Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua Shamba la Miti Chato kesho Januari 27, 2021 katika eneo la Butengo, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita.
Wananchi maeneo husika pamoja na wananchi wote mnakaribishwa kuhudhuria hafla hii ya kihistoria kwa nchi yetu. Hafla hii inatarajiwa kuanza saa kumi na mbili asubuhi.
SHAMBA la Miti Chato ni miongoni mwa mashamba ya Serikali yaliyoanzishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika mwaka wa fedha 2017/18.
JANUARI 12, 2021 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro alitangaza Chato kuwa Kitovu cha uhifadhi na utalii katika Kanda ya Ziwa alipokuwa katika ziara ya kikazi shambani hapo.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017/2018(miaka minne iliyopita) shamba hili limepandwa jumla ya miche 7,449,255 kwenye hekta 2,682(sawa na ekari 6,705).