Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

WEWE NI MACHINGA HUNA LOLOTE.
 
Hapa nategemea hao machinga kujibu mashambulizi kwa kutumia aina yoyote ya siraha watakayokuwa nayo mkononi
 
Tangazo limesema wenye vibanda waviondoe kwasababu waenda kwa miguu wanakosa nafasi ya kupita. Badala yake watumie miamvuli kufanya biashara zao.

WAVUNJE VIBANDA PEMBEZONI MWA BARABARA HALAFU WATUMIE MIAMVULI.
Kwa maana hiyo hapo kinachokatazwa ni vibanda vilivyojengwa tu, ila wao waendelee kupiga mzigo kama kawaida kwa kutumia miamvuli.
 
Wawekewe utaratibu mzuri wa mahali kwa kufanya buashara zao.
Vinginevyo tutaongeza wezi mitaani.
 
Kwa kweli waondoke maana hali imekuwa mbaya maana nje ya maofisi kumegeuzwa hotel hadi wanapikia majiko ya gas wameset meza na viti na miavuli ya pepsi kama hotel kabisa pale Akiba. Siku likitokea janga la moto sijui kama majengo ya ofisi na mali zao kama yatasalimika.
 
I second you mkuu. Nishaongea Sana hili hapa Jukwaani tangu kitambo. Lakin SIJUI ni kwanini hawatengewi maeneo
 
Magufuli ameiharibu nchii hii. Wamlaumu Magufuli kwa kuwaelekeza kuvunja Sheria. Wamguate huko wamkabe makofi
Magufuli ni marehemu kwa sasa. Mimi na wewe ni marehemu watarajiwa. Punguza machungu ya nafsi yataishia kukuumiza na kukupatia maradhi.
 
Bongo kila anaekuja anakuja na mambo yake na hakuna wa kumfunga 'Paka kengele'.
-Raha hadi basi.

Kuna Mpuuzi ataniuliza;
"Nani kasema nyong'onyon'gonyong'o ndie aliesema",

Kwani huna Akili?

Nawasilisha.
 
Hii inafaa ifanyike baada ya kuwapatia wamachinga Alternative kinyume cha hapo ni kutaka kuyafanya maisha ya wamachinga yawe magumu sana na hili halikubaliki.

Wapeni wamachinga mbadala msituletee social unrest nchini.

Mlichukua 20000 zao halafu mnawafanyia mambo ya ajabu?
 
Pale kariakoo kuna majengo yanayotaka kuendana na unayoyasemea hapa,ila wanadai kule juu hamna biashara,wateja awapandi!,kikubwa serikali iandae maeneo ya machinga nje ya mji,soon pale mbezi kutakua kama kulivyokua mbagala mwisho na tandika,jamaa wangetafutiwa eneo mapema sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…