Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,316
- 871,876
Ni mada ya kiroho lakini itakayoanzia kimwili, Hi yo inaweza kuwatatiza wengine!
Pili mifano nitakayotoa ni halisi na ikibidi nitataja majina halisi ili watu wapate kuelewa vema.. .
Kuna aina tofauti ama mbalimbali za minada. Mada hii haiangazii minada ile ya furaha ya kwenda kula nyama choma na kufanya shopping mbalimbali kwenye masoko ya siku za wiki
Mada hii pia haihusiki na ile minada ya Ku clear stock ghalani baada ya mmiliki kutaka kuingiza mali mpya
Wala mada hii haihusiani na ile minada ya msimu ya watu wanaoamua kuuza vitu vyao kwa hiari baada ya kuvichoka ama kukaa navyo muda mrefu
Na mwisho haihusiani na ile minada ya mashirika ama site zilizomaliza projects
Mada hii ni maalum kwa wale wanaonunua mali na vitu vya wengine wanaodaiwa na ambao wameshindwa kulipa madeni hivyo vitu ama mali zao hizo inabidi kuuzwa ili kufidia deni husika!
Mali na vitu vya namna hii maranyingi huuzwa kwa bei ya chini tofauti na uhalisia! Usishangilie kuvipata kwa bei ya kutupa vina changamoto zake kiroho
Iwe nyumba, shamba ama kiwanja
Iwe gari, mashine, au mtambo
Iwe samani za ofisi, nyumbani au kwenye biashara
Iwe vyombo vya biashara ama matumizi nyumbani.. Vyote hivi vina muhuri wa umiliki wa mtu mwingine.. Kuvibadili umiliki kwa lazima bila hiari ya moyo ya mmiliki wake kuna shida zake kiroho.. Tena kubwa tuu
Unaataka kuanzisha biashara yoyote tena kwa pesa yako halali kabisa mfano gesti, gari ya abiria au mizigo, mgahawa, bar nk! Unapata nyenzo zitokanazo na mnada wa aliyekuwa anafanya biashara kama yako kisha akafeli vitu vikapigwa mnada kulipia madeni ya wafanyakazi, mkopo kodi nk halafu ukavununua wewe kwenda kuanzisha biashara kama hiyohiyo. Ukifaulu shangilia sana..!
Unaweza kuanzisha biashara husika na vitu vya mnada na ukafaulu vizuri tuu lakini mapato yake yasiwe na baraka! Hayakuzi biashara wala hayatunzi faida! Kila ukiikata pesa yake kuna changamoto inajitokeza unaitumia yote!
Kama ni gari la kukodi kila ukipokea hela yake kuna jambo litajitokeza uitumie kwalo.. Kama sio kwenye gari lenyewe basi ni la kwako binafsi ama ndani ya familia.
Utaendelea hivyo mpaka utafilisika na kufunga biashara huku sometimes ukibaki na madeni na changamoto kibao
Bila kujua ni mambo ya kiroho utajifariji na kauli za kimfaacho mtu chake! Utauza zile nyenzo zote na pesa yake hutaona umeifanyia nini
www.jamiiforums.com

Pesa za mikopo, mali za minada: Je, kuna ulazima wa kuzifanyia tambiko ama kafara?
Kuna vitu hata tuvipinge namna gani bado vipo na vinafanyika na vitaendelea kufanyika tu. Na hii ni kwa sababu moja tu, vina mahusiano ya moja kwa moja na mila, desturi na tamaduni. Ishu ya kafara ama tambiko ni kongwe tangu kuandika misahafu. Manabii na mitume walifanya kafara, walifanya...