Viatu na Kivuli cha Magufuli kwa Tanzania ya Samia - Kuna cha Kuhofia?

Viatu na Kivuli cha Magufuli kwa Tanzania ya Samia - Kuna cha Kuhofia?

Mimi namshauri Rais awe firm kwenye maamuzi kuhusiana na maswala mbali mbali ya kitaifa.

Kwakua yeye ndiye mwenye taarifa nyingi na sahihi kuliko wengine atumie resources zote kuhakikisha kuwa kila decision is for the best interest of the country.

Simshauri afanye mambo kwa kufurahisha kundi lolote,

Only for the best interest of our Nation.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Na. M. M. Mwanakijiji
(Makala hii imetoka kwenye gazeti la Raia Mwema, Jumatano Machi 31, 2021. Picha juu kutoka kwa Michuzi Blog).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ana kibarua kigumu. Anakabiliwa na kuridhisha pande nyingi kiasi kwamba upande wowote ambao hatouridhisha au hatoonekana kuuridhisha hautachelewa kumpinga na upande ambao utaonekana unapendelewa utachukiwa na ule upande mwingine. Kama kuna mtu anadhania kuwa Rais Samia atafanya Watanzania wote tushikane mikono na kuanza kuimba kwa pamoja “Ukuti Ukuti” kana kwamba hatuna tofauti za msingi mtu huyo anajidanganya. Tofauti na mtangulizi wake Rais Samia anaingia akiwa anakabiliwa na changamoto ambazo hakuna Rais mwingine yeyote wa Tanzania amewahi kuzipata. Ni katika hili hekima, ujasiri, ubunifu, na uthubutu wake utaenda kupimwa na labda ataangaliwa kwa macho makali zaidi kuliko Rais mwingine yeyote.

Viatu vya Magufuli
Upande wa kwanza anakabiliwa kujaribu kuvivaa viatu vya kiungozi vya Magufuli. Mtu anapojaribu kuvaa viatu vya mtu mwingine anakabiliwa na changamoto; ama vitamtosha, vitambana, au vitampwaya. Kama vitamtosha bado ataangaliwa kama vimemkaa; vinaendana naye au la; kama vitambana swali ni kwa kiasi gani au vipanue au atafute vingine; na kama vitampwaya ni je anahitaji kuongeza nini ili vimtoshe au bado atahitaji kutafuta vile vinavyomtosha tu hadi atakapokuja mwingine ambaye viatu hivyo vitamtosha.

Rais Samia atahukumiwa kwanza kwa kabisa ni kwa kiasi gani ataenda kusimamia miradi mikubwa “ya kimkakati” iliyoanzishwa chini ya Rais Magufuli. Ni kwa kiasi gani mradi wa SGR (treni ya umeme) utaenda kukamilika na kusimamiwa; mradi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere, na kuhamia Dodoma. Hii ni baadhi tu ya miradi hiyo. Uzuri ni kuwa kwa vile alikuwa ndani ya serikali hii toka mwanzo mama Samia inawezekana ni mtu pekee anayeilewa na kujua ni kwa kiasi gani inahitajika na hivyo kwake inaweza isiwe ngumu kabisa kufuatilia miradi hii mikubwa, ile ya kati na midogo.

Kama tulivyoshuhudia suala la ubadhirifu, ufisadi na kutokuridhika na utendaji kazi aliouonesha siku ya Jumapili akipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali; Rais Samia atahukumiwa pia ni kwa jinsi gani hatoacha uzembe, kubebana na kupeana “second chances” kutaendelea. Hii ina maana hatoacha wateuliwa wa Rais Magufuli ambao wanapwaya sasa hivi na labda walishaonekana wanapwaya. Je, atatakiwa asubiri hadi arudi ofisini kabla ya kuchukua hatua au atachukua hatua pale pale kwa staili ya Magufuli ya “kutumbua”. Je, tumbua yake itakuwa ni ile ya kupisha uchunguzi ili mtu achunguzwe kabla ya kumfuta mtu kazi papo kwa papo kama alivyokuwa akifanya Magufuli?

Ataangaliwa kwa jinsi gani analiongoza taifa kuelekea kujitegemea kuliko kurudi kwenye kutegemea. Je, katika hili atatumia lugha tofauti kuliko ile ya Magufuli? Je, katika kujitegemea atajaribu kulitenga taifa na dunia au atajaribu kuliweka taifa katika nafasi yake sahihi ya kushirikiana na dunia. Kwamba, kama Magufuli hatolirudisha taifa katika aibu ya kuombaomba hata kwa vitu visivyoombeka? Je, ataanza safari za kwenda duniani kujitambulisha na kuomba misaada tena? Au ataangalia kimkakati ni wapi Watanzania bado tunaweza? Na katika hili tena alikuwa chini ya mwalimu mzuri. Rais Samia aliona na kuielewa kiu ya Rais Magufuli ya kuona Watanzania wanajiamini na kuwa hawajioni wanyonge; na jinsi gani aliwahusisha Watanzania katika kutekeleza mambo mbalimbali bila kusubiri vibali vya wakubwa wa dunia.

Ni kwa sababu hiyo wapo watakaoangalia na kuona kama amevivaa viatu vya Magufuli au vimemvaa yeye; ama ameingia na viatu vyake na vikapendeza zaidi kuliko vile vya Magufuli. Akaamua kupita alikopita Magufuli lakini kwa hatua zake na kwa mwendo wake. Inawezekana akawa ametengenezewa njia nzuri zaidi ya kupita na Magufuli na yeye akaipita kwa urahisi zaidi kuliko kama mtangulizi wake asingekuwa Magufuli.

Kivuli cha Magufuli
Lakini Rais Samia pia anauamuzi wa kwake mwenyewe. Japo ameingia kuziba pengo la Magufuli na chini ya mwaka mmoja tu wa ngwe yao ya pili kwa kweli si lazima afuate kila alichofanya Magufuli. Si lazima azungumze alivyozungumza Magufuli, si lazima aoneshe ukali kama Magufuli au afanye maamuzi kama alivyofanya Magufuli. Kwa hakika kabisa japo kinadharia hapaswi kwenda nje ya Ilani na ajenda yao na Magufuli lakini pia hafungwi kuanzisha ya kwake na hata kufutilia mbali ajenda ya Magufuli. Lakini vyovyote atakavyoamua kufanya kivuli cha Magufuli kitaendelea kumfunika.

Kundoka kwa Magufuli na kumwachia Samia kunamfanya Samia aingie akiwa na jukumu kubwa la kuonesha siyo tu alikuwa Makamu lakini alikuwa Makamu aliyeweza kuwa Rais kama historia inaita hivyo. Kumuondoa Ronaldo uwanjani kunatoa nafasi kwa mchezaji wa akiba kuonesha kama anastahili kuchukua nafasi ya mchezaji huo nyota. Lakini uchezaji wote utapimwa na kuona kama anaweza kutoa mchango wa kuisaidia timu kushinda. Mama Samia anaingia kuchukua nafasi ya mchezaji nyota; ni jinsi gani ataifungia magoli timu yake na kuisadia kushinda na hivyo kujihakikishia namba ni suala la muda.

Lakini la muhimu ni kuwa si lazima afanye kazi akiwa na kivuli cha Magufuli mgongoni. Japo, anaenda kuibeba ajenda ya Magufuli si lazima aibebe mabegani kama Magu kama ana uwezo wa kuibeba kichwani. Kivuli cha Magufuli kisiwe kizuizi bali kiwe ni daraja la kuvukia kwenda anakotaka kuipeleka Tanzania. NI kwa sababu hiyo asiogope, asifikirie mara mbilimbili, au hata kujishuku endapo ataamua kufanya mabadiliko ya lazima ambayo labda Magufuli asingeyafanya. Kipimo chake sasa siyo Magufuli tena bali ni yeye mwenyewe kama Rais. Kauli yake msibani kuwa aliyesimama pale ni “Rais” itume ujumbe kwa yeyote mwenye shaka na shuku; kwamba siyo tu yeye ni Rais bali pia madaraka aliyokuwa nayo Magufuli ndiyo aliyonayo yeye leo; uwezo aliokuwa nao Magufuli aliopewa na Katiba ndio uwezo ule ule aliopewa yeye. Yeye sasa anatakiwa kutengeneza kivuli chake mwenyewe na akifanya vizuri basi atajitengenezea haki na nafasi ya kutengeneza ajenda yake ya 2025 akitaka kugombea tena.

Tanzania ya Samia
Ni wazi basi kuwa Watanzania wanapompokea Rais wao mpya wapo wenye matarajio mengi na yenye kutofautiana. Wapo ambao wanatarajia kuwa anaingia na kuwa kama Rais kutoka upinzani ambaye atafutilia mbali jina, historia, mafanikio, na maamuzi yote ya Magufuli na hivyo kutengeneza historia (legacy) yake mwenyewe nje ya Magufuli. Kwamba, akijiweka mbali na Magufuli na ajenda yao basi atakubalika zaidi na wapinzani na wakosoaji wa Magufuli. Kwamba, atake kupendwa na wale waliomchukia Magufuli.

Lakini pia anaweza akajikuta anajitahidi sana kuwa kama Magufuli na kujikuta anatengeneza maadui na wakosoaji wengi zaidi kuliko aliokuwa nao Magufuli na hivyo kuoneakana ni Magufuli 2.0. Changamoto kubwa ya Tanzania hii ya Samia ni kutafuta mizania kati ya alikotoka na Magufuli na anakotaka kwenda bila Magufuli. Je, itakuwa ni Tanzania ya namna gani? Je, watu wake watasimama vipi? Je, atatengeneza taasisi na kuinua watu kwa namna gani? Je, anatamani iwe Tanzania ya namna gani. Swali hili naamini litajibiwa siku si nyingi pale atakaposimama kulihutubia taifa na kutoa mwelekeo wa maono yake kwa taifa na tutaona atakavyoanza kuipanga serikali yake ili kutimiza maono hayo.

Kwa sasa ni wazi kuwa Watanzania bado wamegawanyika na wanasubiria kuona kama mgawanyiko wao utaendelea kuwa ni wa kudumu au utawasogeza karibu karibu au utapanua zaidi mgawanyiko huo. Kwa kweli, siwezi kumuonea wivu katika kibarua hiki. Ninachomtakia ni kila la kheri katika kuliongoza taifa letu na kuwa vyovyote atakavyokuwa historia itaweza kumhukumu si kwa jinsi gani alivyokuwa kama Magufuli au kwa jinsi gani alivyokuwa tofauti na Magufuli; atahukumiwa kwa jinsi gani aliliongoza taifa letu kuelekea mafanikio ya kweli, ubora wa maisha, kuinuliwa kwa tunu zetu mbalimbali za kitaifa kiasi kwamba ije kusemwa Tanzania ya Samia ilikuwa ni Tanzania tuliyoitarajia.

Na ili kuifikia Tanzania hiyo ni lazima tukatae mbinu, majaribio au hata jitihada zozote za kumshusha Rais Samia, kumdhoofisha au kumtendea kana kwamba si Rais “kamili” kwa sababu tu ni mwanamke. Tukatae tena kwa ukali wote unaostahili lugha zote za kinyanyasaji kijinsia ambazo nyingine zimeenea mitandaoni. Tuwakatae wale wote wanaozungumza kana kwamba wanamuunga mkono lakini wanafanya hivyo ati kwa sababu “ni mama” kana kwamba umama wake ni kitu cha kumdhoofisha.

Tujue kuwa anaingia madarakani akiwa na nguvu zote kama Rais wa Tanzania bila kujali jinsia yake. Lakini pia inatupa nafasi ya kuwa na kiongozi ambaye ana mtazamo tofauti kuliko wengine na hivyo labda ataweza kuwainua pia wanawake wengi wenye uwezo ambao labda hawakupata nafasi zozote za juu za uongozi kwa sababu ya mitazamo mibaya ya kijinsia (gender biases).

Lakini pia naamini atawapa nuru mabinti zetu kutamani kufikia nafasi yoyote ya uongozi wa nchi yetu na kuwa wale wote wenye nafasi za uongozi wafanye hivyo kwa weledi mkubwa zaidi bila kuonekana wanajikomba kwa mwanamme yeyote. Na kama nitakavyoonesha wiki ijayo kuna mambo ambayo naamini Rais Samia ni LAZIMA ayafanye tofauti na Magufuli.

Katika Tanzania ya Samia hakuna cha kuhofia.

Niandikie: klhnews@gmail.com
Mshaanza Kujipendekeza kwa Mama Samia? Sio ninyi mlijaribu kutuhadaa kuwa hakuna mbadala wa Magufuli? Some of you guys mtaanza kuwa wakosoaji muda si mrefu kwa sababu baadhi yenu mlimpinga Jk kwa Uislamu wake na kumsapoti JPM Kwa Ukristo wake. Time will tell.
 
Mshaanza Kujipendekeza kwa Mama Samia? Sio ninyi mlijaribu kutuhadaa kuwa hakuna mbadala wa Magufuli? Some of you guys mtaanza kuwa wakosoaji muda si mrefu kwa sababu baadhi yenu mlimpinga Jk kwa Uislamu wake na kumsapoti JPM Kwa Ukristo wake. Time will tell.
Dereva wa TISS, wewe ulilipwa kumpigia kampeni Magufuli na unanyooshea watu vidole. You're so cheap yani wewe tapeli 🚮🚮🚮🚮🚮
 
Most are selfish and with high time preferences...Hawataki kuwekeza wanataka kula mbegu badala ya kuipanda izae...Kiuhalisia watumishi wengi output yao ni ndogo compared na salaries....Wamekosa ubunifu na wana dublicate activities ili tu waonekana wanajishughulisha hata kama hiyo shughuli haiongezi tija kwa taifa...
Pole Sana kwa msiba...
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Pole Sana kwa msiba...
Ahsante sana....For sure you understand better what it means to me amd what I have for my country....Lakini bado Mungu yu hai na yeye ndiye wakuabudiwa...Tumaini letu liko kwake na siyo kwa binadamu...Ninamwombea Mama Samia Rais wetu, kuendelea kusimama imara kama alivyo anza, Mungu aendelee kumtegemeza...
 
Watumishi wa umma tunamuangalia tu kama ataendeleza dhuluma ya mtangulizi wake au atatenda haki! Mwaka wa sita huu! Hakuna madaraja, hakuna annual incriment, hakuna nyongeza ya mishahara.

Zaidi tu tumeongezewa makato ya Bodi ya Mikopo na rentation fees. [emoji56]

Hii comment ni kama huwa unahamisja kwa kila thread[emoji3][emoji3]. Nakushauri ewe mtumishi wa Umma,jiongezee kipato kwa kufanya hata na ujasilia mali mdogo mdogo,unaonekana kama maisha yako kwa 100% unategemea “kupanda daraja” na “salary Increment” peke yake. [emoji3][emoji3]
 
Kila mtu ana viatu vyake and so be it.

Samia halazimika hata kidogo kuvaa viatu vya Magufuli.

Msitupotezee Dira.
Na Propaganda zenu.

Huyo Magufuli yeye ndo alikuwa na ubora upi kwamba yake ndo benchmark ya Urais?
Hebu vingine MUWE na Aibu jamani!
 
Mshaanza Kujipendekeza kwa Mama Samia? Sio ninyi mlijaribu kutuhadaa kuwa hakuna mbadala wa Magufuli? Some of you guys mtaanza kuwa wakosoaji muda si mrefu kwa sababu baadhi yenu mlimpinga Jk kwa Uislamu wake na kumsapoti JPM Kwa Ukristo wake. Time will tell.
Dah!

Yaani mtu akisema jambo zuri kuhusu mtu fulani ni anajipendekeza? Na ajipendekeze ili iweje sasa?

Na kumpinga JK kama hukuwa Muislamu basi ni ulimpinga kutokana na Uislamu wake?

Kwa watu waliomuunga mkono Magufuli ambaye makamu wake alikuwa ni Samia, sasa hivi wakimuunga Samia, nini cha ajabu?

Hao wote wawili si walikuwa ni timu moja au?

Watu kama wewe huwa mna project mlivyo kupitia watu wengine!

Yawezekana hivyo wewe ndivyo ulivyo....
 
Sure wana ubinafsi sana. Everyone deserve same and equal opportunities
Kwa kuuza mitumba ulipwe mshahara?
Omba mazingira rafiki kwako, kama wewe uko kimya unataka wao wakusemee? Acha huo utoto.
 
Huyu na Dr Slaa soon watajiunga tena opposition....aibu hawana..
Alipopigwa risasi Tundu Lissu hakuandika chochote kama kapigwa risasi panya

Tumeshawajua wanakosoa kwasababu nyuma pazia wanakuwa na ajenda fulani either udini ama ukabila au ukanda.
 
Dah!

Yaani mtu akisema jambo zuri kuhusu mtu fulani ni anajipendekeza? Na ajipendekeze ili iweje sasa?

Na kumpinga JK kama hukuwa Muislamu basi ni ulimpinga kutokana na Uislamu wake?

Kwa watu waliomuunga mkono Magufuli ambaye makamu wake alikuwa ni Samia, sasa hivi wakimuunga Samia, nini cha ajabu?

Hao wote wawili si walikuwa ni timu moja au?

Watu kama wewe huwa mna project mlivyo kupitia watu wengine!

Yawezekana hivyo wewe ndivyo ulivyo....

Mama si bhaghosha
 
Ahsante sana....For sure you understand better what it means to me amd what I have for my country....Lakini bado Mungu yu hai na yeye ndiye wakuabudiwa...Tumaini letu liko kwake na siyo kwa binadamu...Ninamwombea Mama Samia Rais wetu, kuendelea kusimama imara kama alivyo anza, Mungu aendelee kumtegemeza...
Mungu ataendelea kukusimamia na kulisimamia taifa letu. Mama Samia atatenda makubwa kuliko watu wanavyofikiria kwani anajua taifa linategemea nini kutoka kwake. Heri ya Pasaka.
 
Hili la dini very soon litajitokeza..
Hawataweza jizuia..
Dah!

Yaani mtu akisema jambo zuri kuhusu mtu fulani ni anajipendekeza? Na ajipendekeze ili iweje sasa?

Na kumpinga JK kama hukuwa Muislamu basi ni ulimpinga kutokana na Uislamu wake?

Kwa watu waliomuunga mkono Magufuli ambaye makamu wake alikuwa ni Samia, sasa hivi wakimuunga Samia, nini cha ajabu?

Hao wote wawili si walikuwa ni timu moja au?

Watu kama wewe huwa mna project mlivyo kupitia watu wengine!

Yawezekana hivyo wewe ndivyo ulivyo....
Unajua haiingii akilini; wengine tulimpinga Mkapa na alikuwa Mkatoliki, tulimuunga mkono JK mwanzoni hadi makorokocho yalipoanza... najua wapo wakristu waliomuunga mkono Magufuli mwanzoni lakini baadaye wakaamua kuacha na kumpinga; sitoshangaa utakuta wapo Waislamu wanaomuunga mkono Samia na baadaye wakiona hailipi wataamua kumuacha. HIli la dini ni namna tu fulani ya watu kutaka kuzima mijadala ili wasipingwe; kwamba ukiwapinga tu wanasema ni "dini".
 
Mwacheni Rais Samia aongoze kwa maono yake na si vivuli au viatu vya wengine
Kumtaka afuate nyayo ni kumkwaza. Samia ana personality yake tofauti na ya mwendazake

Hawezi kutumia personality yake kufanya ya Marehemu, JK, Hayati Mkapa, Mwinyi au Hayati Nyerere!
kila zama na kitabu chake , ni wakati wake kuandika zama hizi kwa kitabu chake

Katika mambo aliyoandika Mzee Mwanakijiji moja ni sisi kuwa Taifa lililogawanyika.
Kazi ngumu mbele ya mama Samia ni kuliunganisha Taifa lilivyovurugwa na Marehemu

Marehemu aliligawa Taifa kwa namna zozote unazofikiri, iwe jinsia, ukabila, udini , hata rangi

Marehemu hakujali Utu alijali Vitu, Mama Samia arudishe hadhi , heshima na utu wa mwananchi
Kiongozi anaongoza watu si madaraja au miti, hivyo kutojali uhai na maisha ya watu si kiatu cha kuvaa

Hivi mnataka Rais Samia avae viatu vya kukataa sayansi na kuhubiri madogori na mapambio kwa gharama kubwa sana za maelefu ya maisha ya wananchi! kiatu hicho mama asikijaribu wala kukifikiri!

Rais Samia halazimiki kufuta kila kilichoachwa na Marehemu lakini analazimika kufuta mabaya aliyoacha na yaliyoliacha Taifa hili na makovu makubwa sana.

Kiongozi hapimwi kwa Vitu bali Utu. Mwendazake anapimwa kwayo ndiyo maana kipimo cha utu wake kipo mgongoni kama si kushoto. Hukumu yake imesimama katika utu licha ya vitu alivyotengeneza

Mwacheni Rais Samia aongoze kwa zama zake na aandike legacy yake kwa maono yake

Mtazamo sahihi huu. Lakini inabidi tuwe makini zaidi. Hiyo sifa ya “kutengeneza VITU” nayo anapewa kirahisi sana. Kwanza, je, ni kweli kuwa awamu yake ndiyo imehusika na ujenzi wa miundombinu yote aliyojinasibu nayo? Halafu, pale alipohusika, yalikuwa ni maamuzi yanayozingatia vipaumbele vya taifa au utashi wake mwenyewe (at the expense of coordinated development plans)?

Uamuzi wa kuzima transparency kwenye miradi ya kimkakati unaashiria nini kuhusu ufanisi na ufisadi kwenye miradi hiyo? Nchi kweli imepata value for money hapo? Hizo sio pesa za mtu binafsi asifiwe kwa “kujenga madaraja, SGR, airports, JNHPP, kununua ndege kwa cash, n.k.” Ni muhimu ufanisi wa miradi hiyo uthibitishwe ndipo mtu apewe sifa. Hii ndio miradi yenye 10% kibao na sifa rahisi rahisi.
 
Huyu na Dr Slaa soon watajiunga tena opposition....aibu hawana..
Alipopigwa risasi Tundu Lissu hakuandika chochote kama kapigwa risasi panya
Boss unasema kwa sababu unajua sikuandika "chochote" au kwa sababu unaamini sikuandika"chochote"?
 
Nataka ninukuliwe vizuri kabisa ...legacy ya JPM ni ngumu kuivaa! Huko mbele atakumbukwa kuliko hata alivyozikwa! Tena wasiompenda sasa ndio wataoanza kukiri na kutubu! Naomba mtunze hii comment.
Absolutely, umeandika vyema kabisa, ni vigumu saaaanaaa kuona umuhimu JPM mapema hii, time will tell

NAITUNZA COMMENT YAKO!
 
Aprili 31, 2021?

Pole in advance....maana naona matusi na mapovu ya watu tayari 😄

Hana jipya huyu mzee mwenzetu,
Nachokiona ni anajiandaa kufanya zile kampeni zake za awamu ya JK. Maana anatambua kabisa hii nizamu ya # DiniYetu.

Kifupi apige kimyaa kama kipindi cha Maliyamungu muaji na mtekaji.
 
Back
Top Bottom