Uzinduzi wa shamba la miti Chato kesho, Rais Magufuli kuwa mgeni Rasmi

Uzinduzi wa shamba la miti Chato kesho, Rais Magufuli kuwa mgeni Rasmi

View attachment 1686608

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua Shamba la Miti Chato kesho Januari 27, 2021 katika eneo la Butengo, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita.

Wananchi maeneo husika pamoja na wananchi wote mnakaribishwa kuhudhuria hafla hii ya kihistoria kwa nchi yetu. Hafla hii inatarajiwa kuanza saa kumi na mbili asubuhi.

SHAMBA la Miti Chato ni miongoni mwa mashamba ya Serikali yaliyoanzishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika mwaka wa fedha 2017/18.

JANUARI 12, 2021 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro alitangaza Chato kuwa Kitovu cha uhifadhi na utalii katika Kanda ya Ziwa alipokuwa katika ziara ya kikazi shambani hapo.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017/2018(miaka minne iliyopita) shamba hili limepandwa jumla ya miche 7,449,255 kwenye hekta 2,682(sawa na ekari 6,705).

View attachment 1686589
Hili shamba limeanzishwa kwenye uongozi wa JPM. It tells all.
 
Ni vizuri tutunze mazingira maana kama hapa Dsm hiyo miti itapandwa wapi tuache wivu jamani
 
Hivi mawaziri wake kazi ni nini. Hata msitu anafungua mzee baba. Mimi nilidhani uchaguzi umeisha kampain sasa basi kumbe ni yale yale. Hapa swali ni ana mpango wa kugombea tena au ni hulka tu ya kutaka sifa na utukufu ziende kwake tu.
 
Mkuu, wengi wa watu wa Kitanzania, hawajawahi kujua wakitakacho hivyo, wewe wasikupe homa.

Uko sahihi sana, ndio maana bado nchi yetu ni masikini sana, maana kuanzia viongozi hadi wananchi hawajui wanataka nini. Mfano mrahisi sana, wakati wa JK tulikuwa tunaimbishwa umeme wa gas kwani umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi na watu wakaamini. Lakini sasa hivi tumejikita kwenye umeme wa maji na tatizo la mabadiliko ya tabia haliongelewi na ujenzi wa umeme wa maji unaitwa uzalendo! Kichekesho ni kuwa kundi lililosifia umeme wa gas, ndio hilo hilo linasifia wa maji sasa!
 
View attachment 1686608

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua Shamba la Miti Chato kesho Januari 27, 2021 katika eneo la Butengo, Wilaya ya Chato, Mkoani Geita.

Wananchi maeneo husika pamoja na wananchi wote mnakaribishwa kuhudhuria hafla hii ya kihistoria kwa nchi yetu. Hafla hii inatarajiwa kuanza saa kumi na mbili asubuhi.

SHAMBA la Miti Chato ni miongoni mwa mashamba ya Serikali yaliyoanzishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika mwaka wa fedha 2017/18.

JANUARI 12, 2021 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Damas Ndumbaro alitangaza Chato kuwa Kitovu cha uhifadhi na utalii katika Kanda ya Ziwa alipokuwa katika ziara ya kikazi shambani hapo.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017/2018(miaka minne iliyopita) shamba hili limepandwa jumla ya miche 7,449,255 kwenye hekta 2,682(sawa na ekari 6,705).

View attachment 1686589
Ama kweli Chato kilikua kichaka ila pesa imefanya uwe mji sasa.....
 
Kacovid kameshawasili Chattle! Na katazidi kushamiri kwa sababu ya ziara za voingozi mbalimbali.

Safari hii ukweli ndio utatunusuru, hakuna janjajanja

Sio maombi tena?
 
Nadhani pia kesho mtumishi wa Mungu aliye hai, atatoka na njia nzuri tena na mwongozo sahihi kuhusu Naroko!!

Mungu wa mbingu na nchi, ni kwako tu kwenye msaada kututoa ktk majanga ya kidunia, Iponye Tanzani na watu wake,Mungu mwenyezi, Iponye pia Dunia yote na watu wake, Amen
 
Naona vijana tuwahi fursa Chato, Mississippi ya Africa!.,pale kwa bibi kufanane na Chato
 
Hivi prezdent katika kipindi hiki cha new_more_near hana issue za kufanya kutuletea chanjo? Mambo ya kuzindua miti angewaachia watendaji wa kata au vijiji.
 
Back
Top Bottom