Hizo nyimbo ni matokeo ya bifu hivyo huwezi kuzitenganisha na bifu. Me
#kende nimemuelewa. Ni kuwa kabla ya hizo nyimbo 2 jide ashaanza kusahaulika kwenye game mpaka alipoingia kwenye bifu akapata cha kuimba... zaid alikua akipiga live band kama akina Banana na TID pale Nyumbani Loungh. Baada ya Nyimbo hizo Mbili za Mipasho kuwananga SebaMaganga,Ruge na Kusaga keshatoa nyingine kama 3 lakini hazijahit. Hata hizo live band zimefulia kwakua hana jipya kila ukienda pale MOG pamenyauka mda wote monday hadi sunday. Hata wasanii wenzie wanamkimbia.
Ni juzi tu watu walijitahidi kuhudhulia kwan wengi walikua Team Kiba.
Vanessa Toka alipochomoka na kwenye featuring ya ommy mpaka wa leo anazidi kupanda kwanini tusiseme kwa sasa kamfunika jayd?
Jide hivi sasa kabaki u-legendary ila kimziki v kamfunika. Tatizo bongo tuna kasumba ya kukariri historia na kuifanya ionekane iko hai muda wote.