Uzoefu wa biashara ya juisi ya miwa; Changamoto na ushauri

Uzoefu wa biashara ya juisi ya miwa; Changamoto na ushauri

Habari, wana Jf.

Kutokana na faida na utamu wa juice hii, imepelekea juice ya miwa kupendwa sana mjini.

Tubadilishane uzoefu kwa wamiliki wa biashara hii, je mashine hasa zile za umeme zinapatikanaje na kwa bei gan, na vp kuhusu upatikanaji wa Miwa hususani kwa Dar es salaam.

Karibuni.
 
Miwa inatoka mtibwa morogoro machine china kuhusu bei ngoja waje
 
20170217_140122.jpg
 
Hizo ndiyo mashine nilizonazo moja ni manual na umeme na nyingine ni umeme tu.
Uwezo wa mashine ni glasi 300 ya juice kwa siku. Bei ni 2m. Nipo arusha
 
Habari ndugu zangu. Km kichwa kinavyoelezea naomba kujua kuhusu biashara ya juice ya miwa. Changamoto zake na upatikanaji wa mashine ya kutengeneza juice ya miwa ni bei gani? Najua hapa jukwaani swezi kukosa wafanyabiashara hii na wenye uzoefu wake hasa kwa maeneo ya Dar

Asanteni
 
Nenda SIDO utapata bei ya hiyo mashine au tafuta wanaouza hiyo juice waulize maswali yako haya watakusaidia na utapata pa kuanzia
 
Sahiv msimu wa mvua aise unaweza kunywa Mwenyew Subil kidogo ata kiangazi
 
Mashine zipo aina mbili, ya kutumia umeme(mpaka 1,000,000) na manual kuanzia 350,000 pale buguruni kituoni kama unaelekea ubungo. Matumizi yanategemea sehemu ulipo(kama kuna umeme)..mimi nilikuwa nayo hiyo manual hapo ubungo songas kwasiku nilikuwa napata faida 30,000 baada ya kutoa matumizi yote..changamkia fursa binafsi nimepatia mtaji hapo
 
Habarini za jioni wanabody.

Kama kichwa cha habari inavyojieleza nimevutiwa sana na biashara hii ya kuuza juice ya miwa. Mwenye uzoefu na hii biashara naomba mawazo chanya ili niweze kuwekeza kwenye biashara hii.
Pia itakuwa poa ukiniambia gharama ya mashine ya kukamua miwa. Upatikanaji wa miwa na bei. Na kama kuna vitu vingine vya ziada. Ahsanteni naomba kuwasilisha
 
jiulize wewe mwenyewe maswali haya
1.unaishi wapi ?
2.ninapoishi hapa wateja wapo ama wateja wangu ni akina nani?
3.malighafi ya bidhaa zangu natoa wapi kwa hapa?
4.ninapanga kutumia kiasi gani cha fedha
5. nitatoa wapi mtaji
7. mashine hizi zinapatikana wapi je nimewahi kufanya survey juu ya mashine hizo
8. kuna mtu anafanya biashara kama hii eneo nililopo hapa?
ukimaliza hayo njoo tena kasha uende SIDO iliyopo maeneo yako
 
jiulize wewe mwenyewe maswali haya
1.unaishi wapi ?
2.ninapoishi hapa wateja wapo ama wateja wangu ni akina nani?
3.malighafi ya bidhaa zangu natoa wapi kwa hapa?
4.ninapanga kutumia kiasi gani cha fedha
5. nitatoa wapi mtaji
7. mashine hizi zinapatikana wapi je nimewahi kufanya survey juu ya mashine hizo
8. kuna mtu anafanya biashara kama hii eneo nililopo hapa?
ukimaliza hayo njoo tena kasha uende SIDO iliyopo maeneo yako
Mtu kauliza Ili apate ufumbuz, still na ww unampa Maswali..
 
Back
Top Bottom