'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

Vestiges ni viungo katika miili ya wanyama ambavyo vinaweza visiwe na kazi katika baadhi ya wanyama lakini vinakuwa na muhimu na ni vya lazima katika miili ya wanyama wengine.

Mfano 'tail bone' / mfupa wa mkia hauna umuhimu wowote katika mwili wa binadamu maana hatuna mikia sisi, lakini tunao mfupa huo; mfupa huo ni lazima na ni muhimu sana kwa wanyama wenye mikia kama ngedere nk. Hii inashiria kwamba hapo awali binadamu tulikuwa ni kiumbe tofauti kabisa kilichokuwa na mkia ila kwa sasa kiungo hicho kimepotea sababu matumizi yake hayapo tena. (If you don't use it, loose it), hii ndio principle inayotumika katika evolution.

Vestiges zipo nyingi sana katika animal kingdom, mfano nyangumi ana mifupa ya miguu iliyojificha ndani japo hana miguu,hii inashiria kwamba hapo awali alikuwa ni mnyama wa ardhini aliyetembea, na tena bado anazaa na kunyonyesha kama wanyama wengine wa ardhini na sio kutaga mayai kama wafanyavyo samaki.
Vestiges ni nyingi sana, tusaidiane kuziorodhesha na kuzichambua vilivyo na kwa undani kabisa.

Sasa binadamu mwenye akili timamu anaweza weza vipi kuamini kwamba binadamu aliumbwa kama alivyo leo hii na mwonekano wake huu wa sasa, yaani hakubadilika kutoka aina moja ya muonekano hadi kufikia huu muonekano wa sasa. Huwa mnatumia mbinu gani kujitoa akili kwa kiwango hicho?! Mbona mi nashindwa kabisa??!!!

=============================
Mfano mwingine ni kifuko cha appendix kwenye utumbo wa binadamu, kwetu hakina kazi lakini kwa wanyama wanaokula mimea huwa wanakihitaji sana hicho kifuko na kinakuwa ni kikubwa sana kwao na huwasaidia kwenye kusaga chakula, hii inaashiria kwamba tulikuwa mnyama mmoja ila kila mmoja akabadilika kulingana na mazingira yake..
=============================

Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
=============================

=================================
Update: 27/08/2021
Mifupa ya nyangumi mwenye miguu ‘dating millions of years ago’ yapatikana.

View attachment 1912340
_______________________________
WaChina ni WaAfrika waliohama na kubadilika kutokana na mazingira

Kuhusu kifuko cha appendix hata kwenye mwili wa binadamu kina kazi hasa jamii za maporini wanaokula mimea. Wewe wa daslam unauekula chipsi yai huwezi elewa.

Tatu: mijusi kutohitaji viungo vya uzazi wakti huohuo unasema wanatumia kujistqrehesha sijakuelewa.

Hiyo miguu ya nyangumi ni imaginary 100%
 
Hoja yako ya kwanza kuhusu mkia.

Siku nikioneshwa skeleton ya binadamu na kuoneshwq mahali uti wa mgongo ulipoqnzia na kuishia, kisha nioneshwe huo mkia nitawqelewq sana wanasqyansi

View: https://youtu.be/h1NHVDOQKjg?si=JFrurvO9YIJcFqhe

Coccyx au kwa jina lingine ‘Tail bone’. Ina consist of 3 to 5 vertebrae. Yaani hata sasa wapo binadamu wana pingili 3 za mfupa wa mkia na wengine wana pingili 5, kutegemeana na level ya evolution katika kuupoteza mkia. Na kupitia adaptive capabilities, kwa sasa hakitumiki tena kushika mkia kama ilivokuwa awali..
 
Kuhusu kifuko cha appendix hata kwenye mwili wa binadamu kina kazi hasa jamii za maporini wanaokula mimea. Wewe wa daslam unauekula chipsi yai huwezi elewa.

Tatu: mijusi kutohitaji viungo vya uzazi wakti huohuo unasema wanatumia kujistqrehesha sijakuelewa.

Hiyo miguu ya nyangumi ni imaginary 100%
Binadamu akikatwa appendix anaweza kuishi bila kupungukiwa chochote na bila athari yeyote. Ila wanyama kama Sungura, ukikata hicho, hatoweza kuishi katika mazingira yake ya asili na kula na kisaga chakula chake cha asili, na aanaweza kupoteza uhai. Hii ina maana hata kwetu kilikuwa na umuhimu sawia hapo awali, ila baada ya mazingira ya lisje kubadilika, kwa sasa hakina kazi, na eventually ikitazidi kuwa kidogo na kupotea kabisa mwishowe kupitia mutation na natural selection.

Kuhusu mfano wa hao mijusi, tofautisha ‘need’ and ‘want’. Viumbe vinavyozaliana kwa kujamiina vina hitaji (need) tendo kujamiiana ili kuzaliana., ila pia huwa tunataka (want) tendo la kujamiiana pasi na lengo la kuzaliana kwa ajili ya kujiburudisha, ndio maana tunatumia condom au kwenda kinyume na maumbile, ni burudani tu.
Viumbe vinavyozaliana ‘asexually’ hawahitaji (need) tendo la kujamiiana ili kuzaliana, ila kwa kuwa zile zana bado zipo ambapo kwa sasa hazina ‘kuhitajika’ katika kuzaliana, wanazitumia kwanupande wa burudani, japo awali walizitumia kwa kuzaliana.

Kuhusu hiyo mifuoa ya miguu kwa nyungumi ambae hana miguu, mifupa ipo , angalia video chini…

View: https://youtu.be/qvX_BV_Cgtc?feature=shared
 
Hahahaha bwana mdogo kaingia kwenye mfumo. Kumbe umekiri kwamba muanzilishi yupo. Basi taratibu pia utajua kwamba hatujatokana na kiumbe kimoja
Mwanzilishi wake yupo, hakuna anaepinga, ila kinachojadiliwa ni namna viumbe mbali mbali vilivyotawiwika kutoka kwenye kiumbe kimoja cha kwanza (single celled organism)
 
Yani unakufuru huku unajiona wewe ndio mjanja. Haya tuseme tuli-evolve kutoka muonekano fulani kwenda mwingine, tusaidie sasa huo muonekano wa asili wa kila kiumbe kilitokea wapi? Nani alikisimika hicho kiumbe cha awali cha jamii za aina mbalimbali za wanyama na mimea (spiecies)?

Acha jeuri, fanya toba na umtukuze Mungu Muumba wa vyote ukiwemo wewe. Muda wako ni mchache tu hapa duniani, ukishakufa (kama unaamini utakufa), ambalo ni jambo la lazima hutakuwa na muda tena wa kutubu.

Namwomba Mola asije nifanya kumkufulu yeye na namwomba anipe mwisho mwema hapa duniani. Allahu akbar
 
Hahahaha bwana mdogo kaingia kwenye mfumo. Kumbe umekiri kwamba muanzilishi yupo. Basi taratibu pia utajua kwamba hatujatokana na kiumbe kimoja
Onyesha sehemu moja tu ambayo nilisema hakuna mwanzilishi, japo kuna uwekano pia hayupo mwanzilishi, si hoja hapa. Hoja ni process ya uumbaji, kwamba hatukuumbwa kuwa tulivyo leo, bali ni mchakato wa mabadiliko unaoendelea (evolutionary process).
 
Yani unakufuru huku unajiona wewe ndio mjanja. Haya tuseme tuli-evolve kutoka muonekano fulani kwenda mwingine, tusaidie sasa huo muonekano wa asili wa kila kiumbe kilitokea wapi? Nani alikisimika hicho kiumbe cha awali cha jamii za aina mbalimbali za wanyama na mimea (spiecies)?

Acha jeuri, fanya toba na umtukuze Mungu Muumba wa vyote ukiwemo wewe. Muda wako ni mchache tu hapa duniani, ukishakufa (kama unaamini utakufa), ambalo ni jambo la lazima hutakuwa na muda tena wa kutubu.

Namwomba Mola asije nifanya kumkufulu yeye na namwomba anipe mwisho mwema hapa duniani. Allahu akbar
Kwani wapi nimesema hakuna aliyekisimika? Hiyo si hoja hapa. Mimi naongelea kwamba hatukuumbwa kuwa kama tulivyo leo , bali ni mchakato wa mabadiliko hadi kufikia tulivyo leo, na huo mchakato wa mabadiliko bado unaendelea (evolutionary process).
 
Ok Ni sawa kwa hoja yako lkn Kuna kasehemu uliongea kwamba binadamu mwenye akili hawezi kukubali kwamba Mungu aumbe samaki mwenye alama za macho lkn Ni kipofu.

Upande wangu siwezi kubisha juu ya badiliko coz alietuumba anauwezo wa kulishape jambo ambalo hakuliumba ili lije kutokea baadae. Mfano Ni mvi, mav*zi, kubarehe, nk.
Vilevile Kuna muziki, pesa, ambavyo havikuwapo japo alijua kwamba lazima vitakuja kuwepo.

Upande wa vestiges pia Ni hivyo kwa mabadiliko ya kimwili kulingana na mazingira. Maana adamu akifufuka leo anaweza kudhani dunia nzima imejaa watoto kumbe Ni watu wazima walio badilika maumbile kwa msaada wa mazingira.
Onyesha sehemu moja tu ambayo nilisema hakuna mwanzilishi, japo kuna uwekano pia hayupo mwanzilishi, si hoja hapa. Hoja ni process ya uumbaji, kwamba hatukuumbwa kuwa tulivyo leo, bali ni mchakato wa mabadiliko unaoendelea (evolutionary process).
 
Ok Ni sawa kwa hoja yako lkn Kuna kasehemu uliongea kwamba binadamu mwenye akili hawezi kukubali kwamba Mungu aumbe samaki mwenye alama za macho lkn Ni kipofu.

Upande wangu siwezi kubisha juu ya badiliko coz alietuumba anauwezo wa kulishape jambo ambalo hakuliumba ili lije kutokea baadae. Mfano Ni mvi, mav*zi, kubarehe, nk.
Vilevile Kuna muziki, pesa, ambavyo havikuwapo japo alijua kwamba lazima vitakuja kuwepo.

Upande wa vestiges pia Ni hivyo kwa mabadiliko ya kimwili kulingana na mazingira. Maana adamu akifufuka leo anaweza kudhani dunia nzima imejaa watoto kumbe Ni watu wazima walio badilika maumbile kwa msaada wa mazingira.
1.) Mungu hakuwahi kuumba samaki mwenye vishimo vya macho ila hana macho, hajawahi. Kama Mungu yupo, na kama aliumba, basi aliumba single celled organism mmoja tu, aliyetawiwika kuwa viumbe hai vyote unavyoviona leo, ikiwemo mimea, wanyama nk., vyote vimetokea kwa cell hiyo moja. Ndio maana cell structure ya mimea na ya wanyama inafanana kwa zaidi ya asilimia 90.

2.) Hayo mengine ni vizuri kwamba tunakubaliana sasa..
 
In Tanzania what we have is bunch of christian doctors, engineer, bankers, businessmen, politicians etc

Science age is near, endelea kuwaelimisha hawa wanazuoni, focus on Darwinism etc.....
 
Huko unakoenda ni mbali, hawa wanaokataa sio wanyama wanaishi kwenye nchi yenye jamii ya hunter gatherer, na bado wanashindwa kuona,

Na kingine tunachokikataa ni kwamba tunaishi kwenye modern world where common sense is more applicable than historical sense, ni aibu kwa mushi wa kibosho kusema alizaliwa eden
 
Hili swali la Evolution na Uumbaji mimi huwa najibu sijui maana sikuwepo na hilo si kosa langu kikubwa me naishi na nazalisha basi.
 
Ah! Haya Mambo bado Ni magumu sana kiukweli. Maana ukitafakari vizuri sidhani Kama Kuna kiungo ambacho kipo pasina kazi mwilini.
Mf. Appendix inakazi yake ambayo Ni kutunza mchanga ambao tunakula kwabahati mbaya na hii kwa binadamu kujaa Ni Mara chache sana, maranyingi huwatokea eidha wanaopendelea ukoko vyuoni na sehemu za masherehe ambapo uangalifu wakuchambuliwa mchele Ni mdogo.
Au wajawazito wanaokula udongo. Hata Mungu kaiweka akijua sisi tunautashi wa kuepuka kula mchanga lkn inapotokea tumekula bahati mbaya basi appendix inahusika Sasa.
 
Hahaha shahawa sio majimaji tu ni mbegu. Alafu zile zimebeba kila kitu muhimu kumuhusu binadamu.
Mungu Ni special sana. Namna alivyomsuka mwanadamu inastaajabisha sana. Mara nyingi nilikuwa nikidhani kwamba wasomi hasa wa biologia ndio wawe mstari wa mbele kueleza ukuu wa huyu Mungu. Duh! Kumbe Mambo Ni tofauti kabisa mzee, kuongeza maarifa kumeongeza wazimu.

Mambo yapo kwa ustadi wa hali ya juu sana, sio tu katika miili yetu Bali hata katika mazingira. Nakubali mstari mmoja wa bibilia unasema alivichagua vinyonge vya dunia ili kuviaibisha vyenye nguvu. Coz anaelewa kwamba ukishakuwa msomi tu utahitaji kuabudiwa na kusahau matendo makuu ya Mungu atusaidie Sana.
 
View: https://www.instagram.com/reel/DCUaQ3PKTtx/?igsh=MXVpb3FkOTRveWRyZA==

Hapa natural selection ime ‘favor’ unene, angekuwa mwembamba hapo ndio ingekuwa bye bye, hii ndio natural sselection and elimination ya evolution inafanya kazi. Kwa mantiki hii, huyo bonge amepewa chamce ya kusambaza mbegu zake za unene kwa vizazi vijavyo, maana unene umekuwa favourable kwa survival katika mazingira ya kutekana, na ikiendelea hivi watz wote wata’adapt’ na kubadilika kuwa mabonge.
 
Ingekuwa kweli bin Adam tumeibuka tu from no where naamini yafuatayo yangekuwa yanatokea duniani:

1. Race zingekuwa nyingi sana.
2. Kuna kizazi kingekuwa hakiongezeki kwa kuzaliana kwa njia ya tendo.
3. Watoto wanaozaliwa wangeacha katika hatua za ukuaji kuanzia mimba hadi anafikia mtu mzima i.e uniformity isingekuwepo ya kuzaliwa.
4. Kifo kingekuwa kwa sababu ya umri na ajari tu.
5. Kuna watu wangekuwa na umbo tofauti na la kibinadamu.

NB: Dhana ya Single Source ni kwa Mungu tu.Sisi sote tumetokana na Mungu mmoja ila sio mzazi mmoja(Adam & Eve).
 
Ujinga wenu usiwe kinga ya kutojua mambo.Watu wanahoji miaka milioni 200 juu ya sisi wanadamu kuijua mbona ni michache sana hiyo?Uranium-lead dating technique yawezapima umri wa miamba tangu big bang mpaka sasa.Sasa hako kamungu kenu ambako hakajulikani(atheotatous) si kujilisha upepo wa ujinga kwa kuzifunga fahamu zenu?
 
Back
Top Bottom