Vatican yasisitiza kufanyika kwa uchunguzi huru kufuatia mauaji ya Oktoba 2025

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
7,840
Reaction score
18,115
Kutokana na upotoshaji wa baadhi ya watu kuhusiana na ziara ya Waziri Kombo, huko Vatican; Vatican na Kanisa Katoliki Tanzania kwa kupitia taasisi yake za Kanisa, ya Wasomi wataalam, imetoa ufafanuzi kuepusha upotoshaji:

1. Waziri Kombo alimweleza Papa kuwa Samia ameunda tume kuchunguza matukio ya mauaji kufuatia uchaguzi wa Oct 29.
Taarifa kamili kupitia taasisi ya wasomi wa Kanisa Katoliki ni hii hapa:

TAARIFA RASMI YA CPT ( The Catholic Professionals of Tanzania) Kuhusu taarifa ya Waziri wa mambo ya nje Balozi Kombo huko Vatican:

Kwa Niaba ya: Chama cha Wanataaluma wa Kanisa Katoliki – Tanzania

Dr Nagaikaya Thomas M (PhD)
The Catholic Professionals of Tanzania
Dar es Salaam
Tanzania

Kuhusu: Masuala ya Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vatican, Utendaji wa Kanisa Katoliki, na Heshima ya Mifumo ya Kikanisa:

Chama cha Wanataaluma wa Kanisa Katoliki, kikiwa ni jumuiya ya wasomi na wataalamu wanaolihudumia Kanisa kwa uaminifu wa kiakili, kimaadili na kitaasisi, kinatoa taarifa hii rasmi kwa umma, kwa nia ya kuweka sawa uelewa wa kweli kuhusu namna Kanisa Katoliki linavyofanya kazi, nafasi yake katika jamii, na mahusiano yake na dola na taasisi za kimataifa.

1. Kanisa Katoliki ni Taasisi ya Kisheria, Kihierarkia na Kitaaluma:
Kanisa Katoliki si jukwaa la maigizo ya kisiasa wala taasisi inayoweza kushughulikiwa kwa mbinu za mkato. Ni taasisi ya kale yenye sheria zake (Canon Law), nidhamu ya juu, na muundo wa ki-hierarchical unaoheshimika duniani kote. Maamuzi, mawasiliano na mahusiano yake hufuata taratibu zilizoainishwa wazi na zinazotambulika kimataifa.

2. Vatican na Njia Halali za Mawasiliano ya Kikanisa:
Vatican haifanyi kazi nje ya mifumo halali ya Kanisa. Papa, kama Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, hapokei taarifa, wala kufanya maamuzi, nje ya sheria na taratibu za Kanisa.
Kwa Tanzania, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ndicho chombo halali cha mawasiliano kati ya Kanisa la ndani na Vatican. Kupitia TEC, taarifa huandaliwa, kuchambuliwa na kuwasilishwa kwa uhalali unaotambulika. Ndani ya mfumo huo, Katibu Mkuu wa TEC (Padre Dr Charles Kitima) ndiye msimamizi wa kitaasisi wa mtiririko wa taarifa na mawasiliano ya Kikanisa.
Kwa hiyo, kuruka ngazi na kutegemea mapokezi chanya Vatican bila kupitia TEC ni kinyume na utamaduni, sheria na utendaji wa Kanisa Katoliki.

3. Kanisa Katoliki Lina Mtandao Mpana wa Taarifa Duniani:
Ni muhimu kukumbusha kuwa Kanisa Katoliki lina mtandao mpana wa taarifa katika kila kona ya dunia kupitia Maaskofu, Mabalozi wa Kitume (Apostolic Nuncios), taasisi za haki za binadamu, mashirika ya kijamii, na waamini wake.
Kwa mantiki hiyo, Kanisa haliwezi kudanganywa kwa simulizi za juu juu, propaganda au taarifa zilizochujwa.

4. Wajibu wa Serikali Kuheshimu Kanisa na Kulinda Heshima yake:
Tunasisitiza kuwa heshima ya Kanisa huanza ndani ya nchi. Kabla ya jitihada zozote za kidiplomasia nje ya mipaka, kulikuwa na wajibu wa kushughulikia:
Vitendo vya uzushi, kejeli na udhalilishaji wa Kanisa Katoliki vinavyofanywa na makundi yanayojitambulisha kama “Wakatoliki” bila uhalali wa Kikanisa,
Makundi ambayo kwa matendo yao yanalichafua Kanisa.
Na kuhakikisha kuwa hakuna ulinzi wa kisiasa unaotolewa kwa vitendo vinavyodhalilisha Kanisa, hata pale wahusika wanapojificha chini ya taswira za vyama vya siasa.
Hatua hizi ndizo zingetoa ishara ya kweli kwamba serikali na chama tawala vinajitenga wazi na udhalilishaji wa Kanisa Katoliki.

5. Msisitizo wa Vatican: Haki, Ukweli na Uponyaji wa Taifa:
Kwa mujibu wa taarifa sahihi zilizopo Vatican, msimamo wa Holy See umejikita katika misingi ya haki na ukweli, ikiwemo:
Wito wa kuitisha uchunguzi huru wa kimataifa na wa haki kuhusu matukio ya uchaguzi wa Oktoba 29 na siku zilizofuata,
Na kusisitiza kuwa matokeo ya uchunguzi huo yatumike kuliponya taifa, kukuza maridhiano, na kurejesha imani ya wananchi katika mifumo ya haki na demokrasia.
Huu ni msimamo wa kudumu wa Kanisa Katoliki duniani kote: amani ya kweli haiwezi kujengwa bila haki.

6. Hitimisho:

Tunapenda kuweka bayana kwamba:
Kanisa Katoliki halirukiwi ngazi; linaheshimiwa kwa kufuata taratibu zake,
Halifanyi kazi kwa picha, kauli au shinikizo la kisiasa,
Na litasimama daima upande wa haki, ukweli, na utu wa binadamu, hata pale msimamo huo unapokuwa mgumu kisiasa.
Tunatoa wito kwa wadau wote serikali, vyama vya siasa na jamii kwa ujumla kuliheshimu Kanisa Katoliki kama taasisi huru, ya kimaadili na ya kitaasisi, na kushirikiana nalo kwa uaminifu, ukweli na kwa njia halali.

Imetolewa na:
Chama cha Wanataaluma wa Kanisa Katoliki (CPT)– Tanzania Kwa ajili ya haki, ukweli, na ustawi wa Taifa.⁩
 
Nilijua tu kuwa wameambiwa ukweli lazima kuwepo na uchunguzi huru sio huu wa mchongo wa Chande.

Huwezi kujichunguza.

Kitima aliwaambia hamkumuelewa, huwezi kwenda kwa Papa bila kuanzia kwa Paroko then Askofu, askofu ndiye atakayewasiliana na Papa, ukianzia kwa Papa definitely utarudishwa kwa Paroko.
 
What's is Next nani yuko juu ya Rais au Kiongozi Mkuu wa Nchi na mwenye ushawishi zaidi duniani kuliko wote? Hili ndilo swali walilojiuliza na wakagundua kua ni Papa ila move waliyoichukua ndio imewafelisha kuruka hairakia ya Kanisa yaan nani anaanza na nani anafuatia ni kosa lingine ambalo hawakulifikiria kabla, kwa kilichotokea huwezi kukimbilia kwa Papa kabla ya kuweka sawa ulipokesea maana Papa nae lazima akupe za Uso bila kukuchekea
 
Hii maana yake ni nini kwa sisi waumini wa kawaida wakatoliki ni kuwa hatuyatambui matokeo ya uchaguzi, waraka utaandikwa na utasomwa kwenye makanisa yote.
 
Kutokana na upotoshaji wa baadhi ya watu kuhusiana na ziara ya Waziri Kombo, huko Vatican; Vatican na Kanisa Katoliki Tanzania kwa kupitia taasisi yake za Kanisa, ya Wasomi wataalam, imetoa ufafanuzi kuepusha upotoshaji:
1. Waziri Kombo alimweleza Papa kuwa Samia ameunda tume kuchunguza matukio ya mauaji kufuatia uchaguzi wa Oct 29.
Taarifa kamili kupitia taasisi ya wasomi wa Kanisa Katoliki ni hii hapa:

TAARIFA RASMI YA CPT ( The Catholic Professionals of Tanzania) Kuhusu taarifa ya Waziri wa mambo ya nje Balozi Kombo huko Vatican:

Kwa Niaba ya: Chama cha Wanataaluma wa Kanisa Katoliki – Tanzania

Dr Nagaikaya Thomas M (PhD)
The Catholic Professionals of Tanzania
Dar es Salaam
Tanzania
Kuhusu: Masuala ya Mahusiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Vatican, Utendaji wa Kanisa Katoliki, na Heshima ya Mifumo ya Kikanisa:
Chama cha Wanataaluma wa Kanisa Katoliki, kikiwa ni jumuiya ya wasomi na wataalamu wanaolihudumia Kanisa kwa uaminifu wa kiakili, kimaadili na kitaasisi, kinatoa taarifa hii rasmi kwa umma, kwa nia ya kuweka sawa uelewa wa kweli kuhusu namna Kanisa Katoliki linavyofanya kazi, nafasi yake katika jamii, na mahusiano yake na dola na taasisi za kimataifa.
1. Kanisa Katoliki ni Taasisi ya Kisheria, Kihierarkia na Kitaaluma:
Kanisa Katoliki si jukwaa la maigizo ya kisiasa wala taasisi inayoweza kushughulikiwa kwa mbinu za mkato. Ni taasisi ya kale yenye sheria zake (Canon Law), nidhamu ya juu, na muundo wa ki-hierarchical unaoheshimika duniani kote. Maamuzi, mawasiliano na mahusiano yake hufuata taratibu zilizoainishwa wazi na zinazotambulika kimataifa.
2. Vatican na Njia Halali za Mawasiliano ya Kikanisa:
Vatican haifanyi kazi nje ya mifumo halali ya Kanisa. Papa, kama Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki, hapokei taarifa, wala kufanya maamuzi, nje ya sheria na taratibu za Kanisa.
Kwa Tanzania, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) ndicho chombo halali cha mawasiliano kati ya Kanisa la ndani na Vatican. Kupitia TEC, taarifa huandaliwa, kuchambuliwa na kuwasilishwa kwa uhalali unaotambulika. Ndani ya mfumo huo, Katibu Mkuu wa TEC (Padre Dr Charles Kitima) ndiye msimamizi wa kitaasisi wa mtiririko wa taarifa na mawasiliano ya Kikanisa.
Kwa hiyo, kuruka ngazi na kutegemea mapokezi chanya Vatican bila kupitia TEC ni kinyume na utamaduni, sheria na utendaji wa Kanisa Katoliki.
3. Kanisa Katoliki Lina Mtandao Mpana wa Taarifa Duniani:
Ni muhimu kukumbusha kuwa Kanisa Katoliki lina mtandao mpana wa taarifa katika kila kona ya dunia kupitia Maaskofu, Mabalozi wa Kitume (Apostolic Nuncios), taasisi za haki za binadamu, mashirika ya kijamii, na waamini wake.
Kwa mantiki hiyo, Kanisa haliwezi kudanganywa kwa simulizi za juu juu, propaganda au taarifa zilizochujwa.
4. Wajibu wa Serikali Kuheshimu Kanisa na Kulinda Heshima yake:
Tunasisitiza kuwa heshima ya Kanisa huanza ndani ya nchi. Kabla ya jitihada zozote za kidiplomasia nje ya mipaka, kulikuwa na wajibu wa kushughulikia:
Vitendo vya uzushi, kejeli na udhalilishaji wa Kanisa Katoliki vinavyofanywa na makundi yanayojitambulisha kama “Wakatoliki” bila uhalali wa Kikanisa,
Makundi ambayo kwa matendo yao yanalichafua Kanisa.
Na kuhakikisha kuwa hakuna ulinzi wa kisiasa unaotolewa kwa vitendo vinavyodhalilisha Kanisa, hata pale wahusika wanapojificha chini ya taswira za vyama vya siasa.
Hatua hizi ndizo zingetoa ishara ya kweli kwamba serikali na chama tawala vinajitenga wazi na udhalilishaji wa Kanisa Katoliki.

5. Msisitizo wa Vatican: Haki, Ukweli na Uponyaji wa Taifa:
Kwa mujibu wa taarifa sahihi zilizopo Vatican, msimamo wa Holy See umejikita katika misingi ya haki na ukweli, ikiwemo:
Wito wa kuitisha uchunguzi huru wa kimataifa na wa haki kuhusu matukio ya uchaguzi wa Oktoba 29 na siku zilizofuata,
Na kusisitiza kuwa matokeo ya uchunguzi huo yatumike kuliponya taifa, kukuza maridhiano, na kurejesha imani ya wananchi katika mifumo ya haki na demokrasia.
Huu ni msimamo wa kudumu wa Kanisa Katoliki duniani kote: amani ya kweli haiwezi kujengwa bila haki.

6. Hitimisho:

Tunapenda kuweka bayana kwamba:
Kanisa Katoliki halirukiwi ngazi; linaheshimiwa kwa kufuata taratibu zake,
Halifanyi kazi kwa picha, kauli au shinikizo la kisiasa,
Na litasimama daima upande wa haki, ukweli, na utu wa binadamu, hata pale msimamo huo unapokuwa mgumu kisiasa.
Tunatoa wito kwa wadau wote serikali, vyama vya siasa na jamii kwa ujumla kuliheshimu Kanisa Katoliki kama taasisi huru, ya kimaadili na ya kitaasisi, na kushirikiana nalo kwa uaminifu, ukweli na kwa njia halali.

Imetolewa na:
Chama cha Wanataaluma wa Kanisa Katoliki (CPT)– Tanzania Kwa ajili ya haki, ukweli, na ustawi wa Taifa.⁩
Sasa mnahangaika Nini na Vatican
Wakati nyie ni sovereignty
Ccm inatumia
Nguvu nyingi akili kisoda
 
Screenshot_20260129-114352~2.png
 
Kweli natamani hii serikali mufilisi na ya hovyo ya Mke wa tatu wa mvuvi wa Kasa pale Makunduchi na mchambawima ifeli ila hili andiko la Dr. Thomas ni la mchongo.

Kwanza huyo Thomas anayejita Dr mwenye Phd sio kweli ni Dr pia ni TAPELI aliyewahi kufukuzwa chuo Kimoja hapa nchini tokana na utapeli wake.

Sijui huo udr na uongozi wa wasomi wa RC kutoa wapi. 😂😂
 
BAKWATA is typing........
 
Back
Top Bottom