Viatu na Kivuli cha Magufuli kwa Tanzania ya Samia - Kuna cha Kuhofia?

Viatu na Kivuli cha Magufuli kwa Tanzania ya Samia - Kuna cha Kuhofia?

Kwake Mama Samia tunategemea hii miradi mikubwa iliyoanza haitaishia njiani. Nina imani naye kubwa sana na kusema ukweli yeye kama Rais ana hiari ya kuchukua namna nzuri ya kufanikisha bila kuiga nyayo za mtangulizi wake.
Lakini ili hii miradi iweze kuwa na tija, lazima tuanze kuboresha mahusiano mazuri ya majirani na wadau wengine wa maendeleo. Tufungue milango ya uwekezaji, hasa kwenye natural resources zetu. Itakuwa ngumu sana kukusanya mapato bila kuhakikisha wigo wa kupata hizo kodi unaongezwa.
Kusema kweli sasa ndio wakati wa kukumbatia dhana nzima ya kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji, ili tufikie azma ya kujitegemea
Akili kama hizi hazitakaa ziisaidie Africa...mkiturudisha tena huko basi hata vizazi vyenu baadaye vitawahukumu kama kina mangungo wa msowero...History is a best teacher!
 
Ni kweli kabisa maana ulifaidika na utawala wake wa kidhalimu, kwa kuwa member wa lile kundi lake la watu wasiojulikana.
Watanzania wote walinufaika na wataendelea kunufaika pamoja na wewe, wazazi wako na mke na watoto wako ( kama unao lakini).
 
Watanzania wote walinufaika na wataendelea kunufaika pamoja na wewe, wazazi wako na mke na watoto wako ( kama unao lakini).

Kama sisi wote tulivyofaidika na miradi ya wakoloni.
 
Ila kama Samia atajaribu viatu vya Magufuli huko ni ku fail 100%
Hivyo viatu kama sio vya kutupa choo cha shimo basi ni vya kuchoma moto.
Magufuli was failure na sio muda mrefu watu wote watajua hilo, lakini Mama Samia ameshalijua hilo.
Ndio maana jana katamka jambo alilokuwa anaona fahari jiwe la kukusanya kodi kuwa "tumieni akili kukusanya kodi sio ubabe wa kijinga".
Mpaka muambiweje kuacha ujinga?
"Ubabe wa kijinga"!!
Nani ni mjinga hapo!!??
Anayeagiza,anayeagizwa au anayetekeleza!!??
Kuna mmoja ni .jinga kupindukiaa!!
 
Kama sisi wote tulivyofaidika na miradi ya wakoloni.
Yeah! Lakini hatuwezi kuendelea kuitegemea hiyo kamwe na ndio maana JPM akaanzisha mambo mapya. Mfano SGR. Au wewe unaona bora tubaki na reli ya Mkoloni?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Yeah! Lakini hatuwezi kuendelea kuitegemea hiyo kamwe na ndio maana JPM akaanzisha mambo mapya. Mfano SGR. Au wewe unaona bora tubaki na reli ya Mkoloni?

Ule ni wajibu wake wala haikuwa hisani maana sio mshahara wake. Naona alidhani kutekeleza miundombinu kadhaa ni ticket ya kutawala kwa mabavu, dhuluma na mauaji, huku akinajisi chaguzi za nchi. Kama miundombinu ni ticket ya kutawala wananchi utakavyo, mbona akina Mandela walimpinga Kaburu Pieter Botha wa Afrika kusini?
 
Mkuu sio kazi Sana ,ila mama kazi kutokana na Jiwe kuvuruga misingi ya utawala Bora inabidi mama aanze upya.
Yule jamaa alikua akilala akiamka anakuja na yake,hafuati katiba wa sheria Wala kanuni za uongozi.
Anajifanyia Mambo kivyake.
Kiufupi hakuwa na sifa ya kiongozi wala hata "mtawala".
Alikuwa "nyonya damu".
 
Mwacheni Rais Samia aongoze kwa maono yake na si vivuli au viatu vya wengine
Kumtaka afuate nyayo ni kumkwaza. Samia ana personality yake tofauti na ya mwendazake

Hawezi kutumia personality yake kufanya ya Marehemu, JK, Hayati Mkapa, Mwinyi au Hayati Nyerere!
kila zama na kitabu chake , ni wakati wake kuandika zama hizi kwa kitabu chake

Katika mambo aliyoandika Mzee Mwanakijiji moja ni sisi kuwa Taifa lililogawanyika.
Kazi ngumu mbele ya mama Samia ni kuliunganisha Taifa lilivyovurugwa na Marehemu

Marehemu aliligawa Taifa kwa namna zozote unazofikiri, iwe jinsia, ukabila, udini , hata rangi

Marehemu hakujali Utu alijali Vitu, Mama Samia arudishe hadhi , heshima na utu wa mwananchi
Kiongozi anaongoza watu si madaraja au miti, hivyo kutojali uhai na maisha ya watu si kiatu cha kuvaa

Hivi mnataka Rais Samia avae viatu vya kukataa sayansi na kuhubiri madogori na mapambio kwa gharama kubwa sana za maelefu ya maisha ya wananchi! kiatu hicho mama asikijaribu wala kukifikiri!

Rais Samia halazimiki kufuta kila kilichoachwa na Marehemu lakini analazimika kufuta mabaya aliyoacha na yaliyoliacha Taifa hili na makovu makubwa sana.

Kiongozi hapimwi kwa Vitu bali Utu. Mwendazake anapimwa kwayo ndiyo maana kipimo cha utu wake kipo mgongoni kama si kushoto. Hukumu yake imesimama katika utu licha ya vitu alivyotengeneza

Mwacheni Rais Samia aongoze kwa zama zake na aandike legacy yake kwa maono yake
Eti tuongozwe kishirikina tena!!?
Hapana.
Mh. Rais Samia Suluhu Hassan,fanya vile ambavyo hekima,werevu,akili na busara zako zinavyokuongoza.
Ongoza Tanzania kwa mujibu wa katiba, sheria, kanuni, miongozo na taratibu tulizojiwekea.
Ongoza Tanzania kwa mujibu wa maono yako.
Ongoza Tanzania kwa mujibu wa ushauri "mwema" unaopewa toka kwa "wateule na wasaidizi" wako.
Ongoza Tanzania kwa mujibu wa muongozo unaopewa na Mungu Muumba.
 
Bora umeliona hilo kwa mleta mada, huyu mleta mada aliamua kumtetea Magufuli, na akaingia kwenye ushindani wa kisiasa humu mitandaoni, saa hii anajiweka kwenye mazingira kuwa SI Unit ya urais eti ni Magufuli. Kwa taarifa yake Magufuli alijikita kwenye miundombinu tu na sio kazi ya urais, anataka kila mtu aamini kuwa rais aliyejikita kwenye miundombinu ni rais bora.

Lakini ukimwambia aseme rais bora kati ya Mandela ambaye hakujenga miundombinu ya maana, na rais Pieter Botha aliyejenga miundombinu kibao huko Afrika Kusini, atakuja na majibu tofauti! Amwache huyo mama afanye kazi na sio kuleta habari za Magufuli.
Yani wanataka wote waendeleze uchawa kwa mwendazake na hata Samia akisifiwa wao wataka awe ka mwendazake huko ka si ku mu undermine madame president ni Nini, Mara waje na assumption baadae watu watamsema kwani kumsifia mtu mwanzo mzuri ni kosa.
I asee to me Mheshimiwa Samia ni far better than Mwendazake, na Raisi mzuri hapimwi kwa miundo mbinu inajumuishwa Mambo mengi. Mama kuongelea tu TRA kutumia nguvu na kupoka watu hela zao nimemwona ana maono, huwezi kukusanya na kufungia watu biashara kibabe bila negotiation hayo ni matumizi mabaya ya akili. So to me Mama kaanza vizuri tuache kumkatisha tamaa
 
Chadema wanaponda kwamba JPM hana la kukumbukwa nalo, wamejikuta wameamia ccm kumuunga mkono Samia wakifikiri wanamkomoa mtu aliye kaburini.

Mimi nawaambia kuna siku itatakiwa sauti ya mamlaka kunyoosha mambo na itakosekana watu watamlilia Magufuli kama kwenye msiba wake.

Mama Samia tayari ni rais wa kwanza mwnamke hiyo ndio legacy yake kubwa ambayo aina mjadala.

JPM atakumbukwa kama kiongozi mwenye ujasiri, mthubutu, mtu asiyetaka mzaha na raslimali za watanzania na anayepigania tabaka la chini lifaidi matunda ya nchi yao. Huyu mtu wa hivi kuna siku atakosekana.
Sielewi mtu anayeandika "aina" badala ya "haina" kama anapaswa kuwa humu jukwaani.
Jiwe atakumbukwa kama kiongozi "sadist" mwenye uthubutu wa kuangamiza wale wote wanaomkosoa na waliomzidi kiuweledi,kiakili, kiushawishi na kiuchumi.
Atakumbukwa kwa kuwa kiongozi aliyekuwa na wivu na sisi matajiri kwa uongo wa kuwapigania tabaka la chini kwa kutupora sisi matajiri huku akijineemesha yeye na genge lake.
 
Mwanakijiji nimependa sana andiko lako, limesheni mambo mengi ya busara na hekima na ushauri mwema.

Nimefurahi sana matokeo ya upinzani kwa mama Samia, amepokewa kwa bashasha na upendo wa hali, pia ameonyeshwe ushirikiano. Yaliyobaki tunamwachia yeye atuthibitidhie kilichopo kifuani na kichwani mwake ( ndani ya moyo na akili yake )

JPM tulimpokea kwa kukataa matokeo ya Uchaguzi na kutaka kuitisha maandamano nchi nzima kulazimisha matokeo yafutwe na uchaguzi urudiwe.
Tulipinga hatua zake nyingi za kisiasa alizochukua na tulizibeza hatua zake za kiuchumi alizochukua. Yawezekana tulimuonyesha hatumtaki tangu mwanzo na kumlazimisha achague upande wa kuegemea. Yeye akaamua kama alivyo amua, yawezekana sisi ndio tulimsukuma awe mkamiti juu yetu.

Mama Samia ame pata wa saa mzuri wa kurekebisha mapungufu ya mtangulizi wake na kutuonyesha upendo ambao tuliusahau.
Unapomkosoa mwenye má lakini ni vizuri kujivunia kumtupa na, kumbe za, kumdhihaki na kumdharau kwa kuwa lazima tujuwe yeye anaweza kubembeleza na kuadhibu.

Pamoja na yote hayo muda ni mwalimu mzuri, tumepata elimu ya kutosha kupitia Rais aliyepita kwa pande zote mbili kwa ujumla wetu, Watawaliwa na Watawala.
Ni binadamu sukule (taahira/aliyetolewa ubongo) anayeweza jiita yeye ni "mtawaliwa".
Dunia ya sasa inahitani viongozi na waongozwaji/wananchi, na si mtawala na watawaliwa.
 
Na. M. M. Mwanakijiji
(Makala hii imetoka kwenye gazeti la Raia Mwema, Jumatano Machi 31, 2021. Picha juu kutoka kwa Michuzi Blog).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ana kibarua kigumu. Anakabiliwa na kuridhisha pande nyingi kiasi kwamba upande wowote ambao hatouridhisha au hatoonekana kuuridhisha hautachelewa kumpinga na upande ambao utaonekana unapendelewa utachukiwa na ule upande mwingine. Kama kuna mtu anadhania kuwa Rais Samia atafanya Watanzania wote tushikane mikono na kuanza kuimba kwa pamoja “Ukuti Ukuti” kana kwamba hatuna tofauti za msingi mtu huyo anajidanganya. Tofauti na mtangulizi wake Rais Samia anaingia akiwa anakabiliwa na changamoto ambazo hakuna Rais mwingine yeyote wa Tanzania amewahi kuzipata. Ni katika hili hekima, ujasiri, ubunifu, na uthubutu wake utaenda kupimwa na labda ataangaliwa kwa macho makali zaidi kuliko Rais mwingine yeyote.

Viatu vya Magufuli
Upande wa kwanza anakabiliwa kujaribu kuvivaa viatu vya kiungozi vya Magufuli. Mtu anapojaribu kuvaa viatu vya mtu mwingine anakabiliwa na changamoto; ama vitamtosha, vitambana, au vitampwaya. Kama vitamtosha bado ataangaliwa kama vimemkaa; vinaendana naye au la; kama vitambana swali ni kwa kiasi gani au vipanue au atafute vingine; na kama vitampwaya ni je anahitaji kuongeza nini ili vimtoshe au bado atahitaji kutafuta vile vinavyomtosha tu hadi atakapokuja mwingine ambaye viatu hivyo vitamtosha.

Rais Samia atahukumiwa kwanza kwa kabisa ni kwa kiasi gani ataenda kusimamia miradi mikubwa “ya kimkakati” iliyoanzishwa chini ya Rais Magufuli. Ni kwa kiasi gani mradi wa SGR (treni ya umeme) utaenda kukamilika na kusimamiwa; mradi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere, na kuhamia Dodoma. Hii ni baadhi tu ya miradi hiyo. Uzuri ni kuwa kwa vile alikuwa ndani ya serikali hii toka mwanzo mama Samia inawezekana ni mtu pekee anayeilewa na kujua ni kwa kiasi gani inahitajika na hivyo kwake inaweza isiwe ngumu kabisa kufuatilia miradi hii mikubwa, ile ya kati na midogo.

Kama tulivyoshuhudia suala la ubadhirifu, ufisadi na kutokuridhika na utendaji kazi aliouonesha siku ya Jumapili akipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali; Rais Samia atahukumiwa pia ni kwa jinsi gani hatoacha uzembe, kubebana na kupeana “second chances” kutaendelea. Hii ina maana hatoacha wateuliwa wa Rais Magufuli ambao wanapwaya sasa hivi na labda walishaonekana wanapwaya. Je, atatakiwa asubiri hadi arudi ofisini kabla ya kuchukua hatua au atachukua hatua pale pale kwa staili ya Magufuli ya “kutumbua”. Je, tumbua yake itakuwa ni ile ya kupisha uchunguzi ili mtu achunguzwe kabla ya kumfuta mtu kazi papo kwa papo kama alivyokuwa akifanya Magufuli?

Ataangaliwa kwa jinsi gani analiongoza taifa kuelekea kujitegemea kuliko kurudi kwenye kutegemea. Je, katika hili atatumia lugha tofauti kuliko ile ya Magufuli? Je, katika kujitegemea atajaribu kulitenga taifa na dunia au atajaribu kuliweka taifa katika nafasi yake sahihi ya kushirikiana na dunia. Kwamba, kama Magufuli hatolirudisha taifa katika aibu ya kuombaomba hata kwa vitu visivyoombeka? Je, ataanza safari za kwenda duniani kujitambulisha na kuomba misaada tena? Au ataangalia kimkakati ni wapi Watanzania bado tunaweza? Na katika hili tena alikuwa chini ya mwalimu mzuri. Rais Samia aliona na kuielewa kiu ya Rais Magufuli ya kuona Watanzania wanajiamini na kuwa hawajioni wanyonge; na jinsi gani aliwahusisha Watanzania katika kutekeleza mambo mbalimbali bila kusubiri vibali vya wakubwa wa dunia.

Ni kwa sababu hiyo wapo watakaoangalia na kuona kama amevivaa viatu vya Magufuli au vimemvaa yeye; ama ameingia na viatu vyake na vikapendeza zaidi kuliko vile vya Magufuli. Akaamua kupita alikopita Magufuli lakini kwa hatua zake na kwa mwendo wake. Inawezekana akawa ametengenezewa njia nzuri zaidi ya kupita na Magufuli na yeye akaipita kwa urahisi zaidi kuliko kama mtangulizi wake asingekuwa Magufuli.

Kivuli cha Magufuli
Lakini Rais Samia pia anauamuzi wa kwake mwenyewe. Japo ameingia kuziba pengo la Magufuli na chini ya mwaka mmoja tu wa ngwe yao ya pili kwa kweli si lazima afuate kila alichofanya Magufuli. Si lazima azungumze alivyozungumza Magufuli, si lazima aoneshe ukali kama Magufuli au afanye maamuzi kama alivyofanya Magufuli. Kwa hakika kabisa japo kinadharia hapaswi kwenda nje ya Ilani na ajenda yao na Magufuli lakini pia hafungwi kuanzisha ya kwake na hata kufutilia mbali ajenda ya Magufuli. Lakini vyovyote atakavyoamua kufanya kivuli cha Magufuli kitaendelea kumfunika.

Kundoka kwa Magufuli na kumwachia Samia kunamfanya Samia aingie akiwa na jukumu kubwa la kuonesha siyo tu alikuwa Makamu lakini alikuwa Makamu aliyeweza kuwa Rais kama historia inaita hivyo. Kumuondoa Ronaldo uwanjani kunatoa nafasi kwa mchezaji wa akiba kuonesha kama anastahili kuchukua nafasi ya mchezaji huo nyota. Lakini uchezaji wote utapimwa na kuona kama anaweza kutoa mchango wa kuisaidia timu kushinda. Mama Samia anaingia kuchukua nafasi ya mchezaji nyota; ni jinsi gani ataifungia magoli timu yake na kuisadia kushinda na hivyo kujihakikishia namba ni suala la muda.

Lakini la muhimu ni kuwa si lazima afanye kazi akiwa na kivuli cha Magufuli mgongoni. Japo, anaenda kuibeba ajenda ya Magufuli si lazima aibebe mabegani kama Magu kama ana uwezo wa kuibeba kichwani. Kivuli cha Magufuli kisiwe kizuizi bali kiwe ni daraja la kuvukia kwenda anakotaka kuipeleka Tanzania. NI kwa sababu hiyo asiogope, asifikirie mara mbilimbili, au hata kujishuku endapo ataamua kufanya mabadiliko ya lazima ambayo labda Magufuli asingeyafanya. Kipimo chake sasa siyo Magufuli tena bali ni yeye mwenyewe kama Rais. Kauli yake msibani kuwa aliyesimama pale ni “Rais” itume ujumbe kwa yeyote mwenye shaka na shuku; kwamba siyo tu yeye ni Rais bali pia madaraka aliyokuwa nayo Magufuli ndiyo aliyonayo yeye leo; uwezo aliokuwa nao Magufuli aliopewa na Katiba ndio uwezo ule ule aliopewa yeye. Yeye sasa anatakiwa kutengeneza kivuli chake mwenyewe na akifanya vizuri basi atajitengenezea haki na nafasi ya kutengeneza ajenda yake ya 2025 akitaka kugombea tena.

Tanzania ya Samia
Ni wazi basi kuwa Watanzania wanapompokea Rais wao mpya wapo wenye matarajio mengi na yenye kutofautiana. Wapo ambao wanatarajia kuwa anaingia na kuwa kama Rais kutoka upinzani ambaye atafutilia mbali jina, historia, mafanikio, na maamuzi yote ya Magufuli na hivyo kutengeneza historia (legacy) yake mwenyewe nje ya Magufuli. Kwamba, akijiweka mbali na Magufuli na ajenda yao basi atakubalika zaidi na wapinzani na wakosoaji wa Magufuli. Kwamba, atake kupendwa na wale waliomchukia Magufuli.

Lakini pia anaweza akajikuta anajitahidi sana kuwa kama Magufuli na kujikuta anatengeneza maadui na wakosoaji wengi zaidi kuliko aliokuwa nao Magufuli na hivyo kuoneakana ni Magufuli 2.0. Changamoto kubwa ya Tanzania hii ya Samia ni kutafuta mizania kati ya alikotoka na Magufuli na anakotaka kwenda bila Magufuli. Je, itakuwa ni Tanzania ya namna gani? Je, watu wake watasimama vipi? Je, atatengeneza taasisi na kuinua watu kwa namna gani? Je, anatamani iwe Tanzania ya namna gani. Swali hili naamini litajibiwa siku si nyingi pale atakaposimama kulihutubia taifa na kutoa mwelekeo wa maono yake kwa taifa na tutaona atakavyoanza kuipanga serikali yake ili kutimiza maono hayo.

Kwa sasa ni wazi kuwa Watanzania bado wamegawanyika na wanasubiria kuona kama mgawanyiko wao utaendelea kuwa ni wa kudumu au utawasogeza karibu karibu au utapanua zaidi mgawanyiko huo. Kwa kweli, siwezi kumuonea wivu katika kibarua hiki. Ninachomtakia ni kila la kheri katika kuliongoza taifa letu na kuwa vyovyote atakavyokuwa historia itaweza kumhukumu si kwa jinsi gani alivyokuwa kama Magufuli au kwa jinsi gani alivyokuwa tofauti na Magufuli; atahukumiwa kwa jinsi gani aliliongoza taifa letu kuelekea mafanikio ya kweli, ubora wa maisha, kuinuliwa kwa tunu zetu mbalimbali za kitaifa kiasi kwamba ije kusemwa Tanzania ya Samia ilikuwa ni Tanzania tuliyoitarajia.

Na ili kuifikia Tanzania hiyo ni lazima tukatae mbinu, majaribio au hata jitihada zozote za kumshusha Rais Samia, kumdhoofisha au kumtendea kana kwamba si Rais “kamili” kwa sababu tu ni mwanamke. Tukatae tena kwa ukali wote unaostahili lugha zote za kinyanyasaji kijinsia ambazo nyingine zimeenea mitandaoni. Tuwakatae wale wote wanaozungumza kana kwamba wanamuunga mkono lakini wanafanya hivyo ati kwa sababu “ni mama” kana kwamba umama wake ni kitu cha kumdhoofisha.

Tujue kuwa anaingia madarakani akiwa na nguvu zote kama Rais wa Tanzania bila kujali jinsia yake. Lakini pia inatupa nafasi ya kuwa na kiongozi ambaye ana mtazamo tofauti kuliko wengine na hivyo labda ataweza kuwainua pia wanawake wengi wenye uwezo ambao labda hawakupata nafasi zozote za juu za uongozi kwa sababu ya mitazamo mibaya ya kijinsia (gender biases).

Lakini pia naamini atawapa nuru mabinti zetu kutamani kufikia nafasi yoyote ya uongozi wa nchi yetu na kuwa wale wote wenye nafasi za uongozi wafanye hivyo kwa weledi mkubwa zaidi bila kuonekana wanajikomba kwa mwanamme yeyote. Na kama nitakavyoonesha wiki ijayo kuna mambo ambayo naamini Rais Samia ni LAZIMA ayafanye tofauti na Magufuli.

Katika Tanzania ya Samia hakuna cha kuhofia.

Niandikie: klhnews@gmail.com
The man is dead. You guys have to learn to live with it!

Hakuna kivuli chochote 'cause the man is now lying 6M deep in the soil while his cronies (Kakoko, Bashiru - to mention just a couple) are being chucked out one after the other!

Mama SSH is a breath of fresh air to Tanzanians.... albeit the lesser of the devils crowd.

Exit brawn, enter brain!
 
The buck stops with you madam President.

You are the dealer for the reminder of the term(and possibly beyond) and obviously you can’t pass it over to anyone else leastways the dead.

My congrats and symphasies but be very selective of the tunes you listen and dance to.
 
Never! Yani ikifikia point naanza kumkumbuka Jiwe SIJUI!
Nitakufuatilia, miaka 10 nitakuja kuona kama bado una haya mawazo...

Lakini uzuri ni kuwa amekufa akiwa hajageuza kauli yake huo ni ushindi ambao Mungu mwenyewe kampa...Naye mtoa hukumu ya haki atatupa muda wa kupima mawazo na matamanio yetu...Yeye kafa hivyo kaumbika sisi je? Time is a good healer, naomba Mungu tusijekusutwa makaburini na vizazi vyetu...
 
Ni binadamu sukule (taahira/aliyetolewa ubongo) anayeweza jiita yeye ni "mtawaliwa".
Dunia ya sasa inahitani viongozi na waongozwaji/wananchi, na si mtawala na watawaliwa.
Umeongea vizuri sana, lakini hiyo ni nadharia kwa Tanzania yetu ya leo. Hali tunayo itaka haijafika kwetu. Tunachokipata ama huwa hatukitaki na ikitokea tumekipata huchukua muda sana kutokea na huwa sio sahihi sana. Decision are always made without our input. Where necessary the decision has to be made informed by our input, the deciders select what? When? Where to implement it.
 
Ndio maana watumishi wanapuuzwa na hakuna anayewajali kwasababu ya ubinafsi wao.
Most are selfish and with high time preferences...Hawataki kuwekeza wanataka kula mbegu badala ya kuipanda izae...Kiuhalisia watumishi wengi output yao ni ndogo compared na salaries....Wamekosa ubunifu na wana dublicate activities ili tu waonekana wanajishughulisha hata kama hiyo shughuli haiongezi tija kwa taifa...
 
Back
Top Bottom