Vibweka na vimbwanga vya mtaani kwetu...

Vibweka na vimbwanga vya mtaani kwetu...

5. Hiki ndio kiota pekee cha maraha...


Hapa siongei mengi, hawa hapa chini ndio wadosi wa huku kwetu wakijiburudisha na moja moto moja baridi ndani ya viswimingi puli...


558796_378996815557192_2033976927_n.jpg

Hawa wadosi mbana afya zao utadhani wana kale ka ugonjwa
 
Hapo kuna bibi anayekaa nyumba ya mwisho kabisa kashabambikiwa kuwa ni mwanga na manyaunyau ndio huyo aonesha ushahidi wake...sasa subiria timbwili lake

hahahaaa...... Hapo hapata kalika wala kulika
 
haya haya asiekua na kwao shauri yake,kesho mie huyoooooooo Lushoto kwetu nikapumzike hadi Jumapili narudi kwa mkoloni, haya mwenye kunituma matunda anitume ila baridi ndio sitaweza kuwabebea,, naskia kuna baridi balaaa
hahahaa ngoja tumuulize .............weee saudari weee............
 
watu8 naona jinsi ulivyo mbunifu, hayo matete umeyasuka vizuri sana.
Lakini je ni salama? Usije ukawavunja wateja wako migongo
3. Hakuna daraja na huyu bwana ndiye daraja letu...


Kwa miaka mingi tumekuwa tukimtegemea huyu bwana kama kivuko kwenye hako kamto ketu kanakotutenganisha sisi wakazi wa Mangomango na wananchi wengine wa ng'ambo ya pili...


Funny-pics-from-Africa35.jpg
 
Last edited by a moderator:
watu8 naona jinsi ulivyo mbunifu, hayo matete umeyasuka vizuri sana.
Lakini je ni salama? Usije ukawavunja wateja wako migongo

Huo usafiri ni salama kabisa na nimewafungia hadi "shoko mzoba"....
 
4. Wababa wanajukumika hadi kwenye kutunza vichanga vyao


Mmmh!! najua wengi mtaanza na mguno kwa kuwa mjini kumeshawaharibu...Hebu hapa chini mshuhudieni mzee Topetope akiwa ananyonyesha mwanae wa kumi na mbili...
Hiyo chupa aitumiayo zililetwa mtaani kwetu na wazungu waliokuja kusaidia maisha ya mama wajawazito na watoto...


1013383_578567655508241_620427823_n.jpg

Mtoto ana afya...nimemependa
 
6. Huku kwetu kila mtu ana gari...


Mimi la kwangu nililiokota kipindi fulani hivi, sijui jina lake ila rangi yake ni jekundu...


544748_380815765375297_439914972_n.jpg

Ha ha ha haaa .....yaani wewe???
 
Back
Top Bottom