Alphonce Mawazo
R I P
- Sep 10, 2013
- 335
- 478
Ndoto kubwakubwa za wanasiasa na wanataaluma vijana zimeuawa na vihela vidogo vidogo visivyojaa hata bahasha ndogo.
Kwa wanasiasa vijana wameamua kutumikishwa na wakongwe wa siasa na kazi yao kubwa ni kutumwatumwa kama vijakazi ingawa wanapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na kuitwa majina mazuri mazuri ya uongo.
Kazi yao kubwa Hawa vijana ni kutengeneza fitina na kutukana waliotumwa kuwatukana,wamekuwa kama vijibwa vidogo vidogo vinavyoamuriwa mbwekee huyu au yule bila kuhoji kwa nini.
Utavikuta Dodoma wakati wa bunge utafikiri ni madreva au mautingo wa magari, hulala kwenye hotel cheap cheap huku vikiwinda mademu kwa ajili ya mabosi wao,vina akiri lakini vimeamua kuwa Vijinga,
Kundi la pili ni la wanataaluma,wanalipwa mishahara viduchi sana mwisho wa mwezi,vinabebeshwa mizigo mizito kama punda lakini wanauwezo wa kuanzisha biashara au kufungua ofisi zao kubwa maishani na kujenga taasisi kubwa duniani.
Kama ilivyo kwa punda awekewavyo karoti mbele yake na kuburuta mzigo mzito ili aifikie karoti na akiipata huitafuna yote bila kuacha akiba kisha huwekewa nyingine tena ndivyo ilivyo kwa waajiriwa hawa na vibahasha vya mwisho wa mwezi.
Katika kundi hili la wanataaluma naumizwa zaidi na waandishi wa habari vijana ambao mchana kutwa utawaona wanavyopigwa vumbi na jua kwenye mabenchi ya ofisi za wakubwa kutafuta habari,ukweli ni kwamba hawatafuti habari bali vibahasha vya kaki vyenye elfu thelathini ili waandike sifa za uongo kwa mafisadi na walarushw hao.
Taarifa za ukweli ziko vijijini ambako kuna mateso ya kila aina,matukio ya kutisha ambayo wakiyaandika na kuyaripoti yatawakuza sana sana,shida huko hakuna bahasha ukiwaita watakuuliza bahasha..bahasha...bahasha,ndiyo maana watazeekea kwenye mabenchi ya wakubwa.Hawako tayari kusota,kutembea kwa miguu,kulala na njaa ili wakue na kutimiza ndoto Zao.