Kwa mujibu wa kalkuleta ya TRA kodi kwa ujumla utatakiwa kulipa TRA $ 2054 ambayo roughly ni kama TZS 3,429,841/- (assumption $1=TZS 1,670/-)..registration ni 270,000/-,shipping line ni 136,000/-,Port Charge ni 300,000/-,Agent Fee ni 200,000/- na plate number ni 38,000/- jumla kuu ni kama TZS 4,373,941/-
Ntajaribu kujibu swali lako kwa kutumia data zifuatazo - ulizozitaja.
MOdel: Toyota Ipsum Picnic
Year: 2004
Capacity: cc 2000
CIF: 3000$ ($2000 FOB $1000 kusafirisha +insurance (kama 4.8m tzs)
Kutoka kwenye Price List ya TRA version 15 (na baada ya ku-google kidogo) gari ulilotaja linafanana
na:
MOdel: Toyota IPSUM ACM 21/26
Year: 2004
Capacity: cc 2362
Price when new (Hapa ndio kwenye ugomvi, kwasababu naamini bei nyingi wamezichakachua!!): 25,014$
Maswali:
1.Ntalipa sh ngapi kulitoa gari bandarini?
TRA wanatumia bei ya gari likiwa jipya, nakufanya mahesabu ya uchakavu ili kujua thamani ya gari kwa sasa.
kwa kutumia Calculator ya TRA, Thamani ya gari hilo ( Toyota IPSUM ACM21/26 - 2004 ) ni: 3,700$
Kodi ya Jumla ni: 2,303$
Naamini kuna gharama nyingine za bandarini - naomba wadau wanazijua watusaidie.
2.Je TRA wanatumia bei hiyo nliyonunulia($2000) au ($3000) kufanya calculations zao
au wana bei maalum kwa gari la aina hiyo nliyotaja hapo juu?
TRA watatumia bei ya chini kabisa ( a minimum of) ya 3,700$ kufanya hesabu za kodi.
Hivi hizi bei za TRA za Magari mapya/yalipokua mapya wanazipata wapi? Mimi nina mashaka nazo sana!
Kwa mfano tuangalie bei zifuatazo za Toyota RAV4
Model Year CC Price
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR ≤ 2003 1800 60,111 <- inawezekana Bei kuwa sawa toka 2000 ->2003 ???
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2004 1800 53,432
RAV 4 ZCA26W 5 - DOOR 2005 1800 51,206
RAV4 ZCA 3-DOOR 2000 1800 50,379
RAV4 ZCA 3-DOOR 2001 1800 57,149
RAV4 ZCA 3-DOOR 2002 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2003 1800 59,825
RAV4 ZCA 3-DOOR 2004 1800 45,481
RAV4 ZCA 3-DOOR 2005 1800 40,932
source Tanzania Revenue Authority - Home
Fananisha bei hizo na bei ya Toyota RAV4 GX 5D Wagon 2013 - $23,300
source: Toyota Rav4 2013 | Crossover SUV
Jamaa wanakisia Ama?
Naambatanisha: Price list ya TRA ya January, 2013 (from Tanzania Revenue Authority - Home)
Halafu kuna Models nyingi za magari hazijawekwa, Je TRA wanatumia njia ipi kupata hesabu za kodi kwa models ambazo hazipo kwenye orodha yao?
Naomba kuelimishwa.
Kabla sijaendelea niseme kwa dhati TRA hawakisii bali naamini
ni research ambazo wanafanya na kwa taarifa tu kuna idara ya
research iliyo na wanataaluma wa kufa mtu kazi zao ni nyingi
ikiwepo hii ya kuestablish best estimates za bei
Umetuambia tufananishe a bei ya Toyota RAV4 GX 5D Wagon 2013 - $23,300.
Lakini hujasema hiyo $ 23,300 ni FOB, CIF or retail price ikiwa TZ
Kufananisha lazima tufananishe vitu vilivyo ktk mazingira sawa.
Kwa kuwa site uliyoweka ni ya Toyota, then hiyo bei ni ya gari mpya
ikiwa japan, na haijalipiwa freight, insurance na kodi. Bei za TRA ni Retail Prices
yaani zimejumuisha kodi zote pamoja na faida kuanzia mtengenezaji hadi retail seller.
Pia tambua bei za mitandaoni saa nyingine ni promotion tu kuvutia watu waweze kujua
na mambo mengine, so ukitaka kujua bei halisi ya Toyota model hiyo kwa nn
usiende hapo toyota tz ukapata quatation? very ease way to clear your doubt zote.
Bei kuwa sawa toka 2000 ->2003 ???
Hapa tambua madhumuni ya kodi sio tu kukusanya mapato bali ina malengo
mengine ya kuadjust consuption za watu na for public interest at large.
Pia assumption ni kuwa consumers are rational ktk consumption.
Ukiambiwa utalipa kodi sawa kati ya 2000 model na 2003 model, ww utanunua ipi?
Kati ya model hizo 2 ipi unategemea kukupa more satsfaction.
The idea behind ni ku discourage kununua magari mabove ili kulinda walaji
na mazingira pia
Kuwa na Model Zote
Kwa TRA kuweza kuwa na Model zote ni ideal situation, and won't be possible
or impacticable. Hilizopo ni gari ambazo zinanuliwa kwa sana TZ na in case kuna
ambayo haipo then hiyo ni exception na exception haikosi soln, kama ilivyo kwenye
mahakama wanapotumia maamuzi yakimahakama yaliyofanywa na watoa maamuzi hapo
kabla au yaliyotolewa maamuzi nchi nyingine zenye
mifumo sanwa nasi (precedent) ktk kuamua swala ambalo linakuwa gumu au linakosa kifungu
sahihi kulitolea ufafanuzi.
Cheers,
Baada ya kusoma huu uzi wote, nimegundua kumbe siku hizi TRA hawahitaji kujua CIF value maana wanakokotoa kwa kutumia bei ya gari ikiwa mpya (bei ambazo wanazo wao), ila wanahitaji kujua mwaka ili kujua kama ni above or below 10 yrs. Nadhani niko sahihi kama nimewaelewa wadau mliotoa comments
Mkuu CLACET (pamoja na wadau wengine) kama unafahamu custom value ya toyota noah 2004 naomba uniambie tafadhali
Mbona TRA hawaji kujibu kama vile hawana afisa mahusiano jamani, kuweni wawazi kwa wateja wenu kwani kuelimishana kwa wastaarabu ni kawaida, mnatuumiza mno nyie TRA mnakuwa hamna huruma na ndugu zenu maskini kisa mmepewa kamshahara kazuri kuliko Dr Ulimboka uuuuffssss....
Fedhuli Tafadhali tuambie ni gari gani na ni la mwaka gani?TRA wanahitaji maandamano, nimenunua gari kwa shilingi 11,300000 kodi wanasema 11,350,000. Calculator inaonyesha nahitaji kulipa kodi ya 4,580,000 inakuwaje jamaniiii! nifanyaje????
TRA kuna matatizo sana,wanalalamikiwa sana but hawana nia ya kijirekebisha au kutoa elimu kwa wateja wao...badala yake elimu inayotolewa ni ya kulipa kodi ila namna gani ukadiriaji wa kodi unafanyika ni wao wenyewe.
TRA wanahitaji maandamano, nimenunua gari kwa shilingi 11,300000 kodi wanasema 11,350,000. Calculator inaonyesha nahitaji kulipa kodi ya 4,580,000 inakuwaje jamaniiii! nifanyaje????
Twende taratibu mkuu hapo kwenye nyekundu, kwa hiyo TRA wanaestablish bei za magari katika mchakato wa kukokotoa kodi wanatumia retail price, kwa maana bei ya gari pamoja na kodi (KODI IPI) wakati kodi ndiyo wanakokotoa?