Uzio wa nyumba usiathiri ukuaji wa mtoto

Uzio wa nyumba usiathiri ukuaji wa mtoto

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wanaharakati wa haki za watoto kisiwani Pemba, wamewataka wazazi na walezi, wanaomiliki nyumba zilizozungushwa kuta ‘fens’ kuwapa muda watoto wao kuchangamana na wenzao, ili kucheza pamoja, ikiwa ni sehemu moja wapo ya kukuza ubongo wao.

Wamesema, njia moja na rahisi ambayo haihitaji gharama katika kumkuza mtoto ni kumpa haki ya kucheza na wenzake wasioishi pamoja, ili kupata habari na matukio ya mtaani.

Wamesema wazazi wasipokuwa makini wanaweza kudumaza akili na ukuaji wa watoto wao.

Wameeleza kuwa akili ya mtoto haijengwi kwa chakula bora, gari ya kwendea skuli, uzuri wa nyumba pekee tu, bali njia nyingine rahisi ni kuwapa fursa watoto, kuchangamana na wenzao katika michezo mbali mbali.

Mwanaharakati Khamis Uledi Khamis amesema mtoto anapofungiwa ndani kwa madai ya kuepushwa kupigwa na wenzake, ni kudumaza ubongo na kusinyaa ufahamu wake.

‘’Inawezekana wazazi wanamaisha mazuri na nyumba kubwa yenye ukuta na mbwa mkali, lakini kama mtoto hawakumtoa nje kucheza na wenzake, atanyemelewa na udumavu wa kuduma,’’ alieleza.

Mwanaharakati Aisha Hemed Khamis wa Chake chake amesema mtoto anapopata taarifa kutoka nje ya nyumba yao, huwa rahisi kutanua akili na ufahamu wake mara moja.

‘’Kadiri mtoto anapochangamana na wenzake wa nyumba za jirani au mtaa wa pili, na ufahamu wake ndivyo unavyoongezeka mara dufu,’’ alisisitiza.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Chake Chake, Rashid Said Nassor amesema wazazi wengi wenye uwezo, wanadhani ni dhambi kubwa, watoto wao kuchangamana na kucheza na watoto wengine.

Alieleza kuwa, kadiri mtoto anavyokwenda masafa yenye usalama kwa ajli ya kucheza na wenzake, vivyo hivyo na akili yake hupanuka kwa haraka.

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake, Abdalla Rashid Ali akizungumza hivi karibuni, aliwataka wazazi na walezi pamoja na kuwapa fursa watoto wao kucheza na wengine, hata wao wajitengee muda kushirikana kwa michezo.

‘’Ipo michezo kama vile mdako, kupigana mito, mpira, kurusha chungwa, kupangwa kokoto kwa mfumo wa picha na kung’waruziana macho kwa njia ya kutishana mzazi na walezi wanaweza kucheza na watoto kama sehemu ya uchangamshi,’’alieleza.

Naye Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Pemba Omar Mohamed Ali, amesema haki ya kucheza kwa mtoto, inatambuliwa na sheria ya mtoto nambari 6 ya mwaka 2011, hivyo ni wajibu kwa wazazi kuitekeleza kwa vitendo.

‘’Sheria inataka watoto wapewa haki ya kucheza na wenzao, sasa kama kuna wazazi wanafungia kwenye mageti, wanaweza kuwa chanzo cha kusinyaa kwa akili yao."

Nae Msimamizi wa kitengo cha lishe Wilaya ya Chake Chake, Harusi Masoud Ali, amewakumbusha wazazi na walezi, kuwapatia lishe bora watoto wao.

Waziri wa Afya Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, amesema yapo mambo ambayo jamii wanatakiwa kuyafanya, ili kuwa na kizazi bora cha hapo baadae.

‘’Ni nafasi kwa wazazi na walezi, pamoja na kuwapa haki watoto wao kushiriki michezo mbalimbali, lakini wajenge utamaduni wa kuwashauri watoto kwa mambo yanayowahusu,’’ alieleza.

Mzazi Is-mail Ali Juma, amekiri kuwa wamekuwa wakiwafungia watoto wao kwenye kuta ‘fens’ kutokana na uwepo wa majanga kadhaa kwa watoto.

‘’Mtoto ukiwa humuoni dakika 30, tayari wasiwasi, sasa mimi huwafungia, lakini pia huwatoa nje kucheza nawenzao pale nikiwepo,’’ alieleza.

Mjumbe wa Baraza la Watoto Shehia ya Mwambe, Hija Omar Ussi na mwenzake wa Mkoani Hamida Issa Machano waliwakumbusha wazazi kuwa, suala la kucheza kwao halina mbadala.

''Wazazi na walezi wetu wamekuwa wakitengea muda wa kucheza na kupumzika, na sisi ni sawa na binaadamu mwengine yote hayo tunayahitaji,''walisema.

Nae Aisha Haji Mohamed wa Machomane Chake chake, alisema huwa wanafanya hivyo, ingawa kwa ule muda ambao wazazi wapo nyumbani.

Muwezeshaji kwenye mafunzo ya Kitaifa ya Sayansi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ‘SECD’ Everlyne Okeyo, yaliofanyika mkoani Dodoma Tanzania anasema, watoto wanakosa ukuaji mzuri wa kutengeneza ubongo wao, kwa kule wazazi kutowapa muda nafasi ya kucheza.

Katika hatua nyingine, Everlyne alisema, ubongo wa binadamu una nyuroni bilioni 100, na ndio maana mtoto mara anapozaliwa, huwa na asilimi 25 ya ubongo wake ni mtu mzima.

‘’Mtoto anapofikia mwaka mmoja, hufikia asilimia 60, wakati miaka miwili huwa na asilimia 75 na kuanzia miaka minne hadi sita, hubeba asilimia 90 ya uwelewa,’’ alieleza.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wa Tanzania bara Dk. Dorothy Gwajima, aliwataka waandishi wa habari, kuifikisha kwa jamii, dhana ya malezi ya kisayansi ‘SECD.

Source: Pembatoday
 
Ili kumruhusu mwanao kuungana na wenzake lazima kwanza kama mzazi ujiridhishe tabia na mienendo ya watoto wenzie kupitia jamii inayowazunguka.

Maeneo kama Kigogo Mburahati, Manzese, Tandika, Tandale, Sinza, Vingunguti, Yombo na Buza....ni maeneo mabaya sana kwa malezi na makuzi ya mtoto.....tabia za chafu na za ajabu ajabu za jamii za watu wa maeneo hayo wanazohamishia kwa watoto wao badala ya kukuza uwezo wa mtoto kiakili badala yake inamkomaza kiakili kwa mambo mazito ya kifedhuli.

Vile vile jamii zetu siku hizi zimeharibika, kuna mabazazi na mashetani ambayo wenyewe fantasy zao ni kufanya uchafu na watoto wadogo, ndio maana kumeshamiri kesi za ubakaji na ulawiti kwenye jamii zetu nyakati hizi.

Ki kweli ni jambo zuri na la kheri mtoto kucheza na watoto wenzie lakini unapaswa kufanya hivyo kwenye mazingira salama na yenye kumjenga mtoto.

Word is enough for the wise
 
Back
Top Bottom