Vannesa Mdee: Sipendi kupika

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Akiwa anahojiwa na jarida moja la huko nchini Kenya Vanessa Mdee, afunguka mengi ambayo hajawahi kuyasema sehemu nyingine yeyote ile, na kwa wengi wanaomfahamu mkali huyu wa anayezidi ku make headlines na single yake ya "hawajui", watabaki midomo wazi kwa vile ambavyo walikuwa hawavijui kabisa kuhusu mwanamuziki huyu kutoka Tzee.

Moja ya mambo ambayo vanessa huwa hafanyi kabisa mbali na kuwa mwanamuziki, mtangazaji na mwanaharakati ni kupika, Vanessa alifunguka na kusema hata akiwa nyumbani kwake ishu nzima ya kupika haimjii akili kabisa.

Tofauti na wanawake wengi wa afrika, hii ishu ni moja kati ya vitu vilivyotokea kuwashangaza wapenzi wengi na wadau wanao mzimia Vanessa.

Siku alipotoa hit single yake ya "hawajui", Hii ni moja ya single aliyoitoa kwa watu ambao walikuwa hawamkubali hasa baada ya maneno yao kuzidi kusema kuwa Vanessa hakustahili tuzo ya Kilimanjaro Music Awards aliyoipokea na wengine kusema hakuwa tayari kupokea tuzo hiyo, jambo hili lilimhuzunisha sana Vanessa, hii ilimsukuma Vanessa kuandika kuhusu watu wale ambao walikuwa awamkubali(Haters), na kutoa kitu hiki kinachozidi ku-make headlines kila siku.

Vanessa alifunguka na kusema kuwa umaarufu kama wake unakuja na faida zake mbali na kuwa na vikwazo vingi katika kazi, moja ya faida zake ni kuwa huwa mara nyingi hapangi foleni anapoenda mahali, alizidi kufunguka na kusema siku moja aliwahi kushikwa na polisi barabarani kwa kutofunga mkanda akiwa anaendesha, polisi alivyofika pale Vanessa aka-smile tu na kumuomba msamaha na officer yule akabidi amuachie tu.

Mbali na kufunguka kote huko Vanessa anasisitiza kuwa ni vizuri kwa mtu wa kutokata tamaa katika ndoto zako.
 
Vanessa mtoto wa kishua toka day one.. Its likely hata atakaemuoa ni wa kishua and probably atakufa akiwa wa kishua bado. That's life.. Some people are gifted.. Don't ask why.
 
hajui kupika na kingine mazingira aliyokulia ya kibos bos
 
Basi Millard Ayo ajiandae kuajiri Chef.
Vanessa mtoto wa kishua toka day one.. Its likely hata atakaemuoa ni wa kishua and probably atakufa akiwa wa kishua bado. That's life.. Some people are gifted.. Don't ask why.
 
Huyo mvivu kupika mbona kazi rahisi wengne twapenda kupika wenyewe mh ama kweli we differ
 
Huyu ni bure ukimuoa ni shida tu ni aibu msichana ktujua kupika
 
Ila tusimshangae kuna rafiki yangu mmoja....yeye pia hapendi kupika.....kazi anayoipenda ni kufua.....yeye mpeni nguo hata za ukoo mzima atafua na atazikunja vizuri ila mwambie apike....ni ugonjwa kwake.....
 
Aisee mtoto wa kike unasema kabisa hujui kupika? Mbona Aibu hii...


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
Ila tusimshangae kuna rafiki yangu mmoja....yeye pia hapendi kupika.....kazi anayoipenda ni kufua.....yeye mpeni nguo hata za ukoo mzima atafua na atazikunja vizuri ila mwambie apike....ni ugonjwa kwake.....

Nipe number yake ya simu.

Kufua kwangu ni majanga
 
Na kupika pia hajuii hata kitandan atakua hovyo piaaa (MWANAMKE NI JIKONI) wanajiona wazungu haya aendeleee

Hajui kupiga wala kupiga umbea mtoto wa watu, ila angekuwa mbea angependeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…