Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Sham777

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2019
Posts
335
Reaction score
840
Kutokana na hali Ngumu ya maisha na tatizo la ajira vijana wengi tumeamua kurudisha mpira kwa kipa huku tukisubilia mambo yakae sawa tujipange upya na sis tufanye maisha yetu kama awali.. Wengine wamerudisha mpira kwa wazazi wao, wengine wamerudisha mpira kwa Ndugu, ila sisi Ma Pro na Ma Legendary tumerudisha mpira kwa mashemeji zetu walipo olewa dada zetu na hatujali..

Kama ilivyo kawaida kila kitu kina kanuni, sheria na taratibu zake endapo ukizifata zitakusaidia sana jins ya ku survive kipindi hichi kigumu cha mpito. Haya ni mambo muhimu sana ya kuzingatia pindi unapo rudisha mpira kwa shemeji yako.

1. Usipige Gym. Gym inamfanya mtu awe na confidence sana hivyo kupelekea kuingilia ugomvi pindi Shem wako anapo mkata dada yako makofi.. Pia Gym hufanya kiwango cha kula kuongezeka ivyo unapo kaa kwa mtu jitahidi sana uwe una kula kiasi kama wenyeji ulio wakuta..

2. Kamwe usije ingilia Ugomvi wa dada yako na shemeji yako pindi wakikusana/ kuzozana au hata kurushiana makofi.. Jitahidi sana kubaki chumbani kwako jifanye kama hujasikia kitu.. Ugomvi wa mke na mume always unakuwa ni wa muda tu lazima watapatana.. Vip kama uliingilia? Itakuwa ndio mwisho wako kukaa kwa shemeji..

3. Kin'gamuzi kikiisha either Dstv or Azam mwambie dada yako amwambie Shemeji yako / mme wake.. Hili litafanyika kwa haraka zaidi sababu Shemeji yako atajua ni kwa ajiri ya mke wake.. Wew shughulika na mambo kama Luku zikibakia unit chache mjuze shemeji yako hii itasaidia akuone active sana mfatiliaji..

4. Siku za weekend shemeji yako akiwepo jitahidi sana usishinde sebleni kwenye Tv. Hata ukiwa seblen basi jitahidi kukaa mbali na remote.. Sababu wengi huwa wanapenda weekend kuinjoi na familia zao wew pale unahesabika kama mzigo na sio part ya familia only dada yako anakuona memba wa familia..

5. Kamwe usije kuwa shabiki wa Team tofauti na anayo shabikia Shemeji yako. Hii huwa inajenga sana chuki hivyo ili uishi kwa aman kuwa team moja na shemeji yako .. Pia jitahidi sana kumsifia sifia.. Kama ana gari pia jitahidi sana kusifia gari yake ajue ndio dream car yako hata kama ni starlet or Vitz.

6. Usiwe unaleta marafiki zako nyumbani kwa shemeji yako.. Jitahidi sana wanao wote muwe mnakutana nje uko.. Sababu shemeji yako. Mashemeji zetu huwa wanaona sisi tunao kaa kwao kama tumesha feli maisha.. Ivyo huwa wana hisi hata marafiki zetu ni wale walio feli maisha wanawaona ni wezi tu.. Hivyo jitahidi sana kutopeleka marafiki kwa nyumbani kwa shemeji yako.

7. Jitahidi kila ukikaa kimaongezi na shemeji yako mwambie kuna Interview fulani nilipiga wamesema watanipigia simu ivyo nasubilia waniite.. Hii itampa moyo sana shemeji yako atajua soon ukipata kazi utaondoka kwake na ukakae kwako..

NB: Kama kijana usione aibu kurudisha mpira kwa kipa mambo yanapo kuwa magumu sababu kila mtu na maisha yake. Maneno yapo tu binadamu huwa hakosi cha kusema.. Na always mambo huwa yanabadilika hivyi ishi maisha yako.

Hii dhana ya kutuona watu tunao kaa kwa mashemeji zetu ni watu wadhaifu ife leo, Sababu baadhi yetu tumesha pitia mambo magumu na struggle za kila aina na tumesha wai shika hela ambazo wengine mbaka mnakuja kufa haiji tokea ukazishika kwa mkupuo.
 
Nilijua wewe wa kike sasa unaishi kwa semegi hahahaaaaaaaa mwaka wa tatu nadhani ungekuwa unagraduate sasa hivi maisha ya shemeji na ushatoa mimba kadhaa hata kama una sura mbaya hahahaaaaa utani tuu
Hahahahhaa Boss .. Nisha Graduate kitambo sana ni vile life imenifikisha hapa nilipo sina choice
 
Ongeza hizi
Usile sana maana utasemwa mpaka na dada yako 😂😂 unakula na ufanyi kazi yoyote kazi kuangaliaTV
Fanya kazi za nyumbani kifupi act kama house boy/girl
Saidia watoto kuhusu home work na kazi zao za shule
Ukiwa mnyenyekevu hivi watakupenda na wewe ndio sehemu ya kuomba kimtaji walau uingize hata buku 2 kwa siku upate kuthaminika
 
Ongeza hizi
Usile sana maana utasemwa mpk na dada yk [emoji23][emoji23]unakula na ufanyi kazi yoyt kazi kuangalia tv
Fanya kazi za nyumbani kifupi act kama house boy/girl
Saidia watoto kuhusu home work na kazi zao za shule
Ukiwa mnyenyekevu hivi watakupenda na wewe ndio sehemu ya kuomba kimtaji walau uingize hata buku 2 kwa siku upate kuthaminika
Umetisha sana aisee.. Hizi huwa nafanya pia ndio maana nimedumu sana hapa.. Huwa naamka mapema sana kabla ya mtu yeyote, napukuta gari yake , naandaa madogo wenyewe akiamka wanakuta mambo mengi yasha kamilika..
 
Umesahau jambo hili. Usimchunguze sana shemeji ako, anaweza kuwa anatumia hii kitu kila jioni
db917d19270d87b4a625e10729217f4c.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom