1. JE, 'Immuno Deficiency' na 'Immuno Supression' ni kitu kimoja au ni tofauti ??
2. JE, kwa lugha ya kiswahili, Immuno Deficiency / Immuno Supression ndo Upungufu wa Kinga Mwilini yaani UKIMWI ??
3. Mbali na HIV, je ni factors zipi zingine zinazosababisha Immuno Deficiency or Immuno Supression ??
4. 'Immuno Deficiency' inajitokeza ndani ya neno AIDS (Acquired
Immuno Deficiency Syndrome). JE, kuna linkage yeyote kati ya Immuno Deficiency na AIDS ??
Natanguliza shukrani kwako Aragon.
DARASA HURU!
Mkuu
Kaveli ntajaribu kukujibu shortly, naomba nijibu kwa ujumla kama hautalidhika ntarudi point moja moja.
Unajua kinga ya mwili ni somo kubwa sana, ila kwa ufupi niilezee kinga ya mwili inayokuwa provided na seli Hai nyeupe za damu ((white Blood Cells), hizi seli nazo ni collective term zipo za aina tofauti kuna lymphocyte, neutrophils, eosinophils n.k, na hata hizo lymphocyte nazo zipo kwenye magroup madogo madogo mengi tu.
Hizi seli Hai nyeupe za damu zinatukinga na magonjwa mbali mbali.
sasa unaposema immunodeficiency ni term Pana sana, zipo conditions Zaidi ya 100 za immunodeficiency, zimegawanywa kwenye makundi makubwa mawili ambayo ni primary and secondary disorders, primary ni unazaliwa nazo na cause ya most of them ni genetic defect au mutation katika seli hizo nyeupe au products ya seli hizo(antibodies au kuna kitu kinaitwa complement).
Hizo conditions ni very rare (nafikiri kiswahili chake ni nadra sana kutokea), Secondary disorder zinatokana na external source(kitu ambacho hujazaliwa nacho) mfano AIDS, cancer, baadhi ya sumu etc unapozungumzia AIDS ni aina ya immunodeficiency lakini hii Unai-acquire na Unai-acquire after being infected with a virus ambaye ndio tunamwita HIV.
kwenye hizo immunodeficiency nyingine ambazo ni nadra sana kutokea, mtu anapata mara kwa mara maambukizi au infection of certain kind kutegemea na kilichokosekana, kikikosekana kitu ambacho kinakusaidia kukukinga na bacteria wa aina flani basi utapata hayo maambukizi mara kwa mara.
Nadhani wachangiaji wengine waliitumia hiyo term ya ukimwi kwa conditions zote hizo ili waweze kueleweka Zaidi.
Nb: kwenye hiyo AIDS pia S ni syndrome na maana ya syndrome ni kwamba ni mjumuisho wa dalili ambazo zinatokana na ugonjwa flani au condition flani (group of symptoms and signs which correlate with a certain disease)