V.V.U na Upimaji wake (Coincidences)

V.V.U na Upimaji wake (Coincidences)

Nimefuatilia huu uzi toka post ya kwanza hadi ya mwisho, kuna situation inayonihusu mimi binafsi sijaiona kama imeongelewa.

Mimi nina miaka miwili sasa nafanya ngono bila kinga na mwanamke anayetumia ARV's, kila nikipima naambiwa HIV negative, hii inakuwaje?
Juzi jumamosi nimepima, baada ya majibu ya HIV negative nikamueleza aliyenipima hii situation, akashtuka na kuniambia kwa nini nahatarisha maisha yangu, nikamwambia siamini kama HIV inaambukizwa kwa njia ya ngono, akaniambia inawezekana tu michubuko huwa haitokei, hii inanishangaza kwani huwa natumia hadi ile njia nyingine ambayo inasemekana msuguano ni mkubwa kwa kuwa hakuna virainisho(samahani kwa kusema hilo ni katika kuweka rekodi sawa).

Ningeomba hasa Aragon, kupe, mkuyati og pakamwan wanisaidie ufafanuzi.

Kama kuna mtu ana wasiwasi na maelezo yangu, naweza kumpeleka kwa huyo mpenzi wangu akajionea mwenyewe jinsi anavyokunywa ARV's na pia kumthibitishia kuwa tuna miaka miwili tunafanya mapenzi, bila kinga!

Mhhhhhhhhh!!!!!!! Aiseeee
 
Last edited by a moderator:
Kama sija "ask nicely" mkuu niwie radhi, ila naomba ufafanuzi katika post yangu #358 hapo juu.

Wanasema sijui kuna watu wana kinga ya hawa "wadudu" sijui,wanajua wenyewe mkuu....

Unadhani wanakosa sabahu hawa?

By the way ngoja waje wakujibu mkuu......
 
Situation kama hiyo unaizungumziaje mkuu?

Labda mimi "window period" yangu ni miaka mitatu?, baada ya mwaka mmoja kama nitaendelea ku test negative nitajidunga damu ya mtu HIV postive ili niconfirm uongo huu wa HIV-AIDS.

Njoo nikudunge Mkuu naona umechoka kuishi aisee
 
Kama unaona ni uongo na hakuna vvu nenda pale ambiance au kangaroo pub sinza kapige kavu kama machagudoa 3 au 4 halafu tuletee matokeo. au nenda mwananyala hospital wodi ya ukimwi ukawaokoe na tiba yenu mbadala

Aende Mwananyala ktk wodi ya wagonjwa wa ngoma aka do nao ata watatu hivi aone cha moto
 
Aende Mwananyala ktk wodi ya wagonjwa wa ngoma aka do nao ata watatu hivi aone cha moto

Wagonjwa wa ngoma ? Wanatibiwa nini ? Ndugu yangu nimeambiwa anaumwa nauliza anaumwa nini ? Msemaji ananiambia eti ana ngoma nani kuwadanganya kwamba ngoma ni ugonjwa ?
Kama wako mwananyamala watakuwa na magonjwa yanayowasumbua lakini sio ngoma, acheni kupotosha mnasababisha watu wafe kabla ya nyakati kwa kuwapa ugonjwa usiokuwapo
 
Bado hayajawakuta siku yakiwakuta ndio mtajua kua ngoma si ulambu.....
 
Bado hayajawakuta siku yakiwakuta ndio mtajua kua ngoma si ulambu.....
Mkuu umepotea njia, huku sio jukwaa la michezo useme uropike tu.

Huku ni taaluma tu, na taaluma huthibitishwa na matokeo / uhalisia sio hisia.

Kinyume na hapo vepe morine anauzungumziaje ushindi wenu wa kupewa.
 
Anataka tena apewa mwingine....

Hakuna taaluma yoyote watu wanabisha tu. Mtu yeyeto anabisha ajidunge sindano yenye damu ya mtu wa VVU aone cha moto.
 
mkuu Deception,

Umeongea mambo ya ukweli kabisa kaka. Huo ndo uhalisia wa mambo kwa sasa. Na anaepinga hayo uliyoongea, basi akapimwe akili.

Always the truth prevails. Doctor mkuyati og, kwenye hayo maelezo ya Deception (kwenye red), is there any point that you do completely recognize and agree with ?

Kaveli ulianzisha huu uzi ukiwa na malengo mazuri na ya msingi, lakini bahati mbaya umeingia kwenye lindi la madktari wa vitabu na hoja za kufikirika bila uchunguzi.

Swala la vvu/ukimwi kama kinadharia mnasema ni ugonjwa wa kufikirika lakini kiuhalisia upo na wengine madhara yake tumeyapata. Ninavyoandika hapa nina shemeji yangu ni mgonjwa mahututi. Hitoria ya ugonjwa wake; Miaka 15 iliyopita alipimwa na kugundulika ana vvu wakati huo kinga zilikuwa juu, akaambiwa asiwe na shaka ila akapewa taratibu za kuishi na hali hiyo bila kutumia dawa yoyote. Miaka 5 baadae akaanza kuugua magonjwa tofauti kwa vipindi vifupi, hali ilikuwa mbaya sana daktari walimwanzishia arv. Baada ya kuanza kutumia hizo dawa hali yake ilitengemaa kabisa na kuendelea na maisha.

Mwaka mmoja uliopita aliacha arv akidai yeye ni mzima na hakuwa na sababu ya kuendelea kutumia dawa. Miezi miwili iliyopita ile hali ya kuugua imemrudia kwa nguvu kuliko mwanzo na hali yake ni mbaya sana. Na niko naye hapa silali ninauguza!!

Ujumbe kwa hawa madaktari wetu wa huku mitandaoni;
Jaribuni kuwapa watu kile kitakachowasaidia kihalisia na sio nadharia kama mnavyofanya hapa. Mtaua wengi.
 
Hiyo ni hadith yako wewe , wengine tumepoteza ndugu kwa hizo hizo ARV, UKIMWI ni tatizo lakini hatuwezi kubaki kuwa HIV ndiye muhusika kwa kuwa kuna ARV !
Yuwekee huyo HIV hapa japo picha yake ya zamani tuione
 
Last edited by a moderator:
Kaveli ulianzisha huu uzi ukiwa na malengo mazuri na ya msingi, lakini bahati mbaya umeingia kwenye lindi la madktari wa vitabu na hoja za kufikirika bila uchunguzi.

Swala la vvu/ukimwi kama kinadharia mnasema ni ugonjwa wa kufikirika lakini kiuhalisia upo na wengine madhara yake tumeyapata. Ninavyoandika hapa nina shemeji yangu ni mgonjwa mahututi. Hitoria ya ugonjwa wake; Miaka 15 iliyopita alipimwa na kugundulika ana vvu wakati huo kinga zilikuwa juu, akaambiwa asiwe na shaka ila akapewa taratibu za kuishi na hali hiyo bila kutumia dawa yoyote. Miaka 5 baadae akaanza kuugua magonjwa tofauti kwa vipindi vifupi, hali ilikuwa mbaya sana daktari walimwanzishia arv. Baada ya kuanza kutumia hizo dawa hali yake ilitengemaa kabisa na kuendelea na maisha.

Mwaka mmoja uliopita aliacha arv akidai yeye ni mzima na hakuwa na sababu ya kuendelea kutumia dawa. Miezi miwili iliyopita ile hali ya kuugua imemrudia kwa nguvu kuliko mwanzo na hali yake ni mbaya sana. Na niko naye hapa silali ninauguza!!

Ujumbe kwa hawa madaktari wetu wa huku mitandaoni;
Jaribuni kuwapa watu kile kitakachowasaidia kihalisia na sio nadharia kama mnavyofanya hapa. Mtaua wengi.
Wewe hujapoteza ndugu bado maana huyo anaumwa na anapumua,sisi tumepoteza tayari,tatizo lako hujasoma hii mada maana ilichokisema kimeshapewa majibu humu humu kwenye huu uzi

Tatizo lako wewe unadhani ARVs ni dawa za kuponya ugonjwa fulani wakati sio hivyo,ARV hazitibu ugonjwa wowote ule isipokuwa wanadai zinarudisha kinga ya mwili tu

Huyo mgonjwa wako alikua anaumwa maradhi kama watu wengine na hayo maradhi ndio yaliyokuwa yanamuweka kitandani na sio UKIMWI,alipopewa ARVs alipewa na dawa zingine kwaajili ya maradhi mengine na hapo ndio siri ya afya yake kurudi ilipo na sio kwenye ARVs

Halafu kitu kingine ni kwamba unapaswa ujue kwamba taarifa tu ya kwamba una HIV ni ugonjwa pekee achilia mbali malaria,TB n.k,mtu yoyote hapa akiambiwa ana hivyo vidudu anapanic na kusababisha kuhemkwa na kuanza kuugua na wengi wakianza kuugua wanasema ndio ukimwi umeansa tayari,matatizo ya kuhemkwa husababisha maradhi sana na ndio maana amtu akipewa ushauri anaanaa kipata nafuu kabla hata hajabywa dawa yoyote ile...

Mihemko hushusha kinga ya mwili,kwa maana hii hisia nazo ni major cause ya UKIMWI vile vile na dawa yake ni ushauri tu

Soma mada hii upate majibu zaidi......
 
Last edited by a moderator:
Kaveli ulianzisha huu uzi ukiwa na malengo mazuri na ya msingi, lakini bahati mbaya umeingia kwenye lindi la madktari wa vitabu na hoja za kufikirika bila uchunguzi.

Swala la vvu/ukimwi kama kinadharia mnasema ni ugonjwa wa kufikirika lakini kiuhalisia upo na wengine madhara yake tumeyapata. Ninavyoandika hapa nina shemeji yangu ni mgonjwa mahututi. Hitoria ya ugonjwa wake; Miaka 15 iliyopita alipimwa na kugundulika ana vvu wakati huo kinga zilikuwa juu, akaambiwa asiwe na shaka ila akapewa taratibu za kuishi na hali hiyo bila kutumia dawa yoyote. Miaka 5 baadae akaanza kuugua magonjwa tofauti kwa vipindi vifupi, hali ilikuwa mbaya sana daktari walimwanzishia arv. Baada ya kuanza kutumia hizo dawa hali yake ilitengemaa kabisa na kuendelea na maisha.

Mwaka mmoja uliopita aliacha arv akidai yeye ni mzima na hakuwa na sababu ya kuendelea kutumia dawa. Miezi miwili iliyopita ile hali ya kuugua imemrudia kwa nguvu kuliko mwanzo na hali yake ni mbaya sana. Na niko naye hapa silali ninauguza!!

Ujumbe kwa hawa madaktari wetu wa huku mitandaoni;

Jaribuni kuwapa watu kile kitakachowasaidia kihalisia na sio nadharia kama mnavyofanya hapa. Mtaua wengi.

Siku zote huwa nawaambia watu kama ninyi kwamba; Kuona si kuelewa,au waswahili wanasema kwamba kukaa karibu na mahakama si kujua sheria.Huwa ninasema mara nyingi kwamba,ili uone au usikie kitu na kukielewa inabidi uwe na elimu/uelewa wa kutosha kuhusu kitu hicho.

Sasa soma kwa makini hapa chini ujue tatizo lako liko wapi;

1.".....shemeji yangu ni mgonjwa mahututi...."

Shemeji yako anasumbuliwa na ugonjwa/magonjwa gani?Yataje.Kusema tu mahututi haitoshi.Halafu taja matatizo yake halisi,usiniambie anasumbuliwa na HIV au UKIMWI,sema hasa anaumwa ugonjwa/magonjwa gani,yataje yote.

2."...Miaka 15 iliyopita alipimwa na kugundulika ana vvu..."

Sasa hapa ni vizuri ungetaja sababu zilizomfanya yeye aende kupima,jambo hili ni muhimu sana hata kama utalidharau.Pia ingekuwa vizuri sana ungetuelezea bila kutuficha/kutudanganya kuhusu aina ya maisha aliyokuwa anaishi huyo ndugu yako hasa kwenye suala la misosi,vinywaji,matumizi ya madawa mbalimbali ya hospitali nk kabla hajaenda kupima.Na je,wakati alikuwa anaenda kupima alikuwa na ugonjwa wowote?Mambo haya ni ya msingi pia tukayajua.Usifiche chochote kile kwa lengo la kunikwamisha.

3."....wakati huo kinga zilikuwa juu.."

Hapa inabidi utuambie wazi kwamba ni kinga ilikuwa juu au CD4 zilikuwa juu?Fahamu kwamba kinga ya mwili kwa ujumla ni tofauti na CD4 pekee,unalijua hilo.CD4 pekee sio kinga ya mwili.Sasa tuambie aliambiwaje kuhusu kinga yake,usiseme tu kwamba kinga iko juu,kusema hivi kwa mtu kama mimi unakuwa bado hujasema kitu cha maana.

4."..Miaka 5 baadae akaanza kuugua magonjwa tofauti..."

Narudia tena,yataje hayo magonjwa tofauti ni magonjwa gani?

5."...hali ilikuwa mbaya sana daktari walimwanzishia arv. Baada ya kuanza kutumia hizo dawa hali yake ilitengemaa kabisa na kuendelea na maisha...."

Hapa lazima kuna kitu umekiacha:Kama kweli alikuwa anaumwa magonjwa tofauti,lazima daktari alimpa mgonjwa dawa nyingine za kutibu hayo magonjwa ukiachilia mbali hizo ARVs alizopewa.Tuweke wazi hapa,usifiche,alipewa dawa gani nyingine tofauti na hizo ARVs?Hawezi kupona magonjwa yake hayo kwa kula ARVs pekee,hawezi.Tuambie alipewa dawa gani nyingine.

6."...Mwaka mmoja uliopita aliacha arv.."

Sasa hii ndio sehemu muhimu kuwa makini kusikiliza/kutafakari ili uelewe.Kwa maelezo yako inamaanisha mgonjwa alitumia ARVs kwa miaka takribani 9.Kwa mtu aliyetumia ARVs kwa miaka 9,tayari mwili wake utakuwa umeshajengengewa ARVs dependence/utegemezi mkubwa sana kwenye ARVs,au tunaweza kusema kwamba mwili wake/kinga yake imeshapata addiction kubwa sana kutokana na matumizi ya ARVs kiasi kwamba akiacha ghafla bila shaka lazima baada ya muda usiozidi mwaka 1 ataanza kupata matatizo fulani.Baadhi ya matatizo haya huwa yanaendana kabisa na yale yanawapata watu wanaotumia dawa za kulevya halafu wakaacha ghafla.Matatizo haya hayamaanishi kwamba eti virusi vimeongezeka,la hasha,ni addictive effects tu,si kingine.

Baadhi ya matatizo haya ni kama vile,upungufu wa damu,kukohoa sana,kuwashwa mwilini,homa,kukonda,matazizo ya ini,figo,cancer yoyote na mengine mengi kutegemea na mgonjwa alikuwa anaishi vipi.

7."...Miezi miwili iliyopita ile hali ya kuugua imemrudia..."

Sasa hapa ni vyema ukatuambia anaumwa magonjwa gani hasa.Fahamu pia magonjwa haya hayawezi kutibiwa kwa kupewa tena ARVs,lazima apewe tiba husika za magonjwa husika.Kama ana upungufu wa damu basi aongezewe damu au madini ya chuma/folic acid nk.Madaktari wanalijua hilo,lakini hawampi ARVs kutibu tatizo hilo.Kama anakohoa watampa tiba husika na vivyo hivyo kwa magonjwa mengine.

Sasa tuambie ana magonjwa gani?

8."...Na niko naye hapa silali ninauguza!!.."

Pole sana kwa matatizo hayo.Lakini pia,kwa lengo ni kumnusuru mgonjwa,si vibaya tukashirikiana ushauri.Naomba uniambie anaumwa kitu/vitu/magonjwa gani hasa.Kumbuka,hamna mtu anayeumwa ukimwi,watu huumwa magonjwa yatokanayo na ukimwi bila kujali ukimwi huo umesababishwa na nini(VVU/HIV hasababishi ukimwi).Sasa yataje hayo magonjwa.

Fahamu kwamba,usahihi wa ushauri haujali ni mahali gani umeupata,hata kama umeupata hapa mtandaoni usahihi wake utabaki palepale.

Hebu tuanzie hapo kwanza,mgonjwa anaumwa magonjwa gani?Pia uko naye nyumbani au hospitali?
 
Kama unaona ni uongo na hakuna vvu nenda pale ambiance au kangaroo pub sinza kapige kavu kama machagudoa 3 au 4 halafu tuletee matokeo. au nenda mwananyala hospital wodi ya ukimwi ukawaokoe na tiba yenu mbadala

Mkuu

ikiwa unadhani maambikizi ya HIV yanapatikana tu kwa kufanya mapenzi na machangudoa au watu waliotayari wanamaradhi ya AIDS basi unahitaji msaada mkubwa wa elimu juu ya hili tatizo la HIV/AIDS
 
Situation kama hiyo unaizungumziaje mkuu?

Labda mimi "window period" yangu ni miaka mitatu?, baada ya mwaka mmoja kama nitaendelea ku test negative nitajidunga damu ya mtu HIV postive ili niconfirm uongo huu wa HIV-AIDS.

Mjuni

kabla hujafika hatua ya kujidunga sindano ya damu ya mtu ambaye ni HIV+ ili kupima ama uwepo wa HIV ni halisi au ni dhana ya kutunga yafaa usome hii link hapo chini ambayo pamoja na mambo mengine mengi yaweza kukupa mwanga kwa nini mpaka sasa bado umeendelea kupata matokeo ya HIV-

Putting a number on it: The risk from an exposure to HIV | CATIE - Canada's source for HIV and hepatitis C information
 
haha, nilishakwambia haya mambo zamani sana, tatizo "weye" ni mgumu kusoma alama za nyakati!! nilisema hivii, kwanza ni ngumu sana kwa mtu mzima kupata malnutrition. pili, hata akipata hiyo malnutrition, haishushi kinga ya mwili kiasi cha yeye kupata magonjwa nyemelezi. lakini pia, nilitoa ushahidi humu kwamba asilimia 98 ya watu wote wenye magonjwa nyemelezi kwa ajili ya upungufu wa kinga wamekutwa na HIV. hiyo asilimia 2 unayoitetea ni insignificant!!

halafu, hujiulizi kwanini kule PM sikukujibu? maana you have no reason, bila hata kujali unayemuadress ni nani, unakimbilia kuniambia kwamba utaachisha ndugu zangu ARV,, bila reasoning.wala facts!! ulitegemea nikujibu kweli? when you sound sooo deluded?
hata picha uoni? njoo tena!"

Daktari unanisikitisha sana in the bolded areas: U mean malnutrition affects only children? na kwanini unawaza sana cheo chako ? anyway si lengo langu kupindisha hoja ila nakuomba usome side effects za ARVs taratibu na kutafakari kimya kimya. BEing on medics also, have seen many supposedly said to be + and never used ARV and survived many years. Tusipewe giza kwa elimu tulizosoma zilizokuwa moderated na western juu ya nini tusome huku tukitegemea tafiti zilizopitishwa na journals na associations zao zilizo wekwa kwa manufaa yao. Dhana hizi za HIV na Cancer zahitaji usome na uwe na neutral mind kuweza kuona the hidden myths na agenda behind. Tukifunikwa na ego tu basi tutabaki kuugua na kutawaliwa milele.
 
Situation kama hiyo unaizungumziaje mkuu?

Labda mimi "window period" yangu ni miaka mitatu?, baada ya mwaka mmoja kama nitaendelea ku test negative nitajidunga damu ya mtu HIV postive ili niconfirm uongo huu wa HIV-AIDS.

Mimi sina hata la kusema zaidi naangalia tu na kupata elimu hii,Usijidunge kimya kimya uje uniite nishuhudie na mimi.....
 
Wadau

nimeufuatilia na kuusoma uzi huu kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Nimetambua kuwa nimebahatika kupata nafasi kama msomaji kujifunza mengi na kupanua ufahamu wangu juu ya somo la HIV/AIDS. Pamoja na yote niwapongeze Kaveli, Mzee wa Kigonzile, Eiyer, Pakamwam, Mkuyati og, Deception na wengineo wengi kwa michango yao na hoja nyingi walizozitoa humu katika kutoa elimu na taaluma pia
 
Mjuni

kabla hujafika hatua ya kujidunga sindano ya damu ya mtu ambaye ni HIV+ ili kupima ama uwepo wa HIV ni halisi au ni dhana ya kutunga yafaa usome hii link hapo chini ambayo pamoja na mambo mengine mengi yaweza kukupa mwanga kwa nini mpaka sasa bado umeendelea kupata matokeo ya HIV-

Putting a number on it: The risk from an exposure to HIV | CATIE - Canada's source for HIV and hepatitis C information
Mkuu nashukuru Kwa hiyo link, lakini ukiitafakari vizuri, ni Kama kupaza maambukizi ya vvu Kwa njia ya ngono ni vigumu mno, link inasema, Kufanya mapenzi kinyume na maumbile, ni asilimia 0.06 tu ya uwezekano wa kupata maambuzi, Yaani 1 Kwa matendo 1667!

Kwa njia ya kawaida, ili uambukizwe Mara moja, inabidi ufanye wastani wa matendo ya ngono mara 2500!, yaani hatari ya kupata maambukizi ni asilimia 0.04!

Iieleweke vizuri hapa, Huo wastani wa matendo per infection ni wa kufanya ngono bila kinga na Watu ambao ni HIV positive, imagine!

Nimefanya hesabu rahisi, ili ufanye matendo ya ngono 2500 ndani ya mwezi mmoja ni lazima ufanye ngono mara 83 Kwa siku moja!

Hata kupata maambukizi Kwa mwaka pia ni ngumu maana itabidi huyo Mpenzi wako muathirika ufanye nae ngono Mara 6 kila siku, au uwe unatafuta waathiirika 6 kila siku ufanye nao ngono bila kinga, ......

Kuna kitu ambacho hiyo link haijafafanua, Kwa nini ni vigumu hivyo? Kwamba wakati wa ngono ni ngumu hiyo kupata michubuko?, kama ni kweli kuwa ngono ndio njia kuu ya kuenea Kwa vvu hao wanaosemekana wengi wanaishi na Vvu wamepataje?, walikuwa wakifanya ngono wastani wa mara 6 kila siku na wenye vvu?
 
Back
Top Bottom