Vibahasha vya khaki vinavyozuia harakati na kuua ndoto za vijana

Vibahasha vya khaki vinavyozuia harakati na kuua ndoto za vijana

Kamanda angalia Sifa
ulizozipata kwenye harakati zako ndani ya CDM huko kanda ya Ziwa hadi
kupewa jimbo la kalenga wakati wa kampeni zisije haribikia hapa JF. JF
sio sawa na Jukwaani ukishika MC basi wengine kimya kwa mwendo huu
nakupa miezi mitano.

Tatizo nini hapa...
 
Vijana wengi katika nchi hii ni njaa kali na hii inakuwa rahisi mno kwa chama tawala kuwarubuni.
 
Asante sana Kamanda Mawazo ndio maana tutazidi kuwabana wasaliti kwenye chama chetu wanaopandikizwa na hao nyoka wakijani wenye kuangamiza nchi kwa uchumia tumpo tusongeni mbele kuwaelimisha asante sana kamanda wangu
 
Mimi huwa nashangaa sana mtu kuhongwa visenti kiduchu kiasi cha kujitoa ufahamu. Nimekua nikifuatilia sakata la ZZK na ACT yake, pamoja na waraka ule wa Mwigamba na Kitila nikashangaa sana. Yaani figure za viposho ni kiduchu kweli kweli, lakini ndio hivyo vijana wanachangamkia kama nini.

Mungu atusaidie kwa kweli, atufumbue macho.

This is our country, we don't have any other country. Kama tunaihujumu nchi eti kwa kujiona kwamba tunamkomoa Mbowe au Slaa then tunajidanganya.
 
Wewe ni wa kupuuzwa tu, unafanya usanii, huna dhamira ya kweli.
Wapuuzi kama wewe ndo hatuwataki, unawezaje kumkanusha mtu bila opposite facts?
Lete facts zako za ku-support unachokisema otherwise you are also homostupid!
 
Kamanda angalia Sifa ulizozipata kwenye harakati zako ndani ya CDM huko kanda ya Ziwa hadi kupewa jimbo la kalenga wakati wa kampeni zisije haribikia hapa JF. JF sio sawa na Jukwaani ukishika MC basi wengine kimya kwa mwendo huu nakupa miezi mitano.
Uoga ni kitu kibaya sana maishani mdogo wangu... shida na taabu tunazokutana nazo maishani ni zaidi ya siasa za Jf...pole yako
 
Upo sahihi mkuu,vijana wamekuwa wakitumiwa kama daraja tu huku wao wakibaki ombaomba na watu wa kujipendekeza pendekeza ili tu angalau wapate makombo kwenye vibahasha.

Hata hapa JF utakuta wanaanzisha vijipost visivyo na maana wala faida kwa maskini wa Tz wanaosulubishwa na maisha mithili ya jehanamu,kwao bahasha za kaki ni zaidi ya mateso wanayopata wakulima, wafanyakazi, machinga, wazee wanaokosa huduma muhimu,akina mama wanaojifungulia chini sakafuni,wananchi wanaoporwa makazi yao na kuvunjiwa nyumba zao ili kuwapisha wawekezaji uchwara.

Jamani hii ni nchi yetu sote na hivi vibahasha haviwezi kutusaidia chochote, havitaweza kutusomeshea watoto wetu na tusikubali kuwa watumwa wa vitu vidogovidogo.
 
Mkuu alphoce Mawazo, na mimi ngoja nikuite kama kaka unavyotambulika humu, hivyo kamanda Alphonse Mawazo, kwanza asante kwa bandiko lako hili!,

Kuhusu vijana kwenye uzi huu umezungumzia vitu vitatu vikuu,

  1. Ndoto
  2. Taaluma, professionalism
  3. Reality, (bahasha)
  4. What is vs what ought to be
Mimi nimeguswa pale tuu ulipowazungumzia vijana waandishi wa habari kwa sababu na mimi ni mwandishi wa habari na mwanzo pia nilikuwa kijana!.

Umeanza hivi
Ndoto kubwakubwa za wanasiasa na wanataaluma vijana zimeuawa na vihela vidogo vidogo visivyojaa hata bahasha ndogo.

Jee ni kweli hawa waandishi vijana walikuwa na ndoto kubwa kubwa?!. Ndoto gani hizo zilizouwawa na vihela vidogo vidogo visivyojaa bahasha?!.

Katika kundi hili la wanataaluma naumizwa zaidi na waandishi wa habari vijana ambao mchana kutwa utawaona wanavyopigwa vumbi na jua kwenye mabenchi ya ofisi za wakubwa kutafuta habari,ukweli ni kwamba hawatafuti habari bali vibahasha vya kaki vyenye elfu thelathini ili waandike sifa za uongo kwa mafisadi na walarushw hao.
Unaumizwa na na jinsi
wanavyopigwa vumbi na jua kutafuta habari?,
wanavyoshinda kwenye mabenchi ya wakubwa bila kutafuta habari?,
wananavyotafuta vibahasha vya khaki vyenye elfu 30?
wanavyoandika sifa za uongo za mafisadi na wala rushwa hao?.

Taarifa za ukweli ziko vijijini ambako kuna mateso ya kila aina,matukio ya kutisha ambayo wakiyaandika na kuyaripoti yatawakuza sana sana
Kumbe taarifa za ukweli ni zile tuu zilizoko vijijini?!, ndio maana wanaandika sifa za uongo?!, ila pia umetoa sababu za wao kutokwenda vijijini
shida huko hakuna bahasha ukiwaita watakuuliza bahasha..bahasha...bahasha,ndiyo maana watazeekea kwenye mabenchi ya wakubwa.Hawako tayari kusota,kutembea kwa miguu,kulala na njaa ili wakue na kutimiza ndoto Zhao.
Msingi halali wa bahasha za waandishi ni kuwezesha kutimiza makumu yao kikamilifu, na haswa logistics, mimi naziita hizi ni bahasha halali za uwezeshaji!, waandishi kama taaluma nyingine zote, wanabidi wawezeshwe ili watimize majukumu yao kikamilifu!.

Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini, hivyo ni kweli huko vijijini ndiko kwenye habari nyingi, ila pia ili kuzifikia habari hizo huko ni lazima waandishi wawezeshwe ki logistic ili wafike huko kijijini, hakuna sababu ya waandishi kusota, kutembea kwa miguu, kulala nje, kulala njaa, akifuata story kijijini!, kama hakuna logistic za kuwafikisha waandishi vijijini, then waacheni waandishi tubanane hapa hapa mjini!.

Kwa uelewa zaidi kuhusu Waandishi na bahasha, pitia hapa
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni rushwa!

Pasco
 
Last edited by a moderator:
Kamanda mawazo pamoja sana lakini umesahau na kundi lingine hawa ni wanawake vijana na wasanii Wa kike sijawahi kuwasikia wakienda vijijni kuelemisha wanawake walioko vijijini Wako tu Dar wakitoka Dar wanaenda Arusha ,mwanza,Dodoma na mbeya kwishnei kuna sehemu nchi wanawake wanaishi vijijini mateso makubwa wanapata huko mkoa Wa mara,simiyu na rukwa/katavi.lakini utawakuta Wako Dar kazi Yao kupamba magazeti ya shingongo kazi Yao kujipendekeza kujiunga nA ccm chama cha kinyonyaji na kurekodi maisha ya kifahari wakti makwao wanaishi kwenye nyumba za tembe.
 
Kamanda Mawazo kwa nini usiwe na ukurasa wako kwenye magazeti au vipindi kwenye radio ili jamii inufaike kwa upana zaidi?

Hivi we ni Dr kweli au mganga wa mitishamba? Sijaona alichoandika mpaka awe na ukurasa kwenye gazeti au kipindi cha Redio.

By the way unajua huyo Mawazo ana elimi gani? Tumia kichwa kufikiria siyo kufugia nywele.
 
leo umepost mambo ya maana. sio zile pumba za juzi.

Ndoto kubwakubwa za wanasiasa na wanataaluma vijana zimeuawa na vihela vidogo vidogo visivyojaa hata bahasha ndogo.

Kwa wanasiasa vijana wameamua kutumikishwa na wakongwe wa siasa na kazi yao kubwa ni kutumwatumwa kama vijakazi ingawa wanapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa na kuitwa majina mazuri mazuri ya uongo.

Kazi yao kubwa Hawa vijana ni kutengeneza fitina na kutukana waliotumwa kuwatukana,wamekuwa kama vijibwa vidogo vidogo vinavyoamuriwa mbwekee huyu au yule bila kuhoji kwa nini.

Utavikuta Dodoma wakati wa bunge utafikiri ni madreva au mautingo wa magari, hulala kwenye hotel cheap cheap huku vikiwinda mademu kwa ajili ya mabosi wao,vina akiri lakini vimeamua kuwa Vijinga,

Kundi la pili ni la wanataaluma,wanalipwa mishahara viduchi sana mwisho wa mwezi,vinabebeshwa mizigo mizito kama punda lakini wanauwezo wa kuanzisha biashara au kufungua ofisi zao kubwa maishani na kujenga taasisi kubwa duniani.

Kama ilivyo kwa punda awekewavyo karoti mbele yake na kuburuta mzigo mzito ili aifikie karoti na akiipata huitafuna yote bila kuacha akiba kisha huwekewa nyingine tena ndivyo ilivyo kwa waajiriwa hawa na vibahasha vya mwisho wa mwezi.

Katika kundi hili la wanataaluma naumizwa zaidi na waandishi wa habari vijana ambao mchana kutwa utawaona wanavyopigwa vumbi na jua kwenye mabenchi ya ofisi za wakubwa kutafuta habari,ukweli ni kwamba hawatafuti habari bali vibahasha vya kaki vyenye elfu thelathini ili waandike sifa za uongo kwa mafisadi na walarushw hao.

Taarifa za ukweli ziko vijijini ambako kuna mateso ya kila aina,matukio ya kutisha ambayo wakiyaandika na kuyaripoti yatawakuza sana sana,shida huko hakuna bahasha ukiwaita watakuuliza bahasha..bahasha...bahasha,ndiyo maana watazeekea kwenye mabenchi ya wakubwa.Hawako tayari kusota,kutembea kwa miguu,kulala na njaa ili wakue na kutimiza ndoto Zao.
 
Mkuu alphoce Mawazo, na mimi ngoja nikuite kama kaka unavyotambulika humu, hivyo kamanda Alphonse Mawazo, kwanza asante kwa bandiko lako hili!,

Kuhusu vijana kwenye uzi huu umezungumzia vitu vitatu vikuu,

  1. Ndoto
  2. Taaluma, professionalism
  3. Reality, (bahasha)
  4. What is vs what ought to be
Mimi nimeguswa pale tuu ulipowazungumzia vijana waandishi wa habari kwa sababu na mimi ni mwandishi wa habari na mwanzo pia nilikuwa kijana!.

Umeanza hivi

Jee ni kweli hawa waandishi vijana walikuwa na ndoto kubwa kubwa?!. Ndoto gani hizo zilizouwawa na vihela vidogo vidogo visivyojaa bahasha?!.

Unaumizwa na na jinsi
wanavyopigwa vumbi na jua kutafuta habari?,
wanavyoshinda kwenye mabenchi ya wakubwa bila kutafuta habari?,
wananavyotafuta vibahasha vya khaki vyenye elfu 30?
wanavyoandika sifa za uongo za mafisadi na wala rushwa hao?.

Kumbe taarifa za ukweli ni zile tuu zilizoko vijijini?!, ndio maana wanaandika sifa za uongo?!, ila pia umetoa sababu za wao kutokwenda vijijini

Msingi halali wa bahasha za waandishi ni kuwezesha kutimiza makumu yao kikamilifu, na haswa logistics, mimi naziita hizi ni bahasha halali za uwezeshaji!, waandishi kama taaluma nyingine zote, wanabidi wawezeshwe ili watimize majukumu yao kikamilifu!.

Asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini, hivyo ni kweli huko vijijini ndiko kwenye habari nyingi, ila pia ili kuzifikia habari hizo huko ni lazima waandishi wawezeshwe ki logistic ili wafike huko kijijini, hakuna sababu ya waandishi kusota, kutembea kwa miguu, kulala nje, kulala njaa, akifuata story kijijini!, kama hakuna logistic za kuwafikisha waandishi vijijini, then waacheni waandishi tubanane hapa hapa mjini!.

Kwa uelewa zaidi kuhusu Waandishi na bahasha, pitia hapa
Waandishi wa Habari na Bahasha: Sio Kila Bahasha ni rushwa!

Pasco

KAMA OFISI HAIWEZI KUGHARAMIA WAFANYAKAZI WAKE HADI MAFISADI WATIE MKONO , ni BORA KUACHA KAZI KULIKO KUKONGOROKEA KWENYE MABENCHI YA MAFISADI KUSUBIRI BAHASHA .
 
Last edited by a moderator:
Hivi we ni Dr kweli au mganga wa mitishamba? Sijaona alichoandika mpaka awe na ukurasa kwenye gazeti au kipindi cha Redio.

By the way unajua huyo Mawazo ana elimi gani? Tumia kichwa kufikiria siyo kufugia nywele.

umetia aibu sana .
 
Back
Top Bottom