Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Uzoefu: Naishi kwa Shemeji yangu huu mwaka wa tatu

Hili suala la kukaa nyumbani naona watu wanalichukulia kwa tafsiri isiyo sahihi

kweli kabisa aise wana JF tumepitia haya maisha ila saivi tunayapondea
le mutuz tu humu ndio ana haki ya kuyapondea haya mambo mana alianza kujitafutia akiwa mdogo sana na aliondoka kwao ila tatizo lake alipozeeka alirudi tena kwao


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni sawa ina maana jamaa kaambiwa aiongoze familia.
Mimi mama yangu mdogo upande wa mama aliolewa na jamaa wakapata mtoto mmoja ila kabla mama mdogo hajajifungua jamaa alipigiwa simu toka Mbeya aende fasta mzee wake anaumwa.
Jamaa alivyoenda akapewa wosia abaki Mbeya kuitunza familia yake.
Mpaka naandika hii comment ni miaka kama 9 imepita Mama mdogo hajaonana tena na jamaa.
Haha na mama mdogo akaamini kabisa?
 
Wanadamu saa nyingine tunazengua, yaani kuishi na wazazi mpaka miaka 30 ni nongwa wakati Yesu anaishi kwa Baba yake zaidi ya miaka elfu mbili mpaka sasa.
Nyinyi vijana mnaokaa kwa mashemeji au wazazi wakati mshafikia umri wa kupambana fateni huu ushauri.

1. Usiwe mvivu hata kama huna ajira au mishe. Jishughulishe na shughuli yoyote hapo kwenu.
2. Usipende kukaa sebuleni, hii itakuepusha kuonekana mzembe. Kaa pale kwenye muda maalum, either taarifa ya habari au kipindi pendwa.
3. Ukipata ajira au mishe jitahidi kuchangia gharama za kutunza hiyo familia; kwa mfano unaweza leta vitu vidogo vidogo kama carrots, nk.

TAKE NOTE: Hakuna ndugu au mzazi asiyependa kukaa na wewe hadi ukazeeka ikiwa utachangia hata usafi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nakaa kwetu hapa nataka niende kupakua lunch (nimechelewa kuamka sana). Nikimaliza nawasha TV natizama Aljazeera updates za corona mpaka cha usiku kiive.
Chalii unapokaa kwenu usiangalie Aljazeera au BBC....

Unatakiwa kuangalia Clouds n.k.

Mwisho utajadili na baba yako uwe upande asiopenda...akufukuze nyumbani.
 
Kama wewe Ni mtoto wa kiume Hakikisha unamtengea maji ya kuoga..Kama dada yako hayupo
 
Me nakaa na shemeji yangu,kapata mishe juzi kati lakini kawa mtata kwenye upande wa MITIPULA(Pesa) balaa na me namzoom tu baada ya miezi mitatu namtolea mbavuni.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kutoharibu mahusiano watu wakasema umemfukuza, mpangie ghetto.. Mlipie miezi mitatu.. Kitanda anacholalia mwambie akihamishie kule getto kwa kuwa amekua.. Ila wakati wa msosi awe anakuja kula nyumbani.. Atakuja wiki mbili tatu ila baada ya hapo, atajiongeza mwenyewe.
 
Chalii unapokaa kwenu usiangalie Aljazeera au BBC....

Unatakiwa kuangalia Clouds n.k.

Mwisho utajadili na baba yako uwe upande asiopenda...akufukuze nyumbani.
Hahaha naangalia hizo ili mzee tukiwa sebuleni tunajadili siasa na cross-cutting issues tunaenda sawa mzee anaona hili jembe acha libaki baki home.
 
Nitarudisha kwa bi mkubwa na dingi ila sio kwa shemeji aisee ni bora hata nikae kwa masela ghetto kwa muda huku nikipiga mishe yyte halali hata kama si taaluma yangu alimradi nije baadae kutoboa ila kwa shemeji??BIG NO kwanza kwangu ni bonge la tusi aisee .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom