isifungamane na siasa!
 
''Tutaanza rasmi kutekeleza sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Kwa kuanzia, ndani ya siku 100 tutazindua rasmi Mfumo wa Taifa wa Bima ya Afya kwa Wote kwa awamu ya majaribio, tukianzia kwa wazee, watoto, mama wajawazito na watu wenye ulemavu. Gharama za matibabu kwa makundi haya zitabebwa na Mfuko wa Taifa wa Bima''.

2. ''Serikali itaanza kugharamia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo kwa magonjwa yasiyoambukizwa, ikiwemo saratani, figo, moyo, sukari, mifupa na mishipa ya fahamu. Haya ndiyo magonjwa yenye gharama kubwa na ambayo wananchi wasio na uwezo wamekuwa wakishindwa kumudu gharama zake''.

3. ''Kuanzia sasa ninapoongea ni marufuku hospitali yoyote nchini kuzuia miili ya marehemu kuchukuliwa na ndugu zake hata kama gharama za matibabu za matibabu aliyopatiwa marehemu hajazilipwa''.

4. ''Serikali itaajiri wahudumu wa afya wapya 5,000, wakiwemo wauguzi na wakunga, ili kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto''.
5. ''Tutaanda mkakati madhubuti na ya kisanyansi kuhakikisha kila mtoto wa darasa la tatu anaweza kusoma, kuhesabu na kuandika bila shida''.

6.'' Tutazindua mkataba (National Skills Compact) wa kitaifa wa ujuzi kwa viwanda – mpango wa pamoja kati ya waajiri, vyuo vya ufundi stadi (TVETs) na vyuo vikuu kwa lengo la kulinganisha mafunzo na mahitaji ya sekta kipaumbele, kuanzia na nishati, TEHAMA, na viwanda vya kuongea thamani''.

7. ''Tutaajiri walimu wapya 7,000 wa masomo ya hisabati na sayansi''.

8.'' Nitazindua Mfuko wa Ajira kwa Vijana na Wanawake wenye wa thamani ya shilingi bilioni 200 ili kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya biashara ndogo na za kati na kuwezesha uendeshaji wa kampuni changa''

9. ''Nitazindua programu maalum ya kurasimisha sekta isiyo rasmi kwa mama lishe, usafiri na usafirishaji na wajasiriamali wadogo''.

10. ''Tutaanzisha programu maalum ya ujenzi wa mitaa ya viwanda kwa kila wilaya yenye kulenga kuzalisha ajira kwa watanzania kupitia kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi, madini na misitu, pamoja na vifaa vya ujenzi''.

11. ''Tutaanza utekelezaji wa Gridi ya Taifa ya Maji kwa lengo la kuwa na vyanzo vya uhakika vya maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, kilimo, mifugo na biashara. Gridi ya Taifa ya Maji itahusisha vyanzo vikubwa vya maji kutoka maziwa: Victoria, Tanganyika, na Nyasa, pamoja na mito mikubwa nchini''.

12.'' Tutazindua miradi ya haraka ya nishati, ikiwemo umeme vijijini kwa kutumia nishati jadidifu (solar, wind), nishati safi ya kupikia. Hatua hii itapunguza utegemezi wa kuni na mkaa na kuhifadhi mazingira''.

13.'' Kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami na zege katika maeneo ya mijini na vijijini''.

14. ''Tutaanzisha mfumo rafiki ya uwajibikaji ambapo mawaziri, wakuu wa mikoa na watendaji wengine wa serikali watatoa taarifa na kujibu maswali kutoka kwa wananchi kwa njia ya kidijitali na SMS bure''.

15.'' Kuanzisha mazungumzo ya wadau wakiwemo asasi za kiraia, viongozi wa dini, wafanyabiashara na vyama vya siasa ya kuhuisha na kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya''.

Mungu Ibariki Tanzania. Mungu Ibariki Afrika.
 

Attachments

  • aaa1.jpeg
    aaa1.jpeg
    231.8 KB · Views: 31
  • aaa2.jpeg
    aaa2.jpeg
    184.3 KB · Views: 30
Back
Top Bottom