Vanessa Mdee alistahili tuzo ya mwanamziki bora wa kike

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Japo ni tuzo za Tz ilikuwa haina baja ya kusemea hili maana tulilitegemea lakini ukweli lazima uwekwe wazi.

Lady Jay De hakustahili kuchukua tuzo aliyochukua jana labda jana ilikuwa ni kwa ajili ya wakongwe tuu lakini nafikiri hata tukifuatilia upigaji kura utaona Vanessa Mdee alikuwa anakura nyingi tuu.

Tukiachana na kura kwa sasa na kwa miaka 2 nyuma wakati lady Jay De alikuwa nje ya nchi Vanessa Mdee ndo amekuwa mtu anae iwakilisha vyema Tanzania nje ya nchi kwa upande wa kike hadi kuwa nominated Mara mbili Tuzo za Mtv ameshajijengea mashabaki ndani na nje ya nchi lakini mwisho wa siku anakosa tuzo kisa figisu figisu.

Tunaweza kugues why Vanessa Mdee kakosa tuzo lakini sio mahala pake hapa japo waliotoa tuzo wanajua ukweli walioona mchakato wa hizi tuzo waliamua kukaa mbali.

Lakini kiukweliii Vanessa Mdee alistahili hii tuzo bila ubishi hata iwe kwa mchakato wa kura bado Vanessa ana fan base kubwa kuliko huyo.

Haya ndo yanayofanya watu kususia hizo tuzo ila kwangu mimi kwa mwaka huu Vanessa Mdee ndo the best.
 
Hakika kabisa. Jay Dee hakustahili hiyo tuzo mbele ya Linah potelea mbali Vanessa Mdee.

Vee Pesa kafanya kazi nzuri na zilizohit sana mwaka huu kulinganisha na Jide.

Hapo wanazidi kushusha hadhi za tuzo zao,wameboronga mno.
 
Hivi ile blog ya Millard ayo hawaruhusiwi kuripot habari za burudan zinazoandaliwa na media nyingine tofaut na clauds? Jana ilikua ndo siku ya Tuzo za EATV nimeangalia hawajaripot chochote kuhus hizo tuzo badala yake wameripot tu Skul bash hii ikoje wadau
 
Eatv wameshaanza kuboronga hatua ya kwanza tu ya award wameonyesha upungufu, mdee alistahili na sio Jide.
Ila mwisho wa siku niwe mkweli, binafsi sikupiga kura na kuna uwezekano wengi hawakupiga kura ila tunalalamika.
 
Kura hazikutosha.
Nikikuuliza ulimpigia kura vanessa utaniambia nini?
 
Kura ziliamua mshindi ni Nani hakukuwa Na janja janja sasa kwa wingi Wa Kura unazani Kati ya ya komando Na Vanessa Nani Ana mashabiki kwanza jiulize Je mashabiki Wa Vanessa wako wangapi Na Jay Dee wako wangapi ukijua kwa nini man fongo kapata kuwa chipukizi Bora utajua aina ya wapiga Kura kwa hiyo Jay Dee kwa Kura alistahili kuna muda mziki huu kama unataka mashabiki Wa nyumbani uzungu upungue ili kubalance yeye Vanessa alisema yeye kipimo chake ni kupata Kura ya Grammy award yaani ndio mtoto wake Wa kwanza
 
JayDee ana mashabiki wengi kuliko vanesaa

Jay Dee wimbo wake wa ndindindi ni mzuri kuliko alio toa Vanessa

Jay Dee Jana alitunzwa
Vanesaa hakutunzwa

Jay Dee alipata shangwe
Vanessa aliishia kukodolewa tu
 
Kwani Vanessa ndo nani kashidwa akubali matokeo kwa kipi mtoa Post naona unaandika hadi povu linakutoka. Angalia hata Jana wote waliperform nani alikuwa juu. Vanessa kajichanganya unambabaikia nini. Tuzo zimepita washindi ndo hao kanyaga twenda ajipange tena next season
 
Mee hizi tuzo hata sikuzielewa kabisa ivi na diamond nae alisusia hizi tuzo maana sikumuona kabisa hata wasanii wa kundi Lake hayupo hata mmoja, mwenye kujua anijuze
 
Watu sijui vp?Hiyo ni tuzo ya mwanamuziki bora wa mwaka,sio ya mwanamuziki bora wa miaka 3 au 2!
Kura ndio ziliamua,au unataka nini zaidi?Waliowengi ndio wameshamchagua Jide!Wengi hamjajua kitu,wengi wa fans wamepiga kura kuwaprovoke clouds media group,lakini pia wengine wamepiga kura za huruma baada ya Jide kudhalilishwa na mkojozaji!
Nadhani msg ilifika vizuri clouds,kwamba pamoja na kumfitini Jide,hawezi kufitini feelings walizonazo juu yake!
So anaweza asiwe amefanya vizuri kuliko wasanii wengine lakini kura zikaamua vinginevyo?
 
Mkuu hakuna tuzo duniani zinazokosa mapungufu
Bet wenyewe wanapuyanga
MTV vivyo hivyo so ni haki yako kuwa na mtazamo tofauti ila tuzo ni lawama
 
Hizo kura ulikuwa unaziona acha uongo kijana.. Ndindi hatari huwezi fananisha Komando Jd na Vanessa hata siku moja
 
Mee hizi tuzo hata sikuzielewa kabisa ivi na diamond nae alisusia hizi tuzo maana sikumuona kabisa hata wasanii wa kundi Lake hayupo hata mmoja, mwenye kujua anijuze
Wa kimataifa hawezi cheza mchangani yule
 
JayDee ana mashabiki wengi kuliko vanesaa

Jay Dee wimbo wake wa ndindindi ni mzuri kuliko alio toa Vanessa

Jay Dee Jana alitunzwa
Vanesaa hakutunzwa

Jay Dee alipata shangwe
Vanessa aliishia kukodolewa tu
Vanessa ana jiweka Sana kizungu yule ndo tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…