Fredrick Nwaka
Member
- Jul 8, 2013
- 53
- 75
UZINGATIVU WA JINSIA: MFUMO DUME BADO KIKWAZO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII
Utamaduni wa mfumo dume katika jamii umeelezwa ni mojawapo ya sababu za kutozingatia uandishi wa masuala ya kijinsia katika kuripoti habari wakati huu ambao idadi kubwa ya vijana nchini Tanzania wakitumia mitandao ya kijamii ikiwemo Instagram, X na Facebook kufanya uandishi wa kiraia.
Mwandishi wa habari na mtangazaji wa shirika la utangazaji Tanzania TBC Sabina Nabigambo amesema mfumo dume bado unasalia kuwa kikwazo kwa jamii katika kuzingatia masuala ya jinsia. “Kuna muitikio mdogo na bado kuna mfumo dume upo na kukandamiza nafasi ya mwanamke, vijana wanaofanya uandishi wa kiraia citizen journalism wengi ni wanaume na hata wanavyoaddress wanawake wanazingatia mfumo huo.
Lakini kama wanawake wangekuwa wengi huenda wangeleta mabadiliko,” amesema Sabina akisisitiza huenda ongezeko la wanawake kwenye nafasi za maamuzi ukachochea msukumo wa wanawake na kupunguza daraja lililopo katika uzingativu wa kijinsia.
Naye, Simon Binamungu, mwanafunzi wa Chuo cha madini Shinyanga ambaye hutumia zaidi mtandao wa Instagram amesema anaona mwamko wa wanawake katika kuzingatia jinsia hususani wakati huu wa uandishi wa kiraia licha ya changamoto ya mfumo dume ambao bado haujampa nafasi mwanamke kwa kiwango kikubwa.
Takwimu za mtandao wa We Forum zinaonyesha kuwa aslimia 24 pekee ndizo zinazozingatia uandishi wa habari za jinsia kwa wanawake katika mitandao ya kijamii.