V.V.U na Upimaji wake (Coincidences)

Njoo nikudunge Mkuu naona umechoka kuishi aisee
Ong'wise, mwanzo nilikuwa mbishi sana juu ya hili suala, lakini baada ya kufuatilia historia ya ugunduzi wake, nimeona ni usanii mtupu, huyu huyu mgunduzi RObert Gallo aliwahi kuidanganya dunia miaka ya1970 kuwa amegundua kirusi kinachoeneza kansa na kwamba Kansa inaambukiza, baada ya muda mfupi madaktari wenzie wakathibitisha kuwa Kansa haiambukizi na uwongo wake ukafia pale,

Akajipanga tena, alipokuja na hii hadithi ya vvu/ukimwi alikwepa uhakiki wa pamoja(peer review) na wenzie na hii ishu ikapitishwa kiujanjaujanja.
 

That is true. The best efficient way kwa HIV kusambaa ni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (Perintal) kuliko kwa njia ya ngono.
 
Nahisi uwakala wa shetani ndani take kuwafanya watu wafanye ngono bila kujali mambukizi ya virusi
 



Mjuni

sina uhakika wa ufahamu wako kwenye kitu kinachoitwa 'probabilities'. Hesabu zinazoainishwa humo ni kusema kwamba uwezekano wa mtu kupata maambukizi ya HIV kwa namna tofauti ya ngono na 'probabilities' zake. Ukisoma kwa makini kwenye hiyo yaarifa utagundua kuwa haimaanishi kwamba unahitaji kufanya ngono kinyume cha maumbile mara 1667 ili upata maambukizi. La hasha. Kuna uwezekano kwamba tendo lako la kwanza la ngono kinyume na maumbile kwa mtu aliyeathirika likakupelekea moja kwa moja kupata maambukizi.

Vile vile kuna mambo mengine mengi baina ya asiye na maambukizi na mwenye maambukizi yanayoweza kuongeza ama kupunguza hiyo 'probability'. Kwa mfano:

- kuwa na maradhi mengine ya STD kwa mtu ambaye hana maambukizi kunaongeza uwezekano wa kupata maambukizi
- stage ya mtu ambaye ana maambukizi (tafiti zinaonyesha kuwa mtu mwenye VVU ambaye bado yupo kwenye window period na mwili wake bado haujaanza kutengeneza antibodies, huyu ana uwezo mkubwa maradufu wa kuwaambukiza wengine kuliko wale ambao tayari wame-seroconvert)
- mtu mwenye maambukizi ya VVU lakini anatumia ARV mpaka kufikia kiwango ambacho antibodies zake haziashirii uwepo wa HIV, huyu (kwa mujibu wa tafiti) ana uwezekano mdogo kabisa wa kuambukiza wengine

Kwa kifupi mkuu 'probabilities' zote hizo kwa pamoja ndizo zenye kuweza kuweka uwezekano wa hatari iliyo kwa mtu kupata maambukizi kwa kufanya ngono pasipo kinga.


[kwa lugha ya picha ya mchezo wa soka ni sawa na kusema, si kila kosa la mabeki linapelekea kufungwa goli, japo makosa ya mabeki mengi zaidi yanaongezea uwezekano wa kufungwa]

The bottom line is, its is best to use protection regardless the status of one's sexual partner is known or unknown, nadhani ndio maana huyo muhudumu wa afya akatoa ushauri kwako kuwa utumie kinga unapokutana na huyo mpenzi wako ambaye unasema ni HIV+
 
Color.bash;

Kiukweli kabisa Mimi mwenyewe sielewi Nina uelewa kiasi gani Kwenye "probability", ila nilijitahidi tu kuconcentrate Kwenye hiyo link ili nielewe ujumbe wake.

Nilielewa kuwa hizo probability za 1infection per 1667 acts na ile 1 per 2500 ni pale ambapo factors zingine Kama vile Sti's hazipo, Pia naelewa kuwa katika hayo matendo 1667 au 2500 maambukizi yanaweza kutokea katika tendo la 2500 au la 1000 au hata la 1! Kabla sijaeleza kama nitatumia kinga ama la, ningependa kujua Kwa nini hiyo probability iwe ni namba ndogo namuna hiyo?

Wewe mkuu hushangai?, 0.04 na 0.06? Kwa sababu ngono ndio njia juu ya kuenea Kwa Vvu, Kwa nini isingekuwa kwamba hiyo 0.04 ndio uwezekano wa kutopata?, iwe kwamba ukifanya ngono bila kinga na mwenye Vvu Usipopata ni una bahati sana, Kwa nini iwe kupata maambukizi ndio bahati na kutopata ni kawaida?, sababu hasa ni nini?
 
Duh kumbe probability iko hivyo!?
 
Mkuu Aragon, heshima kwako kiongozi.


Mkuu Eiyer alikuuliza hivi :



Wewe ukamjibu hivi :


Mkuu Aragon, I guess wewe ni Daktari by profession. Nafurahi kuona madaktari mnachangia kwenye mada hii ambayo ni very educative kuhusu HIV/AIDS hypothesis.

Nimekuwa interested sana na hayo maelezo yako mkuu, kuna kitu wasomaji wanaweza kujifunza hapo. Naomba utuelimishe kwenye hoja zifuatazo, basing on your knowledge & professionalism.

Hapo kwe RED, nilivyokuelewa mimi ni kwamba mbali na HIV, kumbe kuna 'other factors' zinazoweza kushusha/kudhoofisha kinga ya mwili. Now kwa faida ya wasomaji wa uzi huu, naomba unieleweshe kwenye mambo yafuatayo. Ni vizuri ujibu hoja zote kwa mtililiko kama zilivyo, usijumuishe majibu, yaani jibu kila hoja kama ilivyo (per question):

1. JE, 'Immuno Deficiency' na 'Immuno Supression' ni kitu kimoja au ni tofauti ??

2. JE, kwa lugha ya kiswahili, Immuno Deficiency / Immuno Supression ndo Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI ??

3. Mbali na HIV, je ni factors zipi zingine zinazosababisha Immuno Deficiency or Immuno Supression ??

4. 'Immuno Deficiency' inajitokeza ndani ya neno AIDS (Acquired Immuno Deficiency Syndrome). JE, kuna linkage yeyote kati ya Immuno Deficiency na AIDS ??


Natanguliza shukrani kwako doctor Aragon.

DARASA HURU!

mzee wa kigonzile , everlenk , Deception , color.bash , tindikalikali, Ntuzu , iCode , H1N1 ,
 

Shukrani sana mkuu kwa kuuona umuhimu wa uzi huu. Nafurahi kusikia kuwa umejifunza mengi katika mada hii juu ya HIV/AIDS hypothesis. Na nafurahi sana kuona wachangiaji wanalumbana kwa hoja za msingi kabsa na wasomaji wanapata uelewa mpana kuhusu Ukimwi.

Karibu sana mkuu, tuendelee kushea knowledge with neutral mind, basing on uhalisia na uzoefu huko 'site' . Then wasomaji wataelewa kwa undani kuhusu suala hili la Ukimwi.

Knowledge is power !
 

Mkuu Ngorunde, salaamu kaka.

Malengo ya uzi huu bado ni yale yale mkuu, kwamba wasomaji wajifunze kwa mapana kuhusu Ukimwi. Mimi nipo neutral kabsa katika kujenga hoja zangu zenye kuutafuta ukweli. Nachokoza pande zote mbili kwa hoja za msingi without biasness ili wasomaji wasome na kuelewa vizuri. So, I still heed on the main objective of this informative topic.


Ila kwa kukumbusha tu, kuna hoja za mkuu Deception ambazo bado hujazijibu. Hoja za deception hizi hapa:


Please mkuu Ngorunde, jibu hoja hizo za deception kuhusu huyo mgonjwa wako.
Maswali yanayoulizwa humu na majibu yanayotolewa humu, ndo core ground kwa wasomaji kujifunza na kuelewa.
 
Last edited by a moderator:
1. JE, 'Immuno Deficiency' na 'Immuno Supression' ni kitu kimoja au ni tofauti ??

2. JE, kwa lugha ya kiswahili, Immuno Deficiency / Immuno Supression ndo Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI ??

3. Mbali na HIV, je ni factors zipi zingine zinazosababisha Immuno Deficiency or Immuno Supression ??

4. 'Immuno Deficiency' inajitokeza ndani ya neno AIDS (Acquired Immuno Deficiency Syndrome). JE, kuna linkage yeyote kati ya Immuno Deficiency na AIDS ??


Natanguliza shukrani kwako Aragon.

DARASA HURU!
Mkuu Kaveli ntajaribu kukujibu shortly, naomba nijibu kwa ujumla kama hautalidhika ntarudi point moja moja.
Unajua kinga ya mwili ni somo kubwa sana, ila kwa ufupi niilezee kinga ya mwili inayokuwa provided na seli Hai nyeupe za damu ((white Blood Cells), hizi seli nazo ni collective term zipo za aina tofauti kuna lymphocyte, neutrophils, eosinophils n.k, na hata hizo lymphocyte nazo zipo kwenye magroup madogo madogo mengi tu.
Hizi seli Hai nyeupe za damu zinatukinga na magonjwa mbali mbali.
sasa unaposema immunodeficiency ni term Pana sana, zipo conditions Zaidi ya 100 za immunodeficiency, zimegawanywa kwenye makundi makubwa mawili ambayo ni primary and secondary disorders, primary ni unazaliwa nazo na cause ya most of them ni genetic defect au mutation katika seli hizo nyeupe au products ya seli hizo(antibodies au kuna kitu kinaitwa complement).
Hizo conditions ni very rare (nafikiri kiswahili chake ni nadra sana kutokea), Secondary disorder zinatokana na external source(kitu ambacho hujazaliwa nacho) mfano AIDS, cancer, baadhi ya sumu etc unapozungumzia AIDS ni aina ya immunodeficiency lakini hii Unai-acquire na Unai-acquire after being infected with a virus ambaye ndio tunamwita HIV.
kwenye hizo immunodeficiency nyingine ambazo ni nadra sana kutokea, mtu anapata mara kwa mara maambukizi au infection of certain kind kutegemea na kilichokosekana, kikikosekana kitu ambacho kinakusaidia kukukinga na bacteria wa aina flani basi utapata hayo maambukizi mara kwa mara.
Nadhani wachangiaji wengine waliitumia hiyo term ya ukimwi kwa conditions zote hizo ili waweze kueleweka Zaidi.
Nb: kwenye hiyo AIDS pia S ni syndrome na maana ya syndrome ni kwamba ni mjumuisho wa dalili ambazo zinatokana na ugonjwa flani au condition flani (group of symptoms and signs which correlate with a certain disease)
 
Last edited by a moderator:

Ni kweli lengo ni kujifunza...lakini kwa bahati mbaya mgonjwa wangu amefariki, tumemzika jana.

Nimalize kwanza msiba nitarudi Kaveli
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli lengo ni kujifunza...lakini kwa bahati mbaya mgonjwa wangu amefariki, tumemzika jana.

Nimalize kwanza msiba nitarudi Kaveli

Pole sana mkuu Ngorunde kwa kufiwa na ndugu yako!
 
Last edited by a moderator:



Labda kwa kuongezea alichesema Daktari wetu hapo juu....

- immunodeficiency ni upungufu/ukosefu wa kinga ya mwili (bila kujali nini kimesababisha)
- immunosuppression ni hali ya kupunguza/kuondoa/kuharibu kinga ya mwili ambayo aidha inaweza kuwa kwa kukusudia (katika hali fulani fulani madaktari wanaweza kutoa dawa za kupunguza aina fulani ya kinga ili mwili uweze kukubali upandikizaji wa kiungo cha mwili - mfano figo, ini n.k.) au bila kukusudia(kutokanayo na maradhi, ugonjwa, vijidudu ama vimelea mwilini)
 
Ni kweli lengo ni kujifunza...lakini kwa bahati mbaya mgonjwa wangu amefariki, tumemzika jana.

Nimalize kwanza msiba nitarudi Kaveli

Pole sana mkuu....
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Aragon na color.bash kuna kitu najiuliza sana hapa...

Nakumbuka madaktari walisema hapa kuwa TB kabla haijapatiwa dawa na chanjo watu walikuwa wanaugua sana na kufa lakini baada ta kupatiwa chanjo vifo vya kusababishwa na hata maradhi viliidha kabisa kwasababu unapopewa chanjo mwili unatengeneza askari maalumu kwaajili ya hao bakteria na kuwasambaratisha.....

Wakaendelea kusema kuwa karibia kila mmoja wetu ana hawa wadudu wa bakteria mwilini lakini hatuugui kwasababu hiyo na tutaugua tu pale kinga ya miili yetu itakapopata tatizo

Lakini wakasema kuna kundi la watu ambao wako kwenye hatari ya kuugua maradhi haya,wakasema kundi hili ni lile la wale watu wanaouguza wagonjwa wa maradhi haya ya TB kwasababu wapo kwenye nafasi ya kuambukizwa na wagonjwa hao...

Sasa najiuliza,kwanini sisi ambao tupo huku mitaani na tunakuwa exposed na hawa wadudu kila mara na wakati mwingine tunakuwa nao kwenye miili yetu na hatuugui lakini hawa wanaouguza hawa wagonjwa wawe kwenye hatari ya kupata haya maginjwa wakati wadudu ni wale wale na sote tuna kinga ya chanjo?

Pili,inaonekama huwezi kuugua kama umepewa chanjo kwasababu ya mwili kutengeneza askari maalum wa kupambana na magonjwa haya labda tu kinga yako iwe chini na ni ile inayosababishwa na hiv,mbona kuna watu wanaugua wengi tu na wana chanjo na hawana hiv?

Habu nisaidieni hapo kwanza wakuu.........
 
Last edited by a moderator:

....mkuu unaweka maelezo magumu sana na yame-base sana kwny kiingereza na kisayansi mno kiasi kwmb km mtu hujaenda shule hum ni tatzo....#tunaomba utoe maelezo ya kawaida na yenye lugha nyepesi ili tuielewe kwa pamoja mana huu uzi umewavutia wengi mno#. Ahsante
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…