Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni chama cha siasa kikongwe, kilichojijenga kitaasisi, chenye muundo mpana na ulioenea kote nchini. CCM ndicho chama chenye wanachama wengi zaidi kuliko chama chochote hapa nchini, na ndicho kinachobeba historia na mustakabali wa Taifa letu.
Mathalani, katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee CCM ina mashina 8,918, matawi 762, kata 102 na jumla ya wanachama 1,237,810, huku kikiongoza kwa zaidi ya asilimia 90 ya mitaa yote 565 ya kiserikali jijini Dar es Salaam.
View attachment 3455041
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM, kwa upande wa mijini kila shina huwa na wanachama 100 na zaidi. Tukizingatia kuwa kila shina lina viongozi 5 (Mwenyekiti, Katibu na wajumbe 3), iwapo kila shina litawaleta wanachama 30 tu kushiriki mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM tarehe 28 Agosti 2025 katika viwanja vya Tanganyika Packers - Kawe, basi idadi ya wanachama watakaoshiriki itafikia 267,540.
Idadi hii ya watu ni kubwa zaidi ya uwezo wa kujaza Uwanja wa Benjamin Mkapa mara nne, na bado italazimu kutumia viwanja vya Azam Complex na KMC Complex kwa wakati mmoja au mahema 40 makubwa ya Arise and Shine kwa Mtume Buldoza Mwamposa ili kutosheleza wingi huo.
Kwa wale vibaraka na wazandiki tuwajulishe tu kwamba CCM ni chama kikubwa, CCM imetimia na Uwanja wowote Dar es Salaam tunaujaza na kumwagika.
Shime wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM Twendeni Tanganyika Packers Kawe tarehe 28/08/2025 tukaiandike historia ya kuianza safari ya ushindi wa kishindo pamoja. Tuwapelekee ujumbe wale wote wasiotutakia mema na vibaraka wa CCM na Taifa letu kuwa watasubiri sana – CCM ni Madhubuti, itaendelea kushinda na kulinda heshima ya Tanzania.
Kazi Na Utu, Tunasonga Mbele.
#CCMImetimia
#TwendeNaSamia2025
#SafariYaMaendeleo
#SafariYaUshindi
#DarTupoTayari
MASIGA GA
0738969820
Raia Mwema