"Katika kundi hili la wanataaluma naumizwa zaidi na waandishi wa habari vijana ambao mchana kutwa utawaona wanavyopigwa vumbi na jua kwenye mabenchi ya ofisi za wakubwa kutafuta habari,ukweli ni kwamba hawatafuti habari bali vibahasha vya kaki vyenye elfu thelathini ili waandike sifa za uongo kwa mafisadi na walarushw hao.
Taarifa za ukweli ziko vijijini ambako kuna mateso ya kila aina,matukio ya kutisha ambayo wakiyaandika na kuyaripoti yatawakuza sana sana,shida huko hakuna bahasha ukiwaita watakuuliza bahasha..bahasha...bahasha,ndiyo maana watazeekea kwenye mabenchi ya wakubwa.Hawako tayari kusota,kutembea kwa miguu,kulala na njaa ili wakue na kutimiza ndoto Zao."