'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

'Vestiges' kwenye miili ya wanyama, ushahidi tosha kwamba hatukuumbwa, bali tuli-'evolve' kuwa tulivyo

Msandawe anawinda halafu ashindwe kuwinda? Sijaelewa

Hapo sehem ya pili umeongelea adaptation nimekuelezea inavyofanya kazi na jinsi pia evolution inavyofanya kazi

Okey kama kwa mfano wako huo turudi nyuma kwamba tukianza kukaa nje wala moto hakuna tutaota manyoya tena? Sijui kama nakuelewa ndugu
Simple ulisema kuwa kuna misuli ambayo tunayo na haifanyi kazi kwa sababu ya ukuaji wa teknolojia kwamba zamani tulikuwa tunakimbiza mnyama na kumkaka kisha kumuuwa but now days tunatumia silaha za mbali so ile misuli iliyokuwa inatumika kuwindia kwa kukimbia haifanyi kazi (Though kwa kuangalia body anatomy ya binadamu na kwa uchunguzi wa sokwe na primates wanaokaa kwenye captivity hawajaonesha dalili yoyote ya kupungua muscle mass kwa generations za mbele hali ya kuwa wapo sehemu moja na vyakula ni vingi without fear ya kuuwawa na wanyama wengine pia hawajishughulishi kama wa porini) kingine nikakwambia ufuatilie jinsi jamii ya watu wa xoxa (hii ni error nilimaanisha watu wa SAN wanawinda kwa kukimbiza mnyama au ( persistance hunting) akichoka ndo wanauwa.)

Msandawe nimeuweka kumaanisha yeye alikulia maisha ya kuwinda kama wenzake ila baada ya kuanza kazi ya ku ekti muvi alibadili jinsi anavyoishi kwa muda mrefu (ukizingatia yeye pia ni mtu wa kabila la SAN) sasa je? kwa kuwa aliacha kazi ya uwindaji inamaanisha watoto aliopata mbeleni baada ya kuacha uwindaji watakuwa na baadhi ya misuli isiyofanya kazi?
 
Nimekujibu pia evolution theory sio lazima mbona huelewi? Sio law ni theory ambayo inachagua kutokana na nature ya kila kiumbe. Sio kama gravity kwamba kikienda juu lazima kurudi Chini

Inawezekana sina taarifa za kutosha wewe sema kwanini habadiliki? Ninachangia kwa jinsi ninavyofahamu mkuu kwa jinsi nilivyosoma na ninayoyaona field (Geo ) ila haimanishi mimi najua kila kitu
kuto kuwa affected na changes zozote since their first appearance hii inatosha kusema EVOLUTION THEORY IS A JOKE.
 
Simple ulisema kuwa kuna misuli ambayo tunayo na haifanyi kazi kwa sababu ya ukuaji wa teknolojia kwamba zamani tulikuwa tunakimbiza mnyama na kumkaka kisha kumuuwa but now days tunatumia silaha za mbali so ile misuli iliyokuwa inatumika kuwindia kwa kukimbia haifanyi kazi (Though kwa kuangalia body anatomy ya binadamu na kwa uchunguzi wa sokwe na primates wanaokaa kwenye captivity hawajaonesha dalili yoyote ya kupungua muscle mass kwa generations za mbele hali ya kuwa wapo sehemu moja na vyakula ni vingi without fear ya kuuwawa na wanyama wengine pia hawajishughulishi kama wa porini) kingine nikakwambia ufuatilie jinsi jamii ya watu wa xoxa (hii ni error nilimaanisha watu wa SAN wanawinda kwa kukimbiza mnyama au ( persistance hunting) akichoka ndo wanauwa.)

Msandawe nimeuweka kumaanisha yeye alikulia maisha ya kuwinda kama wenzake ila baada ya kuanza kazi ya ku ekti muvi alibadili jinsi anavyoishi kwa muda mrefu (ukizingatia yeye pia ni mtu wa kabila la SAN) sasa je? kwa kuwa aliacha kazi ya uwindaji inamaanisha watoto aliopata mbeleni baada ya kuacha uwindaji watakuwa na baadhi ya misuli isiyofanya kazi?
Maisha ya xhosa anayeishi mjini (Huyo mwenye kazi ya uigizaji ) na yule aliyebaki kijijini anawinda kwa kukimbiza katika tofauti ya miaka 200 hawawezi kuwa Sawa

Ngoja niishie hapo
 
Nadharia ya evolution bado changa na haijitoshelezi.
Kwa mfano tendo la kuzaa ni la uchungu sana, sasa evolution kwa nini usifanye kazi yake?
Pengine angalau tutage tuatamie kama kuku.
Toto la kilo sita la nini?
Jinsi mama anavyozaa kwa uchungu ndivyo jinsi anavyomthamini na kumlinda mtoto wake kwa nguvu zake zote. Kwahiyo jinsi mama alivyopata uchungu zaidi mkali zaidi, ndivyo uwezekano wa huyo mtoto kusurvive hadi utu uzima unakuwa mkubwa, na wale ambao hawakupata uchungu walidharau na hawakulinda sana watoto wao na wakapoteza maisha, hivyo wakabaki wanao zaa kwa uchungu mkali.
 
Kuhusu uwepo wetu (binadamu) duniani naona theory zote zinafanana maana zinasema binadamu ndiye kiumbe wa mwisho kuja duniani. Tofauti ni maelezo ya jinsi alivyopatikana.

Sayansi inasema kuwa viumbe wa kwanza walikuwa majini na dini hivyo hivyo, wakafuatia viumbe wengine wa nchi kavu kabla ya binadamu na dini pia inasema hivyo.
Baadae tukafuata ama kwa mageuzi isemavyo sayansi ama kwa kuumbwa isemavyo dini.

Mtoa mada naungana naye kuwa yawezekana Mungu aliumba kiumbe kimoja tu chenyewe kikaendeleza kazi iliyosalia

Yaani ni kama vile tunavyoendelea kuzaana leo, tukiamu kuacha kuzaana tutaisha wote
 
Bado hii hai prove kwamba hatukuumbwa .
Hatukuumbwa kuwa binadamu complete kama tulivyo leo, bali kuumbwa kwa kupitia hatua kwa hatua from a single celled organism in sucessive stages, hiyo sawa.
 
Kama Mungu Aliumba Adam na Hawa wakaijaze dunia, je mbona Kuna muafrica, mzungu, mchina, Mwarabu na tuna tofauti sana . Je nini kilitokea ?
Hamna kitu kama Adam na Hawa, kilichotokea ni evolution from a single celled organism- (Mutation, adaptation and natural selection through evolution)
 
Kuna haja gani kuzaana kuwepo ilihali vitu vinatokana na evolution?
achana na ujinga wa kizungu
Eti miaka milioni 200
Chukulia tu miaka 100 iliyopita ,ongezeko la watu kwa miaka hiyo, maendeleo ya technolojia kwa miaka hiyo 100 ,halafu uassume miaka milioni
Think out of the box
za kuambiwa changanya na zako
Reproduction is a tool and a necessity in evolution, evolution through mutation, adaption and natural selection imechuja na kuchagua njia tunayotumia kwa ajili ya procreation (kuzaa) kwamba ndio njia sahihi kwa mazingira tuliyonayo katika kusurvive. Unless ulimaanisha kitu kingine..
 
Kuhusu uwepo wetu (binadamu) duniani naona theory zote zinafanana maana zinasema binadamu ndiye kiumbe wa mwisho kuja duniani. Tofauti ni maelezo ya jinsi alivyopatikana.

Sayansi inasema kuwa viumbe wa kwanza walikuwa majini na dini hivyo hivyo, wakafuatia viumbe wengine wa nchi kavu kabla ya binadamu na dini pia inasema hivyo.
Baadae tukafuata ama kwa mageuzi isemavyo sayansi ama kwa kuumbwa isemavyo dini.

Mtoa mada naungana naye kuwa yawezekana Mungu aliumba kiumbe kimoja tu chenyewe kikaendeleza kazi iliyosalia

Yaani ni kama vile tunavyoendelea kuzaana leo, tukiamu kuacha kuzaana tutaisha wote
Exactly, Kama ni uumbaji, basi ulifanyika kwa mageuzi toka kiumbe cha seli moja majini hadi kufikia binadamu wa nchi kavu, lakini sio kama kwa magic wand kwamba paaaap, binadamu huyo akatokea kwenye udongo, no way!
 
Mambo kadhaa ukikutana na elimu usiyoijua jifunze kwani kujifunza sio kosa, kosa ni kulifanyia kazi jambo lenye kuleta karaha na huzuni kwa wengine.

Ishi kwa furaha tu mengine yatajileta. Ukijawa na furaha ni rahisi kufundisha kufundishwa na kufundishika.
 
Maisha ya xhosa anayeishi mjini (Huyo mwenye kazi ya uigizaji ) na yule aliyebaki kijijini anawinda kwa kukimbiza katika tofauti ya miaka 200 hawawezi kuwa Sawa

Ngoja niishie hapo
Evolution hai operates kwenye scale ya miaka 200
Mwanadamu wa miaka 1000 iliyopita na Mwanadamu wa sasa hivi ni sawa kabisa

Evolution inachua Mamillion ya miaka.....
 
Evolution hai operates kwenye scale ya miaka 200
Mwanadamu wa miaka 1000 iliyopita na Mwanadamu wa sasa hivi ni sawa kabisa

Evolution inachua Mamillion ya miaka.....
Hata miaka 100 unaweza ukaanza kuona dalili mkuu

Ukichukulia mfano wa tembo ndani ya vizazi viwili/3 mabadiliko yameanza kuonekana. Inawezekana kabisa mkuu
 
Vestiges ni viungo katika miili ya wanyama ambavyo vinaweza visiwe na kazi katika baadhi ya wanyama lakini vinakuwa na muhimu na ni vya lazima katika miili ya wanyama wengine.

Mfano 'tail bone' / mfupa wa mkia hauna umuhimu wowote katika mwili wa binadamu maana hatuna mikia sisi, lakini tunao mfupa huo; mfupa huo ni lazima na ni muhimu sana kwa wanyama wenye mikia kama ngedere nk. Hii inashiria kwamba hapo awali binadamu tulikuwa ni kiumbe tofauti kabisa kilichokuwa na mkia ila kwa sasa kiungo hicho kimepotea sababu matumizi yake hayapo tena. (If you don't use it, loose it), hii ndio principle inayotumika katika evolution.

Vestiges zipo nyingi sana katika animal kingdom, mfano nyangumi ana mifupa ya miguu iliyojificha ndani japo hana miguu,hii inashiria kwamba hapo awali alikuwa ni mnyama wa ardhini aliyetembea, na tena bado anazaa na kunyonyesha kama wanyama wengine wa ardhini na sio kutaga mayai kama wafanyavyo samaki.
Vestiges ni nyingi sana, tusaidiane kuziorodhesha na kuzichambua vilivyo na kwa undani kabisa.

Sasa binadamu mwenye akili timamu anaweza weza vipi kuamini kwamba binadamu aliumbwa kama alivyo leo hii na mwonekano wake huu wa sasa, yaani hakubadilika kutoka aina moja ya muonekano hadi kufikia huu muonekano wa sasa. Huwa mnatumia mbinu gani kujitoa akili kwa kiwango hicho?! Mbona mi nashindwa kabisa??!!!

=============================
Mfano mwingine ni kifuko cha appendix kwenye utumbo wa binadamu, kwetu hakina kazi lakini kwa wanyama wanaokula mimea huwa wanakihitaji sana hicho kifuko na kinakuwa ni kikubwa sana kwao na huwasaidia kwenye kusaga chakula, hii inaashiria kwamba tulikuwa mnyama mmoja ila kila mmoja akabadilika kulingana na mazingira yake..
=============================

Mfano mwingine ni 'vitendea kazi' vya uzazi kwa mijusi wanaozaa kwa kuji-clone, yaani hawa mijusi huwa wanataga yai ambalo ni clone yao wenyewe na hivyo hawaitaji kujaamiiana ili kuzaa. Sasa kwakuwa bado wana hivi viungo ambavyo vimebaki huwa wanavitumia kama kujiburudisha tu, lakini havina kazi kwa sasa,japo hapo nyuma vilijuwa na kazi.
=============================

=================================
Update: 27/08/2021
Mifupa ya nyangumi mwenye miguu ‘dating millions of years ago’ yapatikana.

View attachment 1912340
_______________________________
Ur still a learner
 
Nimekujibu pia evolution theory sio lazima mbona huelewi? Sio law ni theory ambayo inachagua kutokana na nature ya kila kiumbe. Sio kama gravity kwamba kikienda juu lazima kurudi Chini

Inawezekana sina taarifa za kutosha wewe sema kwanini habadiliki? Ninachangia kwa jinsi ninavyofahamu mkuu kwa jinsi nilivyosoma na ninayoyaona field (Geo ) ila haimanishi mimi najua kila kitu
Evolution ni Fact,

Mababu zetu walikua ni wabunifu, walikua na uwezo wa kubuni vitu kama kuchonga vinyago, kutengeneza silaha za jadi n.k

Kwahio walipojiuliza swali la "viumbe vimefika vipi duniani? "

Wali 'generalize' uzoefu wao kwa kusema vilibuniwa na mwingine mwenye utashi kuliko wao,

Ni 'honest mistake' walikua sahihi kiasi chao mpaka pale sayansi ilipokuja na jibu bora zaidi

Darwin alikuja na jibu zuri zaidi kiasi kwamba contemporaries wake walijiona wajinga kwa nini hawakuwahi waza hivyo kabla wakati 'jibu'lilikua wazi mno..

Darwin hakua Atheist, alikua ni mkristo so hakukua na bias katika utafiti wake

Kuelewa evolution, Carl sagan aliwahi kutumia mfano wa 'kaa' 🦀 (crab) wa japan

Huko japani, kuna kaa ambao magamba yao yana sura ya mashujaa wa zamani wa japan waliokua wanajulikana kama Samurai,
Ukitazama unaona kabisa picha ya shujaa wa kisamurai kama walivyokua wanaonekana, kwenye magamba ya hao kaa

Sasa hivi ndivyo evolution inayofanya kazi kwa namna simple ila ya kushangaza mpaka kuunda kitu 'complex' kama hiyo taswira ya samurai kwenye Magamba ya kaa bila utashi wowote ule...

Kulikua na vita kati ya makabila mawali ya kijapani, miaka kama 1000 iliyopita

Baada ya vita, kabila lililokua linatawala kwa wakati ule lilizidiwa nguvu na kuangushwa na kabila jingine...mfalme wa wakati ule alikua ni mtoto mdogo wa miaka 7 wa kabila lililozidiwa

Kuona vile, bibi yake akamchukua, pamoja na Samurai wengine waliobakia na kuamua kujiua kwa kujitosa baharini

Wachache walio salia walikua ni vijakazi wasichana ambao baadae waliishia kuolewa na kuzaa na wavuvi walio kua fukwe ile yalipotokea hayo mauaji

Katika kuenzi na kuukumbuka ufalme ulioanguka, wale wavuvi ambao sasa wameshazaa na hawa wasichana wakawa wanahakikisha kaa yoyote yule atakaye kua na magamba yenye 'pattern' zinazo resemble 'sura' ya binadam wasiuawe bali warudishwe baharini

Kumbuka ubongo wa binadam upo vizuri sana kwenye kutambua pattern/alama na kutengeneza maana kutokea kwenye ile alama

Ndio maana unaweza hisi kuna sura ya mtu mwezini japo kiuhalisia hakuna chochote zaidi ya ubongo wako tu

So kitendo hiki kikasababisha kaa waliokua na magamba yenye alama zinazo fanana na sura ya binadamu wazaliane kwa wengine kuliko wale wasiokua nayo, kwa sababu kaa wasiokua na alama za namna hio walivuliwa na kuliwa, so chance ya kuzaliana kwao ilikua ni ndogo uki linganisha na wengine..

Kadri miaka ilivyozidi kwenda, ikawa sasa kaa waliokua na alama ambazo kwa kiasi fulani hao wavuvi waliitafsiri kama sura ya samurai aliyekasirika hawakuvulia uki compare na hawa wengine

Hii ikafanya kaa waliokua na magamba yanayofanana na sura ya samurai waliokasirika wazaliane kwa wingi kuliko wengine

Hiki kitendo cha kubagua kaa kulingana na sifa au traits zao, kinaitwa Artificial selection

Na walifanya hivi cause walikua na imani mizimu ya wale samurai waliojitosa baharini ilikua inaishi ndani ya hao kaa... Imani hii ikafanya bongo zao zianze kuona sura ya mtu kwenye magamba ya kaa,mpaka pale walipoanza kuona sura ya samurai

Ilitokea tu kwa bahati, magamba ya baadhi ya kaa yakawa na alama ambayo kwa wavuvi ili fanana na sura ya mtu, kama unavyoweza ona sura ya mtu kwenye mwezi au 'emoji' hii tunaita 'mutation' yaani mabadiliko yasiotabirika au kuwa na maana yoyote

Then haya mabadiliko yanapotezwa au kutunzwa kupitia artificial selection

Mwisho tunakua na kaa wenye sura ya samurai kabisa japo kuwa hakuna aliyechora ile sura kwenye magamba yao

So organic evolution inafanya kazi hivi hivi, tofauti yake ni kwamba badala ya kuwa na Artificial selection ambayo ipo 'biased'( wavuvi walikua wanapendezwa zaidi na kaa wenye alama inayounda sura ya mtu au ya samurai)
Yenyewe ina natural selection,yaani hizo 'mutations ' zinapotezwa au kutunzwa kulingana na jinsi gani zinamsaidia huyo kiumbe kuishi kwenye mazingira yake

Kama alama zinazofanana na sura ya samurai zilivyo saidia baadhi ya kaa ku survive

Na mabadiliko yenye faida ni nadra sana kutokea inaweza chukua mamilion ya miaka kupata mutation yenye faidi kulingana na mazingira husika

Kuamini kuwa viumbe vimebuniwa na mwenye utashi kuliko sisi ni sawa na kuona sura ya mtu mwezini japo kuwa hakuna sura yoyote ile

Ubongo wetu umekua hardwired kutafuta maana kwenye pattern hata kama haipo
Na hii 'useful mutation' ndiyo iliyofanya mababu zetu wa survive mamilion ya miaka mpaka leo
Plus kuamini tumeumbwa, hakujibu swali lolote?
Kama tunataka kujua asili ya maisha, kudai maisha yameumbwa na mwingine bado hakukati kiu yetu ya kutaka kujua asili ya maisha

Je asili ya maisha ya huyu mwenye utashi kuliko sisi yametoka wapi?

Je kama maisha yake hayana chanzo chochote je kwanini tusi 'save'step na kusema basi hata maisha ya hapa duniani hayana chanzo chochote?
 
Hata miaka 100 unaweza ukaanza kuona dalili mkuu

Ukichukulia mfano wa tembo ndani ya vizazi viwili/3 mabadiliko yameanza kuonekana. Inawezekana kabisa mkuu
Kuna artificial selection ambayo inafanywa na binadamu ndiyo inaweza chukua mda mfupi kama huo lakini sio natural selection
 
Probably Mungu aliumba kiumbe cha kwanza ambacho kilikuwa single celled na kika-evolve na kubranch out kuwa viumbe vyote tunavyovijua leo.

Pia mabadiliko ya kiwango cha vinasaba huweza kuchukua mamiliini ya miaka, kwahiyo usitegemee kuona sokwe akibadilika ndani ya uhai wako, wanaweza kuja kuwa the next super species na wao wakatuona sisi ndio kama manyani..
Kwan umejua vip hao manyan Sasa iv hawakudharau
 
Back
Top Bottom