Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Afadhali kuishi kwa kaka yako au wajomba maisha yakikupiga kuliko kwenda kuishi kwa shemeji mume was Dada yako duuuu! Hapana pale unatakiwa uende siku mbili tatu tu kusalimia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwenye timu mimi kabisa nishabikie arsenal bora unichukie yaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha ni hatua lakini hakuna raha kama mtu ukiwa na sehemu yako ya kuishi bila kumtegemea mtu/watu.
 
One of the hardest thing in life ni kuishi kwa ndugu wa aina yoyote. Ukijikuta kwenye situation kama hiyo, pigana unavyoweza kutoka katika hayo mazingira. Trust me, it is most humiliating way of living, haijalishi ni shemeji wa jinsia ipi au wa upande upi.
 
kurudisha mpira golini ni sehemu ya maisha....then unaanza tena...but 3 yr ni noma sana......mashemeji wana visa balaa....hasa kuolewa dadako........komaa uondoke,,,,,hata ukalale stand akilini inyooke...hapo ni kama gereza huru...
 
Mkuu kwa namna fulani unakuwa kama unafeli hivi, kwa usawa wenyewe huu mzee Shemeji anakuona ni Bonge La mzigo, Furushi kabisa
 
Nyinyi vijana mnaokaa kwa mashemeji au wazazi wakati mshafikia umri wa kupambana fateni huu ushauri.

1. Usiwe mvivu hata kama huna ajira au mishe. Jishughulishe na shughuli yoyote hapo kwenu.
2. Usipende kukaa sebuleni, hii itakuepusha kuonekana mzembe. Kaa pale kwenye muda maalum, either taarifa ya habari au kipindi pendwa.
3. Ukipata ajira au mishe jitahidi kuchangia gharama za kutunza hiyo familia; kwa mfano unaweza leta vitu vidogo vidogo kama carrots, nk.

TAKE NOTE: Hakuna ndugu au mzazi asiyependa kukaa na wewe hadi ukazeeka ikiwa utachangia hata usafi.
 
Shemeji akirudi na dada amekwenda kusukwa nywele mtengee chakula na akimaliza kula osha vyombo.
Hata kama una mvi kumbuka kuosha Gari ya shemeji.
Haya yote yanawezekana kama kuna deadline yako binafsi ya kukaa hapo.

Kama umeregea tu miaka inakatika,hata ukiambiwa na dada kuzugua ukuta vumbi utamind.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…