Bramo
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 13,253
- 10,248
Mkuu, acha hofu ya Kifo, Kifo tumeumbiwaKwa muda mrefu sasa kumekuwa na tabia ya baadhi ya sauti zisizo na sura kutumia mitandao ya kijamii kama jukwaa la kusambaza uzushi kwa lengo la kuleta taharuki, hofu na kupunguza imani ya wananchi kwa nguzo za dola. Miongoni mwao ni wanaojificha kwa majina ya kificho kama Kidnapped King wa X na Mr. Leak wa JF.
Kila mara wanapojitokeza, ajenda yao imekuwa moja tu: kuchafua taswira ya viongozi walioteuliwa na Sponsor, kudhoofisha heshima ya taasisi nyeti na kupandikiza mbegu za shaka dhidi ya mamlaka ya juu ya nchi.
Uzushi Kifo cha Mkuu wa Kivuli
Hivi karibuni, Kidnapped King wa X alitengeneza simulizi kwamba Mkuu wa Kivuli, msimamizi wa idara nyeti ya ulinzi wa taifa, amefariki dunia. Ukweli ni kwamba Mkuu wa Kivuli anaendelea na majukumu yake ya kila siku, akiwa thabiti na imara. Jana tu nilikuwa naye tukipata gahwa huku akinieleza kuhusu kundi fulani linalohangaika kutoboa meli kwa tamaa zao binafsi.
Kauli ya Kidnapped King si chochote bali ni uzushi ulioandaliwa makusudi kuzua taharuki ndani ya taifa.
Wakati huohuo, alieneza propaganda kwamba Bosi wa Daftari Kuu ndiye mrithi anayefuata. Lakini msingi unabaki pale pale: mamlaka ya kuteua viongozi wa ngazi ya juu ipo kwa Sponsor pekee kwa mujibu wa katiba na sheria. Kile kinachozungumzwa mitandaoni hubaki ni uzushi mtupu usio na uhalali wowote.
Njia ya Kumng’oa Bosi wa Daftari Kuu
Swali la msingi ni kwa nini Bosi wa Daftari Kuu anahusishwa kwa nguvu na ajenda hizi za kivuli?
Jibu ni wazi: ni mkakati wa kumchafua, kumwondolea heshima mbele ya umma na kupunguza uhalali wake kama kiongozi. Ni mbinu ya kutengeneza mazingira ya shaka ili ionekane hafai kuendelea na majukumu yake makuu ndani ya Daftari Kuu.
Lakini ukweli unabaki pale pale: nafasi yake ni uteuzi wa Sponsor, na hakuna sauti ya kivuli kutoka mitandaoni itakayoweza kubadilisha uhalali wa uteuzi huo.
Acha hofu,kama imeandikwa utaenda utaenda tu