Uzoefu wangu kwenye mali na vitu vya minada: Jifunze toka kwangu ujiokoe na mengi

Kwanini changamoto zisiende kwa anayeuza? Aliyenunua ana kosa gani?
Mkuu; Ukifuatilia mtiririko wa comments huko juu utajifunza ni kwa nini. e.g. soma comment @From Meru na @Lovebird na wengine.....
Wote wanabainisha kwamba Aliyeuza mali kwa mnada i.e. Dalali aliuza mali kwa kujali maslahi binafsi(Dhuluma)bila kujali maslahi ya mwenye mali, na mnunuzi alijifaidisha kwa kununua kwa bei "chee" i.e. alimdidimiza mwenye mali ambaye hakuwa na namna ya kuipinga bei hiyo ama kuitetea(Bargain) - wote wamemdhulumu mmiliki halali wa mali iliyopigwa mnada..
 
Mwenyewe nimwishia kusoma hili neno mambo ya kiroho.
Huwa sipendi mtu afanye justification ya mambo kwa kuhusulisha na mambo ya kufikirika
Umenena vyema; ila ujue na utambue kwamba, ww kama binadamu aliye hai pia unayo roho ndani mwako. Kwa nini unayakataa mambo ya Kiroho? Ila kama huna roho ndani yako, basi nakiri mm hapa nimeandika upuuzi mtupu naomba nisamehewe.
 
Unaweza kutafuta sababu kwamba
Umerogwa ama lile eneo si zuri kwa hiyo biashara lakini mbona kuna wenzako wako hapohapo na wanashamiri?
Kwa akili za haraka ama kwa kushauriwa utataka kwenda kwa waganga ama kubadili eneo ama biashara.. Utajikuta nawe unaingia kwenye mikopo na kuweka mali zako binafsi rehani nazo kuishia kupigwa mnada. Kuna roho linakuwa linatembea kwenye vile vya kwanza na kuja kuambukiza vyako

Sometimes unaweza ukauza vyote vya mnada na ukabakiza kimoja unachokipenda! Na maranyingi hutokea kwenye samani hasa viti na meza! Kumbe vile ukivyouza havina shida, bali passwords ziko kwenye vile vilivyo baki😂😩
Kea kifupi vitu vya minada hasa kwa ajili ya kulipia madeni havifai kununua ama vya biashara iliyokufa! Viepuke ama vikatae ama vifanyie maombi ya nguvu vitakasike kabla hujaanza kuvitumia. Vinakuwaga na bei poa sana lakini kumbuka rahisi aghali
Hiyo hali haiwakuti wanunuzi tu bali hata wale wanadishaji.. Nioneshe hata dalali mmoja aliyekuwa na mwisho mwema! Yuko wapi Majembe auction mart.. Tulifanya naye sana biashara enzi zake🥺😭😂
Mtu kajibana katumia kila alichonacho kanunua kagari lake ama kajenga kajumba kake na familia yake! Leo kwasababu ya changamoto za maisha kakopa kashindwa kulipa pesa ndogo tu wewe unakuja kibabe kuuza mali yake familia yake ianze kuteseka tena unadhani utabaki salama kweli? Uza basi bei ya halali mkate deni na gharama zenu kinachobaki mumpe kifuta machozi. Hamjali kabisa h
Kuhusu hilo!
Nawe mnunuzi utakuwa na amani kweli!? Tafakari
Tuliwahi kununua jacuzzi bomba kweli la 6M kwa 1M.. Likakaa miaka kibao bila kutumika na halikuuzika tena mpaka tulipolitelekeza mahali na kuliacha hapo kama dhamana ya deni😂
Vitu vingi vya mnada nilivyowahi kununua havukuwahi kunibariki hata kimoja! Leo hii nikitaka kununua kitu cha mnada lazima nikichunguze vema asili yake!
Kesi ya majembe naijua vzr sana, maana Mzee aliyepanbana nae akachemka majembe nilikua namjua
 
Mkuu; Ukifuatilia mtiririko wa comments huko juu utajifunza ni kwa nini. e.g. soma comment @From Meru na @Lovebird na wengine.....
Wote wanabainisha kwamba Aliyeuza mali kwa mnada i.e. Dalali aliuza mali kwa kujali maslahi binafsi(Dhuluma)bila kujali maslahi ya mwenye mali, na mnunuzi alijifaidisha kwa kununua kwa bei "chee" i.e. alimdidimiza mwenye mali ambaye hakuwa na namna ya kuipinga bei hiyo ama kuitetea(Bargain) - wote wamemdhulumu mmiliki halali wa mali iliyopigwa mnada..
Nadhani hujaelewa mada! Hapa anazungumziwa mnunuzi! Naomba ubainishe makosa ya mnunuzi!
 
Umenena vyema; ila ujue na utambue kwamba, ww kama binadamu aliye hai pia unayo roho ndani mwako. Kwa nini unayakataa mambo ya Kiroho? Ila kama huna roho ndani yako, basi nakiri mm hapa nimeandika upuuzi mtupu naomba nisamehewe.
MTU akishakwambia mambo ya kiroho ni ya kufikirika huhitaji hata kuendeleza naye mjadala
 
Nadhani hujaelewa mada! Hapa anazungumziwa mnunuzi! Naomba ubainishe makosa ya mnunuzi!
Kosa la mnunuzi ni kununua mali ya dhuluma tena kwa bei isiyoendana na thamani halisi ya bidhaa. i.e. Mnunuzi ameshiriki kimatendo kuwezesha dhuluma itendeke. Kama mnunuzi angeghairi kufanya manunuzi Dalali muuzaji asingepata "fungu tarajiwa" na mwathirika (mwenye mali iliyouzwa) mali yake ingesalimika.
 
Niuzie tv yako kwa bei ya chini huku unanung'unika halafu nipe deadline lini nitaanza kuona mabalaa
 
Hilo haliko katika scenario ya mada hii. Mm nikikuuzia mali yangu halali (Tv) nimefanya hivyo kwa hiari yangu japokuwa najua bei ya Tv sio hiyo tuloridhiana. Nimeiuza Tv kwa sababu zangu binafsi e.g. Old fashioned, Dharura, nimepata nyingine new model etc. Hutokaa uone mabalaa - umejipatia mali kihalali na hujanidhulumu. Ila kama mm niliiba Tv hiyo kwa mtu na mtu huyo anasononeka kwa kuibiwa mali yake; hapo Huchomoki broo.
 
Mwenyewe nimwishia kusoma hili neno mambo ya kiroho.
Huwa sipendi mtu afanye justification ya mambo kwa kuhusulisha na mambo ya kufikirika
So unajiona una akiili Mkuu eti?
Unajiona smaaart sana wewe,yan hupendagi Kabisa Mambo ya kiroho....aisee!
Me Naomba unisamehe tu ila nikwambie tu ile kweli,kma hupendi,hutaki kutambua,kuelewa Mambo ya kiroho wewe ni maiti inayotembea,wewe Kuna mahali haupo Sawa kiakili,una mapungufu makubwa ila hujijui...so unahisi watu wanajifunza Mambo ya kiroho ni kma washamba hv ila wewe ndo mjaaanja...sasa mbona hapo ulipo umebeba roho?Au Hilo nalo hulitaki kulijua?
Kwa vile Dunia ndo hii hii Kuna siku litakukuta jambo huo usmart wa kijinga uliojivisha ndo utakuwa mwisho wake na somo kwako litaanzia hapo.
 
Kosa la mnunuzi ni kununua mali ya dhuluma tena kwa bei isiyoendana na thamani halisi ya bidhaa. i.e. Mnunuzi ameshiriki kimatendo kuwezesha dhuluma itendeke. Kama mnunuzi angeghairi kufanya manunuzi Dalali muuzaji asingepata "fungu tarajiwa" na mwathirika (mwenye mali iliyouzwa) mali yake ingesalimika.
Ila mwenye mali kutokulipa deni la watu ni sawa?
 
So unajiona una akiili Mkuu eti?
Unajiona smaaart sana wewe,yan hupendagi Kabisa Mambo ya kiroho....aisee!
Me Naomba unisamehe tu ila nikwambie tu ile kweli,kma hupendi,hutaki kutambua,kuelewa Mambo ya kiroho wewe ni maiti inayotembea,wewe Kuna mahali haupo Sawa kiakili,una mapungufu makubwa ila hujijui...so unahisi watu wanajifunza Mambo ya kiroho ni kma washamba hv ila wewe ndo mjaaanja...sasa mbona hapo ulipo umebeba roho?Au Hilo nalo hulitaki kulijua?
Kwa vile Dunia ndo hii hii Kuna siku litakukuta jambo huo usmart wa kijinga uliojivisha ndo utakuwa mwisho wake na somo kwako litaanzia hapo.
Naweka lamination hapa isomwe na woteeeeeee na woteeeeeee tuseme....

tuseme aminaa

Infropreneur , kaka angu Kiranga na wadau wengine wengine.

Karibuni kwa maoni yenu.
 
Back
Top Bottom