Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Bolt wana perce25
Bolt wanakata asilimia 25 ya pesa utakayopakia abiria,mfano abiria ame request route ya elfu 2 bolt ya kwao ni 500 bodaboda ya kwako ni 1500.
Mfano kwa siku umebeba abiria 20
20*1500.=30,000 na kwa bodaboda wa mjini kubeba abiria 20 kwa siku ni jambo la kawaida,Sasa ukiwa na kampuni tatu bolt,Uber na indrive kwa siku utakuwa unaingiza kiasi gani?
Hapo dereva kama hana matumizi mabaya anajenga fasta
 
Hiyo 10k ipo ila sio kwa kazi kama hizo

Nadhani ukienda kwenye viwanda vya steel unaweza ukapata hadi 15k

Ila changamoto yake ni kwamba unaambiwa kila mfanyakazi unayemkuta pale ujue hiyo ni siku yake ya kwanza hapo kiwandani.

Ukishachukua malipo ya 15k ukitoka hapo utachagua mwenyewe ukapatiwe huduma kati ya Amana au Muhimbili

Au usizi home ujiuguze mwenyewe
😂😂😂😂
 
Hiyo 10k ipo ila sio kwa kazi kama hizo

Nadhani ukienda kwenye viwanda vya steel unaweza ukapata hadi 15k

Ila changamoto yake ni kwamba unaambiwa kila mfanyakazi unayemkuta pale ujue hiyo ni siku yake ya kwanza hapo kiwandani.

Ukishachukua malipo ya 15k ukitoka hapo utachagua mwenyewe ukapatiwe huduma kati ya Amana au Muhimbili

Au usizi home ujiuguze mwenyewe
Daaah[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nakumbuka nilishawahi fanya kazi kiwanda cha kusaga chai yaani unaingia asubuhi saa 12 unatoka jioni saa 12 au saa zingine unatoka asubuhi kesho yake kwa ujira wa 2500/day na hakuna overtime.... Maisha ni safari mazee.
Aisee
 
2017 hiyo,

Nilienda kupiga deiwaka kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti na pamba (jina la kiwanda kapuni).

Vumbi lake ni noma, balaa...
Unavaa mask lakin ni hamna tu.

Ukitoka hapo macho, masikio, pua vimejaa vumbi la pamba.

Kikohozi kooh kooh kama chotee...
Nilikimbia mwenyewe baada ya siku 3.
Screenshot_20230118-034534.jpg
 
Mkuu najua ugumu na maumivu ya kuishi bila kazi hasa hapa mjini. Aisee pale kazi zipo huwezi kwenda pale ukakosa kazi lakini ndugu yangu UNA MANGUVU? Mkuu pale kuna ule mpigiko ambao utahisi dunia imekuacha, ni rahisi watu kusema ni bora hicho kidogo kuliko kukosa kabisa lakini nakuhakikishia kuwa aslimia zaidi ya 50 ya vibaruq pqle huacha kazi siku ya kwanza halafu aslimia 30 huvumilia hadi mwisho wa wiki.

Yupo jamaa yangu anaitwa Ngosha ni wale wasukuma wazee wa kazi nzito, aisee mbona aliingia pale akatema mzigo siku ya kwanza. We fikiria kupiga kazi ngumu haswa kwa masaa 12 halafu unarudi nyumbani na 2000 hapo hatujapigia nauli.
Na ubaya zaidi wa ile kazi haupati nafasi ya kusema unaweza kutoka pale ukapata muda wa kwenda kuzurula kutafuta vibarua sehemu nyingine.
Yamkini bahati ipo kwako na una huo moyo na uwezo wa mapambano nenda kajaribu bahati yako. Lakini kwa umbali wa Bunju sioni kama itakua na manufaa sana kwako maana hata nauli ya kurudi unaweza kukosa.

Iwapo unatokea Bunju nauli pekee kwa siku ni karibu 3000, ukiwa pale kiwandani tudanye umepiga chai ya buku na lunch ya 1500. Ukanywa maji ya jero. Halafu mwisho wa siku ukalipwa 4000 aisee itakua ni balaa. Piga hesabu zako vizuri mkuu na ninakuombea kheri kwa Mungu akusaidie katika mapambano haya.
Nimekuelewa mkuu
 
Back
Top Bottom