Amna kina chomsumbua mama anaona haheshimiki kwasabab ya jinsia yake, anaona mbna wakati wa mtanguliz wake wana CCM wengi waliogopa hata kuonesha makundi yakuukwa uraisi muda ukiwa bado.. Mama kazi kubwa aliyonayo kama ata taka afanye kazi kwa raha bila kuhujumiwa atafute safu yake mpya kwanzia kwene baraza la mawaziri, lasi hivyo ata endelea kupata wenge
Sidhani kama mama aheshimiki kwa sababu ya jinsia. Ni maneno tu! Na si kweli kwamba wakati wa Magufuli watu waliogopa kuonesha Makundi. Kama utakumbuka kuna hotuba Magufuli alitoa na kuwaonya mawaziri wake kuwa wafanye kazi na si kuuwaaza urais. Ilifikia sehemu, hadi akadai Rais ajaye atakuwa kijana hivyo, Profesa Kabudi asahau Urais, Lukuvi nae asahau.
Hivyo makundi yalishaanza tengenezwa. Alimuonya hadi waziri Mkuu akadai akicheza hawezi kumaliza mika kumi akiwa waziri mkuu.
Shida hapa ni kwamba mama kapata Urais wakati watu walishakuwa na plan za kugombea baada ya Magufuli. Ghafla Mungu nae akatenda tofauti.
Watu kujiandaa na Urais ilianza kipindi cha Mkapa. Wakati huo Kikwete na kundi lake akina Lowasa walikuwa wakijiandaa ndo Nyerere akapendekeza Mkapa. Hata hivyo Kikwete na kundi lake waliendelea kujiimarisha wakati wa Mkapa alipokuwa Rais. Walipanga mbinu nyingi wakiwepo na akina Samweli Sitta.
Baada ya Kikwete kuwa Rais, Lowasa akaanza kasi ya nguvu akiwa waziri Mkuu, hadi kumzushia Kikwete kuwa hato maliza miaka kumi kutokana na afya yake. Baadae mambo yakabadilika, Lowasa alikuwa na jopo kubwa likimshangilia. Mpaka kwenye Mkutano wa NEC watu wanaimba mbele ya Rais na Mwenyekiti wa Chama kuwa wanaimani na Lowasa. Hii ilikuwa dharau kubwa. Ila Kikwete alikuwa mtoto wa mjini anajua kupambana bila hasira. Anammaliza adui huku akicheka.
Shida hapa mama anakuwa muoga kupingwa, sidhani kama ni dhambi mtu kutaka Urais. Hata wakati wa Nyerere kuna mtu aliitwa Mnasa, huyu alikuwa mjumbe wa NEC na alimweleza Nyerere wazi bila kuogopa kuwa nae atagombea urais. Alipinga Nyerere kupita bila kupingwa. Na mara nyingi alimkosoa Nyerere wazi wazi. Hakuwahi kufukuzwa uNEC au uanachama.
Sioni Kosa la Ndugai, ana haki ya kukosoa na wala hajavunja katiba. Tena yeye hayupo katika baraza la mawaziri, hivyo hafungwi na makubaliano ya pamoja. Akiwa kama kiongozi wa Muhimili wa Bunge. Ana haki ya kuikosoa serikali, na kuisimamia. Watu tunaushabiki tu. Kwa mtindo huu hakuna haja ya Separation of Powers. Kwani inaonesha leo Mbunge au Spika akiwa tofauti na Rais anapingwa.
Rais asiwe muoga kupingwa. Haya mambo ni yakawaida uwezi kupendwa na kila mtu. Nyerere alipingwa, Mwinyi alipingwa, Mkapa akapingwa, Kikwete akapingwa tena na Rafiki wa Karibu. Magufuli huyu kapingwa saaana tu na kusemwa sana tu. Hivyo ni vitu vya kawaida. Kikubwa atekeleze tu Ilani ya Chama. Huu si wakati wa zidumu Fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM.
Watanzania tunapenda tu ushabiki, na tuna gubu, na kuweka visasi moyoni. Hatusimamii ukweli. Rais ni nani asikosolewe! Muda wote anatetea mikopopo. Utasikia hata Marekani na Japan wanakopa. Utasikia Tanzania ilianza kukopa toka zamani. Kwanini tusiwe na Rais alie na maono tofauti. Tunahitaji mtu mwenye vision mpya si yule aneishi kwa mazoea. Ati kwakuwa huko nyuma walikopa basi tuendelee kukopa tujenge vyoo na madarasa. Ati kwakua Marekani au nchi tajiri zinakopa basi nasi tuendelee kukopa. Wananchi wanamshangilia na wabunge.
Hatuna viongozi wenye maono kabisa. Yaani unakopa ili ulipe deni. Ukikosolewa unakasirika, na unaanza mashambulizi kwa Muhimili. Sioni muelekeo wa Tanzania. Naiona Tanzania inayoongozwa kwa mazoea. Tusahau maendeleo na kupiga hatua.