V.A.R katika ligi kuu ya Tanzania bara

makaveli10

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
31,583
Reaction score
92,670
Ni ukweli uliokuwa wazi kwa viwango vibovu vya waamuzi wetu, wanahitaji msaada wa video na kutokana na teknolojia yenyewe inaweza ikawa gharama kidogo.

T.F.F waongee na azam tv, ikiwezekana katika kila mechi ya ligi kuu kuwepo na refa akiwa na tablet, yenye application ya azam tv, mwenye mawasiliano ya moja kwa moja na wale wanaofanya replays katika mechi.

Refa akiona tukio linalohitaji msaada wa video anazungumza yafanyike marudio.

Kama wapo humu ujumbe uwafikie.
 
kufunga VAR kiwanja kimoja ni $150k...tuna mechi nane kwa siku hivyo $1.2m...inawezekana kabisa...Vodacom,Azam,GSM,Mo.Taifa gas nk watoe hiyo pesa TFF waje kuwalipa kidogokidogo
Kwa kuanzia hiyo ni gharama kubwa mnoo, kwa bajeti ya ligi yetu.

Mahesabu yako kama sijayaelewa vizuri vile.
 
Hazitoshi ndio maana haonekani Onyango akimgusa mguu Kisinda wakati anaanguka
Hazitoshi lakini zinaweza kusaidia pakubwa saana, mbona katika replays huwa tunaona hii offside ama sio, hii penati ama sio, hii ni red card ama sio

Matatizo ya offside zilizowazi
Matukio km kina Morrison uwanjani
Kuamua penati
N.k n.k
 
Huu ni ushauri mzuri.
Kwa jicho lingine ni ushauri ambao ni kama wa kuipunguza kasi yanga, kwani ndo timu inayoonekana kufaidika mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote na uamuzi mbovu uwanjani.
Hivyo kuleta VAR viwanjani ni kwamba yanga itakosa hizo faida na kujikuta inaangukia pua.
 
kufunga VAR kiwanja kimoja ni $150k...tuna mechi nane kwa siku hivyo $1.2m...inawezekana kabisa...Vodacom,Azam,GSM,Mo.Taifa gas nk watoe hiyo pesa TFF waje kuwalipa kidogokidogo
Kwani VAR zinafungwa upya kwa kila game, ama zikifungwa ndio zimefungwa.

Kama ni zinafungwa upya kila game na hizo ndio gharama zake basi ni gharama mnoooo.

Kama zikifungwa ndio mazima, basi tupige $150k mara idadi ya viwanja vinavyotumika ligi kuu
 
Nafikiri unaweza kuhamisha
 
Hahaa... Mkuu acha basi kukorofisha watu.
 
Ina maana mkuu yanga wananunua marefa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…