RIPOTI YA ICC, kipengele cha 79.
Mnamo Oktoba 29, kikosi cha kupambana na magendo cha Zanzibar (KMKM) kilitumwa Dar es Salaam kwenda kukandamiza maandamano kwa nguvu. Kikiwa kimepewa maagizo ya “kupiga risasi ili kuua” wakati wa amri ya kutotoka nje, maafisa hawa waliovaa barakoa waliungana na kikosi kingine kikubwa chenye kuogofya.
Operesheni hiyo iliendana na taarifa za kutisha kwamba baadhi ya Wazanzibari walikataa kuchukua hatua dhidi ya ukandamizaji mkali uliofanywa dhidi ya Watanganyika, huku Zanzibar ikiendelea kuwa tulivu. Uzembe huu unaashiria kutokuwa na maslahi kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu.
===============
On October 29th, the Zanzibar anti-smuggling police unit (KMKM) was sent to Dar es
Salaam to violently suppress protests. Ordered to shoot to kill during the enforced curfew,
these masked officers joined a broader, menacing task force. The operation coincided with
disturbing reports that Zanzibaris refused to act against brutal crackdowns on Tanganyikans,
whilst Zanzibar remained calm. Such apathy signals alarming indifference to human rights
abuses. Reports of violence and impunity are mounting. Activists point to the fact that
President Hassan is a Zanzibari (the first to ever hold the title) and that she spared Zanzibar
from the killings and focused her wave of terror only against Tanganyikans
==================
Taarifa za vurugu na ukosefu wa uwajibikaji zinaendelea kuongezeka. Wanaharakati wanaelekeza lawama zao kwenye ukweli kwamba Rais Hassan ni Mzanzibari (wa kwanza kuwahi kushika nafasi hiyo) na kwamba aliyeacha Zanzibar bila kuguswa na mauaji hayo, huku mawimbi ya vitisho na ukatili yakielekezwa kwa Watanganyika pekee.
Kulingana na uchunguzi wa awali wa International Criminal Court -ICC, vikosi vya KMKM, Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magengo, kiliingizwa Tanzania Bara, hususan Dar es salaam.
Kikosi hicho likihusika kuua waTangayika.
Hii ni habari mbaya, mbaya , mbaya sana.
Aliyevileta vikosi hivyo kuja kuua waTanganyika haieleweki alikuwa na nia gani.
Halafu hao KMKM na Vikosi vya Idara Maalumu SMZ vya Bw. Kheir walibuni lugha yao, kujaribu kujipa uficho ili kusingizia wageni.
Kumbe mbinu hizo siyo siri, zilishatumiwa na wengi kwa uzuri na ubaya.
TOMA MAKTABA :
PROPAGANDA YA UWEPO WA WAGENI, NI MFU NI VYOMBO VYETU NDIYO HAO "WAGENI' AMBAO HATA SAMIA ALIDAI WAPO NCHINI
Katika ulimwengu wa vyombo vya usalama, kujitungia lugha isiyoeleweka na wenyeji siyo jambo geni.
Lakini ni jambo geni hasa pale vyombo vinapotumika kuuwa raia wake ndani ya mipaka ya taifa lao kama ilivyotokea kati ya tarehe 29 Oktoba 2025 na tarehe 02 November 2025 nchini Tanzania
Historia inaonesha wakati wa vita kuu ya dunia World War II taifa la Marekani ilipokuwa inapigana na taifa la Japan, wajapani walikuwa wamejitayarisha kuimanya lugha ya kiEnglish almaarufu Kiingereza. Hivyo operesheni zote za Marekani wajapani walikuwa na uwezo wa kusikiliza na kutumia advantage hiyo kupambana na Jeshi la Marekani
Hivyo kuzuia turufu ya Wajapani kufahamu operesheni za wamarekani, jeshi la Marekani liliamua kutumia lugha ya jamii ya wahindi wekundu wa Marekani katika mawasiliano ili kuzima turufu waliokuwa nayo Wajapani kuelewa operesheni za Jeshi la Marekani.
Kabila hilo dogo la nchini Marekani iliwapa usiri mawasiliano na pia operesheni zao kutofahamika.
Kabila hilo ndani ya Marekani likipatikana Navajo na ndani ya jeshi la Marekani walikuwapo wanajeshi wao waliokuwa wanazungumza lugha hiyo isiyo fahamika kwa Wajapani. Lugha hiyo ilipewa jina Navajo Code Talkers
Sasa turudi nchini Tanzania madai ya kuwepo wageni wanaopiga risasi wageni au wageni kukamatwa ni propaganda za vyombo vya usalama vya Tanzania.
Ambapo vyombo hivi vya usalama walitunga lugha yao ya siri ya kioperesheni ambayo raia wa makabila 120 yaliyopo Tanzania hata yale makabila ya mpakani hawajawahi kuisikia lugha hivyo ya kutunga ya vyombo vya usalama vikiwa vinatekeleza mauaji kwa kutumia maneno yasiyofahamika na waTanzania lakini yanayo toa ufahamu vyombo kushambulia, kukimbia, kurudi nyuma, kuondoka n.k