Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Nina imani kua hapo unaishi tu kimwili ila nafsi yako inaona kabisa kua upo kifungoni, hakuna kitu kizuri katika maisha kama kua huru, bora uwe na buku ambayo ni yako kuliko milioni ambayo sio yako,

Jitahidi utoke hapo kifungoni na Mungu akusaidie In sha Allah.
 
Mbona tunawachukulia poa sana mashemeji zetu, kama mtu hujui maisha unaweza kuona karaha kukaa na ndugu(iwe ndugu yako au wa mke) lakini kama imepitia life la kibongo utaona kawaida sana. Muhimu usiishi kama mzigo, jitume, fanya vikazi vidogo vya home, usiwe mtu wa kulala ovyo, onyesha juhudi za kutafuta pesa hata kujishikiza sehemu, usiwe mlevi na usipende kurudi nyumbani very late.
Yaani mkuu mimi nipige deki?
Mimi?
Nioshe vyombo?
Nisafishe choo mimo?
Nimwagilie maua mimi?
 
Nina imani kua hapo unaishi tu kimwili ila nafsi inaona kabisa kua upo kifungoni,hakuna kitu kizuri katika maisha kama kua huru,bora uwe na buku ambayo ni yako kuliko milioni ambayo sio yako,Jitahidi utoke hapo kifungoni na Mungu akusaidie In sha Allah.
Mkuu ndugu wengine hawataki tukoke tunapokaa.
Wanaona labda ukiondoka utapata shida huko unakoenda.
 
Mbona tunawachukulia poa sana mashemeji zetu, kama mtu hujui maisha unaweza kuona karaha kukaa na ndugu(iwe ndugu yako au wa mke) lakini kama imepitia life la kibongo utaona kawaida sana. Muhimu usiishi kama mzigo, jitume, fanya vikazi vidogo vya home, usiwe mtu wa kulala ovyo, onyesha juhudi za kutafuta pesa hata kujishikiza sehemu, usiwe mlevi na usipende kurudi nyumbani very late.
Point sana hii .. Mwenyewe nina malengo mazuri sana sitegemei kukaa hapa forever ingawa napata kila kitu ila kuna vitu nakosa kama privacy
 
Nina imani kua hapo unaishi tu kimwili ila nafsi yako inaona kabisa kua upo kifungoni,hakuna kitu kizuri katika maisha kama kua huru,bora uwe na buku ambayo ni yako kuliko milioni ambayo sio yako,

Jitahidi utoke hapo kifungoni na Mungu akusaidie In sha Allah.
Thanks sana kwa ushauri..
 
Kwani kuna tatizo gani wewe kufanya hizo kazi, hutaki kusafisha choo lakini unaenda chooni kila siku, huoshi vyombo lakini huachi kula, kwani kusafisha mazingira ya nje na kumwagilia maua kuna shida gani?
Mkuu hao watu wa aina hiyo huitwa KKB Kula Kulala Bure.
 
Point sana hii .. Mwenyewe nina malengo mazuri sana sitegemei kukaa hapa forever ingawa napata kila kitu ila kuna vitu nakosa kama privacy
Privacy utaipata ukiwa kwako, najua at your age unatamani uwe na faragha hata ukimleta demu u-enjoy naye hapo, ni watu wachache watakubali ufanye hivyo coz hapo kuna watoto wadogo, tunasema utawafundisha tabia mbaya.

Kingine, waheshimu na kuwasaidia watoto kimasomo, kuna wimbi la vijana(wajomba/baba wadogo) kuwaharibu watoto kingono, usifanye hivyo ni dhambi kubwa sana, mashoga/lesbians wengi wanatokana na hawa watu.

So privacy itakuja ukiwa kwako, vumilia.
 
Back
Top Bottom