Nimekujibu pia evolution theory sio lazima mbona huelewi? Sio law ni theory ambayo inachagua kutokana na nature ya kila kiumbe. Sio kama gravity kwamba kikienda juu lazima kurudi Chini
Inawezekana sina taarifa za kutosha wewe sema kwanini habadiliki? Ninachangia kwa jinsi ninavyofahamu mkuu kwa jinsi nilivyosoma na ninayoyaona field (Geo ) ila haimanishi mimi najua kila kitu
Evolution ni Fact,
Mababu zetu walikua ni wabunifu, walikua na uwezo wa kubuni vitu kama kuchonga vinyago, kutengeneza silaha za jadi n.k
Kwahio walipojiuliza swali la "viumbe vimefika vipi duniani? "
Wali 'generalize' uzoefu wao kwa kusema vilibuniwa na mwingine mwenye utashi kuliko wao,
Ni 'honest mistake' walikua sahihi kiasi chao mpaka pale sayansi ilipokuja na jibu bora zaidi
Darwin alikuja na jibu zuri zaidi kiasi kwamba contemporaries wake walijiona wajinga kwa nini hawakuwahi waza hivyo kabla wakati 'jibu'lilikua wazi mno..
Darwin hakua Atheist, alikua ni mkristo so hakukua na bias katika utafiti wake
Kuelewa evolution, Carl sagan aliwahi kutumia mfano wa 'kaa' 🦀 (crab) wa japan
Huko japani, kuna kaa ambao magamba yao yana sura ya mashujaa wa zamani wa japan waliokua wanajulikana kama Samurai,
Ukitazama unaona kabisa picha ya shujaa wa kisamurai kama walivyokua wanaonekana, kwenye magamba ya hao kaa
Sasa hivi ndivyo evolution inayofanya kazi kwa namna simple ila ya kushangaza mpaka kuunda kitu 'complex' kama hiyo taswira ya samurai kwenye Magamba ya kaa bila utashi wowote ule...
Kulikua na vita kati ya makabila mawali ya kijapani, miaka kama 1000 iliyopita
Baada ya vita, kabila lililokua linatawala kwa wakati ule lilizidiwa nguvu na kuangushwa na kabila jingine...mfalme wa wakati ule alikua ni mtoto mdogo wa miaka 7 wa kabila lililozidiwa
Kuona vile, bibi yake akamchukua, pamoja na Samurai wengine waliobakia na kuamua kujiua kwa kujitosa baharini
Wachache walio salia walikua ni vijakazi wasichana ambao baadae waliishia kuolewa na kuzaa na wavuvi walio kua fukwe ile yalipotokea hayo mauaji
Katika kuenzi na kuukumbuka ufalme ulioanguka, wale wavuvi ambao sasa wameshazaa na hawa wasichana wakawa wanahakikisha kaa yoyote yule atakaye kua na magamba yenye 'pattern' zinazo resemble 'sura' ya binadam wasiuawe bali warudishwe baharini
Kumbuka ubongo wa binadam upo vizuri sana kwenye kutambua pattern/alama na kutengeneza maana kutokea kwenye ile alama
Ndio maana unaweza hisi kuna sura ya mtu mwezini japo kiuhalisia hakuna chochote zaidi ya ubongo wako tu
So kitendo hiki kikasababisha kaa waliokua na magamba yenye alama zinazo fanana na sura ya binadamu wazaliane kwa wengine kuliko wale wasiokua nayo, kwa sababu kaa wasiokua na alama za namna hio walivuliwa na kuliwa, so chance ya kuzaliana kwao ilikua ni ndogo uki linganisha na wengine..
Kadri miaka ilivyozidi kwenda, ikawa sasa kaa waliokua na alama ambazo kwa kiasi fulani hao wavuvi waliitafsiri kama sura ya samurai aliyekasirika hawakuvulia uki compare na hawa wengine
Hii ikafanya kaa waliokua na magamba yanayofanana na sura ya samurai waliokasirika wazaliane kwa wingi kuliko wengine
Hiki kitendo cha kubagua kaa kulingana na sifa au traits zao, kinaitwa Artificial selection
Na walifanya hivi cause walikua na imani mizimu ya wale samurai waliojitosa baharini ilikua inaishi ndani ya hao kaa... Imani hii ikafanya bongo zao zianze kuona sura ya mtu kwenye magamba ya kaa,mpaka pale walipoanza kuona sura ya samurai
Ilitokea tu kwa bahati, magamba ya baadhi ya kaa yakawa na alama ambayo kwa wavuvi ili fanana na sura ya mtu, kama unavyoweza ona sura ya mtu kwenye mwezi au 'emoji' hii tunaita 'mutation' yaani mabadiliko yasiotabirika au kuwa na maana yoyote
Then haya mabadiliko yanapotezwa au kutunzwa kupitia artificial selection
Mwisho tunakua na kaa wenye sura ya samurai kabisa japo kuwa hakuna aliyechora ile sura kwenye magamba yao
So organic evolution inafanya kazi hivi hivi, tofauti yake ni kwamba badala ya kuwa na Artificial selection ambayo ipo 'biased'( wavuvi walikua wanapendezwa zaidi na kaa wenye alama inayounda sura ya mtu au ya samurai)
Yenyewe ina natural selection,yaani hizo 'mutations ' zinapotezwa au kutunzwa kulingana na jinsi gani zinamsaidia huyo kiumbe kuishi kwenye mazingira yake
Kama alama zinazofanana na sura ya samurai zilivyo saidia baadhi ya kaa ku survive
Na mabadiliko yenye faida ni nadra sana kutokea inaweza chukua mamilion ya miaka kupata mutation yenye faidi kulingana na mazingira husika
Kuamini kuwa viumbe vimebuniwa na mwenye utashi kuliko sisi ni sawa na kuona sura ya mtu mwezini japo kuwa hakuna sura yoyote ile
Ubongo wetu umekua hardwired kutafuta maana kwenye pattern hata kama haipo
Na hii 'useful mutation' ndiyo iliyofanya mababu zetu wa survive mamilion ya miaka mpaka leo
Plus kuamini tumeumbwa, hakujibu swali lolote?
Kama tunataka kujua asili ya maisha, kudai maisha yameumbwa na mwingine bado hakukati kiu yetu ya kutaka kujua asili ya maisha
Je asili ya maisha ya huyu mwenye utashi kuliko sisi yametoka wapi?
Je kama maisha yake hayana chanzo chochote je kwanini tusi 'save'step na kusema basi hata maisha ya hapa duniani hayana chanzo chochote?