Nyinyi vijana mnaokaa kwa mashemeji au wazazi wakati mshafikia umri wa kupambana fateni huu ushauri.
1. Usiwe mvivu hata kama huna ajira au mishe. Jishughulishe na shughuli yoyote hapo kwenu.
2. Usipende kukaa sebuleni, hii itakuepusha kuonekana mzembe. Kaa pale kwenye muda maalum, either taarifa ya habari au kipindi pendwa.
3. Ukipata ajira au mishe jitahidi kuchangia gharama za kutunza hiyo familia; kwa mfano unaweza leta vitu vidogo vidogo kama carrots, nk.
TAKE NOTE: Hakuna ndugu au mzazi asiyependa kukaa na wewe hadi ukazeeka ikiwa utachangia hata usafi.