Mkuu najua ugumu na maumivu ya kuishi bila kazi hasa hapa mjini. Aisee pale kazi zipo huwezi kwenda pale ukakosa kazi lakini ndugu yangu UNA MANGUVU? Mkuu pale kuna ule mpigiko ambao utahisi dunia imekuacha, ni rahisi watu kusema ni bora hicho kidogo kuliko kukosa kabisa lakini nakuhakikishia kuwa aslimia zaidi ya 50 ya vibaruq pqle huacha kazi siku ya kwanza halafu aslimia 30 huvumilia hadi mwisho wa wiki.
Yupo jamaa yangu anaitwa Ngosha ni wale wasukuma wazee wa kazi nzito, aisee mbona aliingia pale akatema mzigo siku ya kwanza. We fikiria kupiga kazi ngumu haswa kwa masaa 12 halafu unarudi nyumbani na 2000 hapo hatujapigia nauli.
Na ubaya zaidi wa ile kazi haupati nafasi ya kusema unaweza kutoka pale ukapata muda wa kwenda kuzurula kutafuta vibarua sehemu nyingine.
Yamkini bahati ipo kwako na una huo moyo na uwezo wa mapambano nenda kajaribu bahati yako. Lakini kwa umbali wa Bunju sioni kama itakua na manufaa sana kwako maana hata nauli ya kurudi unaweza kukosa.
Iwapo unatokea Bunju nauli pekee kwa siku ni karibu 3000, ukiwa pale kiwandani tudanye umepiga chai ya buku na lunch ya 1500. Ukanywa maji ya jero. Halafu mwisho wa siku ukalipwa 4000 aisee itakua ni balaa. Piga hesabu zako vizuri mkuu na ninakuombea kheri kwa Mungu akusaidie katika mapambano haya.