V.A.R katika ligi kuu ya Tanzania bara

Tatizo Azam tv wana camera chache
Ni kweli.. Lakini pamoja na uchache wa kamera zao, lakini katika replays huwa tunaweza kuona hii ni offside au lah, huyu kashika au lah!! Huyu kampiga mwenzie ngumi au lah!
 
V.A.R ikiletwa ligi ya bongo kubebwa kutapungua maana imeshakuwa too much!
 
Ni kweli.. Lakini pamoja na uchache wa kamera zao, lakini katika replays huwa tunaweza kuona hii ni offside au lah, huyu kashika au lah!! Huyu kampiga mwenzie ngumi au lah!
Bado haiwez kusaidia nafkir Cuf bado wanazngua maana tungeona wanatunga sheria ambazo zingekuwa rafiki ,ili tueone ubunifu wa washirika wao.
 
Bado haiwez kusaidia nafkir Cuf bado wanazngua maana tungeona wanatunga sheria ambazo zingekuwa rafiki ,ili tueone ubunifu wa washirika wao.
CUF gani unayoizungumzia mkuu hii ya lipumba!?

Mimi sijazungumzia level ya CAF huko, ni ligi yetu ya ndani kwanza,

Wewe ulikuwa unashauri sheria rafiki kama zipi zinazoweza kusaidia!?
 
Mikia fc wanabebwa sn.
Mikia nao watasema utopolo wanabebwa saana..

Hii dhana ya kishabiki ndio inatufanya tusisogee, kiukweli waamuzi wetu ni wabovu mnoo..

Kiushabiki tunatizama simba na yanga, ila hawa kina ihefu, mtibwa, kmc, jkt, sijui polisi,kagera etc zinaumia mnoo na maamuzi mabovu ya waamuzi wetu.
 
Kwani ni lazima kila kitu tuige tu, sisi hatuna vichwa tuna mabox au!? Hata km mabox, hatuwezi kufikiria nje ya box..

Mimi sijawahi kuona, we unaonaje V.A.R tablet inawezekana au haiwezekani!? Sio kila jambo mpaka wafanye wazungu.
labda huwezi jua FIFA pengine wana protocol zao na standard zao za camera za VAR
 
Hatimae azam wameamua kufanya jambo baada ya miaka kadhaa, kama azam wazo mlilitoa humu JF msiogope kusema.

Kuna mchango mkubwa sana wa azam kwenye ligi ya kwetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…