Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Naomba sana hili lifanyike kwenye majiji yote

Yaani jiji la kitalii Arusha ukipita barabara ya kuelekea stand kuu unakutana mpaka na vitanda, magodoro, makabati yaliyofubaa n.k

Vibanda viondolewe vyote
Yani Arusha ndio inasikitisha yani... Mtalii anatoka Ulaya huko anakuja anakutana na uchafu kila kona..
 
Shida inaanzia hapo kwenye floors wateja hatuna utamaduni wa kupanda magorofa zaidi ya floor 2! Ikizidi hapo ujue huyo wa 3 na kuendelea itakula kwake ndo maana hata pale complex machinga hawapataki! Wateja wa wamachinga tunawajua!

Kama ni kuua eneo labda waue block 1 itandazwe jengo la floor 2 ndani ya acres 6 labda! Iwe Kariakoo Machinga Mall! Waue mtaa mmoja hata ule wa wauza simu ambao hauna maghorofa mengi!
 
Yani Arusha ndio inasikitisha yani... Mtalii anatoka Ulaya huko anakuja anakutana na uchafu kila kona..
Mpaka magodoro, majiko ya gesi ysliyooza na takataka zingine, hasa kutoka barabara ya round about ya mianzini kushuka stand kuu pana muonekano mbaya sana

Kingine ni hawa mama lishe wamekuwa wengi sana kila kona na ndoo zao

Watengewe mahala rasmi.
 
msimu WA Baba yetu utatulinda
Kwani mmeambiwa msiuze? Fanyeni biashara halali mahali panapofaa wateja watawafuata. Kwanza walio wengi biashara si zao wamewekwa na wakwepa kodi kwa ujira kiduchu. Acheni kudeka!
?
 
Wewe jamaa unaielewa vyema concept ya marching guys! Na hawa watu asili yao ni kutembeza bidhaa ila walipoiboresha huduma kwa kuona kutembea hamna tija ndio wakaamua kuwategea wapita njia sasa!

Sasa mtu wa aina hii kumtengea eneo ni kumfunga hela kwa kweli sababu purchases zetu huwa ni unplanned! Mie siwezi kupanga kuwa leo naenda kununua lamba lamba ila nikikutana na yule muuzaji nanunua on spot! Siwezi kupanga kununua korosho ila nikikutana nazo nanunua chap.

Hoja ya kuwa embed kwenye vituo vya madala dala nakubaliana nayo kabisa! Na pawe ni eneo la chini tambarare kama ki sub-market chao hapo watu wataingia na kupata mahitaji yao kirahisi! Ni rahisi sana kama watajengewa hubs stand za dala dala mle!
 
Mkuu ishu hapo tusiangalie upande mmoja, je! Hawa machinga wameshatengenezewa mazingira ha kuamishiya biashara zao. Suala ni kuandaa mazingra wezeahi ndipo watolewe maeneo ya town
By the way wanachafua mazingir
 
Hii Nshu ya wamachinga kwa Humu Jf, imenifanya nigundue Kua members wa humu wengi ni wafanya biashara wakubwa, wameajiriwa na hawana ndgu hoe hae,kama wamachinga ,mama ntilie....So kwao hawa watu wakifukuzwa bila kuandaliwa mazngra mazuri ni sawaa tu.....Dahh inafkrisha chuki na ubnafsi ndani yetu sie Binadamu.
 
Ha ha ha!!!! Awamu ya sita hii. Tutademka sana. Asante mama mji sasa utakuwa safi!!!
Huwa nawakubali MAMA na DADA zetu kwa Usafi aisee hii ndio nature yao na nililitegemea hili. ila ANGALIZO isije kuwa mambo ya "Tengeneza tatizo halafu Tatua tatizo "
 
Hao wenye maduka pia wao ni madalali wa uchumi wa wapi mzee maana 80% ni asian countries products
The same same wote nao ni wachuuzi na sio wazalishaji.Tunataka watu wazalishe tuuze nje na sio kuwa soko tu.
Watu walime bamia wauze Kenya,parachichi China,madini wauze nje,mbao wauze china,mifugo,nguo nk.
Kundi kubwa lijikite kwenye uzalishaji kama ilivyokuwa enzi ya ukoloni uzalishaji ulikuwa ni Mkubwa sana.
Nje demand ni kubwa Sana shida hatuna sera, mwendazake alikazania zaidi marufuku.Uchumi na marufuku ni vitu viwili tofauti vinavyopingana.
 
Kabla ya kuzianzisha hizo gezaulole ni muhimu kupeleka vitu muhimu vipatikanayo mijini
 
Waweke mazingira wezeshi na masoko sio unakopa million zako unalima halafu mda wa mavuno watu wanajipangia bei wanayojiskia wao! Mambo ya kishoga kabisa!

Tunatamani kuwa wazalishaji ila swala la kulima halafu unavuna unamtegemea dalalali buguruni ndio hatutaki! Kuwepo na depots ambazo serikali itapokea mazao kwa wakulima wayafanyie standardization kisha mzigo upigwe export mkulima ale chake tena mapema sana sio kwa kuzungushana na hela miezi 6 wakati mzigo ushakabidhiwa! Wakenya wametuzidi hapo tu na online payments zifunguliwe watu wafanye biashara hata mitandaoni humo! Kodi za ajabu sijui youtube waondoe huo ujinga youtube is free sio kuanza kutozana kodi kipuuzi!

Tatizo la bongo ni ukiritimba tu na urasimu wa wenye vyeo kutaka wao wapige hela matokeo yake wanayumbisha michongo mingi mno!
 
Jf wote matajiri[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…