Uzinzi na ulevi ndio sababu ya Watanzania wengi kuwa maskini na mafukara

Uzinzi na ulevi ndio sababu ya Watanzania wengi kuwa maskini na mafukara

Halafu mbaya zaidi ni kua vinamaliza hela huku vikimfanya muathirika ajione ye ndo yeye. Halafu ghafla tu anashangaa haelewi
 
Hivi vitu viwili vikikutawala haswa hata ukiwa Meneja unaweza kupitwa kimaendeleo na dereva wako.

Mifano ni mingi mno, hata msomaji bila shaka una mfano wako jinsi ulevi wa pombe na uzinzi ulivyowaharibia watu.
Kijana mwenzangu please weka kando uzinzi na ulevi, kisha tazama matokeo.

Unaweza kuona umeendelea kumbe ulipaswa kufika mbali zaidi.

Ulevi na uzinzi vimewafanya wastaafu wafulie na kufa haraka.
Ulevi na uzinzi ndio vinaongoza kuwafukuzisha kazi maaskari .
Naleta kisa kimoja tu kati ya vingi nilivyoshuhudia maishani mwangu.

Baba mmoja Askari magereza alistaafu Mei na kulipwa mafao yake Julai mpaka Januari inafunguliwa shule alikosa hata laki 2 ya kumnunulia vifaa vya shule mwanae wa kumzaa mwenyewe ili aanze kidato cha kwanza shule nzuri kabisa ya serikali , ni shule ya vipaji.

Mtoto kakosa elimu tena ni binti.
Within 5 months mzee ashamaliza mafao yake yote kwasababu ya ulevi.

Huyu mzee naweza kumtaja kwa jina na mahali alipofanyia kazi kama itakuwa si kosa.

Kwakuwa nimekulia maeneo ya Kambi za magereza na jeshi nimeona jinsi pombe na uzinzi vilivyowagaragaza wengi.
Vijana acheni uzinzi na ulevi.
Wewe ndiyo unajuwa leo?
 
Ulevi nakataa, ila uzinzi ni kweli unaleta umasikini
 
Wazungu huko Marekani ni walevi na wazinzi sana.
 
Tia hasara za hiyo mambo na faida za kutokutumia
 
Ambao sio wazinzi wala walevi tuambieni mnamiliki utajiri wa shilingi ngapi
 
Kweli kabisa hii imewahi kunitokea mimi binafsi, achana na uzinzi kwani haukuachi tu fukara ila unakuachia laana na mikosi kibao
 
Maaskari wa majeshi yote wanaongoza kwa uzinzi na ulevi..noma sana
 
Back
Top Bottom