Vibweka na vimbwanga vya mtaani kwetu...

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
77,270
Reaction score
111,361
1. Kinyozi maarufu ofisi yake ni chini ya mti

Heheh...najua wengi hamuwezi amini lakini pengine kinyozi wetu afahamikaye kwa jina la Bwana Makorokocho ndiye anayeongoza kwa kuwa na mkazi mkubwaaa kuliko mikasi yote ya kunyolea nywele.
Huwa nasikia tu eti huko mjini huwa mnanyolewa nywele zenu na mashine zinazotumia umeme, bahati mbaya huku kwetu umeme pekee tunaoujua ni ule uliopo kwenye gari la kituo cha afya Mangomango.



 
2. Shughuli za vigagula huwa zinapewa kipaumbele kuliko zile za maendeleo....
Watu wakisikia kuwa mtaa wa saba kuna mwanga kakamatwa basi wataacha shughuli zote hata kama walikuwa wanagegedana ili mradi tu waka-update jalada la mauzazuza kwenye bongo zao...
Kwa kujua udhaifu huo basi vigagula nao kuboresha biashara zao, kila uchwao hawaachi kufanya vimbwanga na machejo yao ili kuvutia wateja wengi...vigagula wengine huenda mbali hadi kunywa hadi damu za wanyama...


 
3. Hakuna daraja na huyu bwana ndiye daraja letu...


Kwa miaka mingi tumekuwa tukimtegemea huyu bwana kama kivuko kwenye hako kamto ketu kanakotutenganisha sisi wakazi wa Mangomango na wananchi wengine wa ng'ambo ya pili...


 
Blazamen sosoliso hahahahaaaaaa
 
Last edited by a moderator:
umkome mume wangu...............huyu ni saudari wakati ule ananifatilia nikiwa twaenda kuotesha kabichi Mlalo

Yaani babe Paloma huyu mpwa wangu Elli sijui kwa nini anapenda sana kunifananisha mie..

Ha ha ha watu8 huo mkasi kiboko.. Wanikumbusha miaka ile nilipokuwa shule ya msingi kuna gangwe mmoja alikuwa anajiiita Mzulu.. Alikuwa na minywele hiyo siku walimu walipotaka kumnyoa kibwenzi mkasi wa kawaida ukashindwa.. Ungekuwapo huu naona angepigwa kipara cha nguvu..
 
Last edited by a moderator:
4. Wababa wanajukumika hadi kwenye kutunza vichanga vyao


Mmmh!! najua wengi mtaanza na mguno kwa kuwa mjini kumeshawaharibu...Hebu hapa chini mshuhudieni mzee Topetope akiwa ananyonyesha mwanae wa kumi na mbili...
Hiyo chupa aitumiayo zililetwa mtaani kwetu na wazungu waliokuja kusaidia maisha ya mama wajawazito na watoto...


 

ha ha ha ha ha........! Kweli uswahilini kuna vituko
 
teh teh...huu hapo hauachi kitu juu ya kichwa yaani unatoa vyote

 
ha ha ha ha ha........! Kweli uswahilini kuna vituko

Hapo kuna bibi anayekaa nyumba ya mwisho kabisa kashabambikiwa kuwa ni mwanga na manyaunyau ndio huyo aonesha ushahidi wake...sasa subiria timbwili lake
 



Ngoja nijipange maana mie na my wife wangu marejesho tunamsubiria kijacho!!!
 
Last edited by a moderator:
Huyu bila shaka ni Bujibuji maana anafanana nae kwa kila kitu
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…