5. Hiki ndio kiota pekee cha maraha...
Hapa siongei mengi, hawa hapa chini ndio wadosi wa huku kwetu wakijiburudisha na moja moto moja baridi ndani ya viswimingi puli...
Hapo kuna bibi anayekaa nyumba ya mwisho kabisa kashabambikiwa kuwa ni mwanga na manyaunyau ndio huyo aonesha ushahidi wake...sasa subiria timbwili lake
Hah haha haha haha! ulipotea njia! Mimi nilikuwa mnadani Dosidosi nakula mbavu za mbuzi!! Pole sana!
umkome mume wangu...............huyu ni saudari wakati ule ananifatilia nikiwa twaenda kuotesha kabichi Mlalo
hahahaa ngoja tumuulize .............weee saudari weee............
3. Hakuna daraja na huyu bwana ndiye daraja letu...
Kwa miaka mingi tumekuwa tukimtegemea huyu bwana kama kivuko kwenye hako kamto ketu kanakotutenganisha sisi wakazi wa Mangomango na wananchi wengine wa ng'ambo ya pili...
4. Wababa wanajukumika hadi kwenye kutunza vichanga vyao
Mmmh!! najua wengi mtaanza na mguno kwa kuwa mjini kumeshawaharibu...Hebu hapa chini mshuhudieni mzee Topetope akiwa ananyonyesha mwanae wa kumi na mbili...
Hiyo chupa aitumiayo zililetwa mtaani kwetu na wazungu waliokuja kusaidia maisha ya mama wajawazito na watoto...
6. Huku kwetu kila mtu ana gari...
Mimi la kwangu nililiokota kipindi fulani hivi, sijui jina lake ila rangi yake ni jekundu...