Vazi lenye nasaba na dini kuvaliwa na Askari kanzu katika Ukamataji linatupa tafsiri mbaya kimataifa kama nchi

Vazi lenye nasaba na dini kuvaliwa na Askari kanzu katika Ukamataji linatupa tafsiri mbaya kimataifa kama nchi

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Moja ya Askari aliyeshiriki Ukamataji Kisutu amefunga kitambaa ambacho uvaliwa na waumini wa dini flani hasa kipindi Cha mfungo na sikukuu kuashiria vazi lenye star na linaloitambulisha dini hiyo kwa watu wengine.

Inapotokea Askari akavaa vazi Hilo na kufanya Ukamataji Tena unaodhaniwa kwenda kinyume kabisa na utu wa mwanadamu hasa pale wanapomkanyaga mtuhumiwa ndani ya gari si Jambo jema. Tunaona vazi hili likitumiwa vibaya na makundi ya kihalifu na ufanya unyama Kama huu na mara zote wenye dini hii wamekuwa wakikemea dini yao kuhusishwa na masuala yakikatili. Askari kanzu aliyevalia vazi ili pale kasitu may be hakua anajua madhara yakutumia vazi ili kwenye kazi zake, may be aliamini ni vazi Kama mavazi mengine na Sasa ameibua mjadala na mjadala huu utakuwa mkubwa Dunia kadri picha hizi zinavyosambaa.

Wito wangu kwa vyombo vya ulinzi na usalama, tujitahidi kuona madhara kabla hayajatokea na kukemea. Askari wetu kuendelea kupita mitaani na vazi hili wakiwa na silaha nikuhusianisha kazi zao na kinachofanyika Somalia na Nigeria ambapo binadamu katili uvaa vazi hili kwenda kufanya ukatili.

Ipo siku watauliza kwanini awavai mavazi ya kiaskofu au kichungaji kwenye magari yao? Pls fanyieni kazi hii siyi sign nzuri vinginevyo mseme mpo kwenye mkakati wakuuchafua utawala uliopo ambao unaongozwa bila itikadi za kidini
 
Kwa hizi fikra zetu kuna kipindi huwa najiuliza sisi kama jamii kama tunapiga hatua za kwenda nyuma au mbele....

Muonekano wa mtu usitumike kama kipimo au fimbo ya kumchapia mtu, bali matendo yake...., kwahio kama alichofanya ni kibaya ingekuwa sawa akifanye sababu yupo uchi ?
 
Mkamatwaji kama ni gaidi, hiyo ndio njia bora kabisa ya kumshika
 
Kwakua haujaweka picha naassume unazungumzia zile scarf za drafti waweza kuta ya rangi nyekundu na nyeupe au nyeusi kwa nyeupe.

Zile hata wanajeshi wa Marekani wanazivaa sana wakiwa huko Iraq na Afghanistan
 
20210813_134708.jpg
 
Huyo polisi ni muhuni,uvaaji gani huo? Yeye kavaa hivyo imamu,ustadhiau shekhe avae nini?
 
Back
Top Bottom